POLISI : NONDO ALIJITEKA,ALIKWENDA IRINGA KWA MPENZI WAKE....ATAFIKISHWA MAHAKAMANI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo kwa kosa la kutoa taarifa za uongo na kujiteka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Machi 13, 2018 Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema Nondo ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.
Alisema uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi kuhusu taarifa za kutekwa kwa Abdul Nondo umetoa na kuwa mwanafunzi huyo alijiteka mwenyewe.
Mambosasa alisema Nondo alikamatwa huko Mafinga Iringa akiendelea na shughuli zake na kusema hakuripoti sehemu yoyote kuhusu kutekwa kwake na kudai kuwa wamebaini kijana huyo alikwenda kwa mpenzi wake ambaye alikuwa akiwasiliana naye mara kwa mara. 
"Pengine alitaka kuzua hilo ili kujipatia umaarufu ila upelelezi uliendelea kubaini kuwa mwanafunzi huyo alikwenda Iringa kwa mpenzi wake ambaye alikuwa akiwasiliana naye mara kwa mara akiwa njiani kuelekea Iringa hii ni baada ya kufanya uchunguzi wa kisayansi na kubaini muda ule aliosema ametekwa simu yake imeendelea kuonyesha mawasiliano aliyokuwa anafanya na huyo binti ambaye alikuwa amemfuata" ,alieleza.
Mambosasa amesema kuwa walipomkamata walikuwa na mashaka kuwa huenda akawa amepatwa na ugonjwa wa malaria ya kichwa iliyopelekea kufanya hayo na kudai kuwa alipelekwa hospitali na kupimwa na kuonekana kuwa mzima asiye na matatizo yoyote ya kiakili. 
"Alikuwa ni mzima wa afya njema na haya aliyafanya kwa makusudi kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe, jeshi la polisi limebaini kuwa mwanafunzi huyo alikuwa huru baada ya kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, alisafiri akiwa huru na akafika Iringa akiwa salama, kwa hiyo ni uzushi mtupu uliokuwa na malengo ya hovyo lakini kuna watu wengine walilishabikia jambo hili wengine huwezi kuamini kwa nafasi zao walilishabikia jambo hili la hovyo mtu kujizushia jambo"alisema Mambosasa 
Nondo alidaiwa kutoweka Machi 6, 2018 lakini alijisalimisha mikononi mwa polisi wilayani Mafinga, Iringa Machi 7.
Baada ya kujisalimisha alifunguliwa jalada la uchunguzi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire ambaye aliwaeleza wanahabari kuwa uchunguzi huo unalenga kubaini iwapo ni kweli alitekwa au alitoa taarifa za uongo kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi kuvuruga amani.
Machi 10, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliliomba Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa litakapomalizana na Nondo limrejeshe jijini Dar es Salaam ili na yeye aanzishe uchunguzi wake kwa mwanafunzi huyo.

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

BBCSwahili

Mahakamani kwa kumchinja mpenzi wake

Kesi imeanza ya mwanamume anayedaiwa kumuua na kumkatakata vipande mpenzi wake na kuwatumia wanasiasa vipande hivyo kwa posta.

 

12 months ago

Zanzibar 24

Aliyemuua mpenzi wake kwa kumchinja atiwa mikononi mwa polisi

JESHI la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Musuguri Sylvester (29), mkazi wa Sinza, kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake.

Hayo yalisemwa jijini hapa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Kamishna wa Polisi, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kamanda Sirro alisema tukio hilo lilitokea Machi 31, mwaka huu saa saa nne usiku katika maeneo ya Sinza Shekilango jijini Dar es Salaam.

Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa...

 

9 months ago

Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Bayern Munich akamatwa na polisi kwa kumpiga mpenzi wake

Mshambuliaji wa Bayern Munich, Kingsley Coman anashikiliwa na polisi kutokana na kumfanyia vurugu mpenzi wake wa zamani.

 

1 week ago

Michuzi

POLISI DAR WABAINI MWANAFUNZI ALIYEDAI KUTEKWA KUMBE ALIKUWA KWA MPENZI WAKE

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

*Mambosasa asema watamchukulia hatua za kisheria, atoa onyo kali
Na Said Mwishehe, Globu ya jamiiKAMANDA wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Abdul Nondo(24), aliyedai kutekwa  na watu wasiojulikna siku za karibuni uchunguzi wao umebaini kumbe alikwenda kwa mpenzi wake mkoani Iringa.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mambosasa amefafanua Machi 6 mwaka huu ,kuanzia...

 

1 month ago

Malunde

MWANDISHI WA HABARI WA MWANANCHI AKAMATWA NA POLISI MAHAKAMANI IRINGA


Mwandishi wa gazeti la Mwananchi mkoani Iringa, Geofrey Nyang'oro amekamatwa na polisi.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), Frank Leonard ameiambia Malunde1 blog kuwa mwandishi huyo wa habari amekamatwa na polisi wakati akiwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa leo Alhamis Februari 15,2018.
Amesema wanaendelea kufuatilia sababu za kukamatwa kwake na yupo chini ya ulinzi kwa mahojiano.

"Ni kweli tumepata taarifa za kuwa Nyang'oro amekamatwa kwa mahojiano na mkuu wa...

 

1 year ago

Mwananchi

Polisi anayedaiwa kumuua mpenzi wake adakwa Dar

Polisi mkoani Tanga  imefanikiwa  kumkamata askari  wake, Michael Komba anayedaiwa  kumuua askari mwenzake wa kike, Elizabeth Stephano aliyekuwa  mpenzi  wake.

 

1 year ago

Zanzibar 24

Aliyemchoma moto mpenzi wake mikononi mwa polisi

Jeshi la polisi Zanzubar limefanikiwa kumkamata Omar Said mkaazi wa Paje  akikabiliwa na tuhuma za kumchoma moto Samira Abasi Amir na kupata majaraha makubwa.

Tukio hilo la kumkamata kijana huyo limetokea majira ya saa nne Leo Asubuhi huko katika manispaa ya mji wa Zanzibar wakati mtuhumiwa huyo akijaribu kukimbia.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wamelimelipongeza jeshi la Polisi kwa kuweza kumdhibiti mtuhumiwa huyo alietenda kesi ya udhalilishaji.

Mwanahabari wetu yupo katika...

 

2 days ago

Malunde

NONDO ASAFIRISHWA KWENDA IRINGA

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam UDSM, Abdul Nondo amesafirishwa usiku kupelekwa Iringa na sasa yuko Mahakama ya wilaya. Wakili wake Jebra Kambole amethibitisha.

 

2 days ago

Zanzibar 24

Abdul Nondo kufikishwa mahakamani leo

Wakili wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini TSNP  Jebra Kambole leo Machi 21, 2018  amesema kuwa Abdul Nondo atasomewa mashtaka huko mkoani Iringa asubuhi hii Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi.

 “Watanzania taarifa zilizonifikia hivi punde kutoka kwa vyanzo vya kuaminika huku tukisubiri kesi yetu kuitwa mbele ya Jaji SAMEJI Mahakama Kuu DSM, kijana Abdul Nondo yupo Iringa akisubiri kusomewa mashtaka mkoani humo” Wakili Kambole.

Mnamo Machi 6, 2018 Abdul Nondo alipotea...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani