OBREY CHIRWA ATWAA TUZO YA MCHEZAJI WA BORA WA MWEZI OKTOBA

Mshambuliaji wa Young Africans ya Dar es Salaam, Obrey Chirwa amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2017/2018.

Chirwa raia wa Zambia alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, beki Erasto Nyoni wa Simba na mshambuliaji Ibrahim Ajibu pia wa Young Africans alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za VPL zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu.


Mshambuliaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa Young Africans mwezi huo ikipata pointi saba katika michezo mitatu iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya sita iliyokuwepo mwezi Septemba hadi ya pili mwishoni mwa Oktoba.


Young Africans iliifunga Kagera Sugar mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja, pia Yanga iliifunga Stand United mabao 4-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.


Kiwango cha mchezaji huyo kilionekana pia katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba uliofanyika Oktoba 28, 2017 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Bao la Yanga lilifungwa na Chirwa, hivyo kwa mwezi huo alifanikiwa kuwa na kiwango cha juu katika kila mchezo ikiwa ni pamoja na kufunga.


Kwa upande wa Erasto naye alitoa mchango mkubwa kwa Simba uliowezesha timu hiyo kupata pointi nane katika michezo minne iliyocheza, akitoa pasi za mwisho za mabao nne, ambapo Simba ilishinda michezo miwili na kutoka sare miwili, huku Ajibu akitoa mchango mkubwa kwa Yanga ikiwa ni pamoja na kufunga mabao matatu na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.


Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu ni mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba).


Kampuni ya Vodacom, ambao ndiyo wadhamini wa ligi hiyo ina utaratibu wa kuwazadiwa wachezaji bora wa kila mwezi, huku pia mwisho wa msimu kukiwa na tuzo mbalimbali zinazohusu ligi hiyo, ambapo msimu wa mwaka 2016/2017 kulikuwa tuzo 16 zilitolewa kwa washindi wa kada mbalimbali. Chirwa atazawadiwa Sh milioni moja kwa kuibuka Mchezaji Bora wa Oktoba.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Michuzi

MCHEZAJI WA STAND UNITED AKABIDHIWA KITITA CHAKE KWA KUIBUKA MCHEZAJI BORA WA MWEZI OKTOBA WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA

Elias Maguli Mchezaji wa timu ya Stand United, amekabidhiwa hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni 1/= na wadhamni wakuu wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara(Vodacom Tanzania) kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi hiyo.
Mchezaji huyo alikabidhiwa hundi hiyo wakati wa mazoezi yaliyokuwa yanafanywa na timu yake katika viwanja vya JKM Park ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga hapo kesho.Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania,Ibrahim Kaude(kushoto)akimkabidhi Mchezaji...

 

2 years ago

Habarileo

Shomari Kapombe atwaa tuzo ya mchezaji bora

BEKI Shomari Kapombe wa timu ya Azam ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa Januari 2016.

 

1 year ago

Mwananchi

Griezmann atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka

Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, raia wa Ufaransa ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga msimu uliopita.

 

1 year ago

Mwananchi

Cristiano Ronaldo atwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa).

 

1 year ago

Zanzibar 24

Msuva mchezaji bora VPL Mwezi Oktoba

WINGA Simon Msuva wa Yanga SC amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Msuva alikuwa na washindani wa karibu wawili katika kinyang’anyiro hicho cha Oktoba ambao wote ni kutoka Simba. Wachezaji hao ni Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin.
Katika mwezi Oktoba ambao ulikuwa na raundi sita, Msuva aliisaidia timu yake kupata jumla ya pointi 14 huku akifunga mabao manne, na kutoa pasi tano za mwisho (assist).

Kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Msuva ambaye...

 

3 years ago

GPL

EDEN HAZARD ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA ENGLAND

Eden Hazard akiwa na tuzo yake ya mchezaji bora wa mwaka nchini England. KIUNGO wa Chelsea, Eden Hazard ndiye mchezaji bora wa mwaka nchini England. Hazard mwenye umri wa miaka 24, raia wa Ubelgiji, amefunga jumla ya mabao 18 katika mechi alizoichezea timu yake msimu huu kwenye michuano mbalimbali na kuisaidia Chelsea kutwaa Kombe la Capital One huku ikishika usukani katika msimamo wa Ligi Kuu ya England inayoelekea ukingoni.…...

 

1 year ago

Bongo5

Riyad Mahrez atwaa tuzo ya mchezaji bora wa BBC Africa

Riyad Mahrez wa Algeria anayechezea klabu ya Leicester City ya Uingereza amefanikiwa kushinda tuzo ya ‘BBC African Player of the Year’ inayotolewa na kituo cha habari cha BBC.

Mahrez amefanikiwa kushinda tuzo hiyo baada ya kusaidia klabu yake ya Leicester kushinda taji la ligi kuu msimu uliopita.

Mchezaji huyo amefanikiwa kuwabwaga wachezaji wengine waliokuwa wanawania tuzo hiyo akiwemo Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon (B’ Dortmund), Andre Ayew wa Ghana (West Ham United), Sadio Mane wa...

 

3 years ago

GPL

YAYA TOURE ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA MARA 4 MFULULIZO

Yaya Toure. KIUNGO wa Manchester City, Yaya Toure amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya CAF ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa mara ya nne mfululizo. Toure, 31, alitajwa kuwania tuzo hiyo baada ya kutoa mchango mkubwa kwa Manchester City kushinda Ligi Kuu ya England na kunyakua Kombe la Ligi. Pia aliisaidia Ivory Coast kufuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.
Toure alipambana na mshambuliaji kutoka Gabon...

 

2 years ago

Dewji Blog

Mohamed Tshabalala mchezaji bora wa mwezi Oktoba Simba Sport Club

Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015.

Mshindi wa mwezi wa Oktoba, 2015 ni Mohamed Hussen Tshabalala ambapo alipigiwa kura nyingi na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka la Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Rais wa Simba Evans Aveva alisema “Uongozi, wanachama na wapenzi wa...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani