POLISI DAR WABAINI MWANAFUNZI ALIYEDAI KUTEKWA KUMBE ALIKUWA KWA MPENZI WAKE

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

*Mambosasa asema watamchukulia hatua za kisheria, atoa onyo kali
Na Said Mwishehe, Globu ya jamiiKAMANDA wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Abdul Nondo(24), aliyedai kutekwa  na watu wasiojulikna siku za karibuni uchunguzi wao umebaini kumbe alikwenda kwa mpenzi wake mkoani Iringa.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mambosasa amefafanua Machi 6 mwaka huu ,kuanzia saa sita usiku zilianza kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwanafunzi huyo ametekwa na watu wasiojulikana na kusababisha hofu kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla.
Kamanda Mambosasa amesema kutokana na taarifa hizo, Polisi walianza kufuatilia ili kubaini ukweli wake ikiwa pamoja na kufungua jalada la uchunguzi lenye kumbukumbu namba DSM/KIN/CID/P.E/51/2018.
"Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Machi 7 mwaka huu tulipata taarifa kutoka kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, mwanafunzi huyo ameonekana mkoani Iringa katika Wilaya ya Mafinga akiwa mwenye afya njema.
"Tena anajitambua  na akiendelea na shughuli zake na wala hakuna mahali popote ambapo ametoa taarifa kwenye kituo cha Polisi kuwa amtekwa.Jeshi letu la Polisi kwa kushirikiana na wenzetu wa Iringa tulifanya uchunguzi na kubaini  Nondo hakutekwa bali alijiteka kwa lengo la kutafuta umaarufu kwa jamii,"amesema Mambosasa.
Ameongeza baada ya kuendelea na uchunguzi wao kutokana na taarifa za tukio hilo, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wamebaini mwanafunzi huyo aliyedai alitekwa kumbe alikwenda kwa mpenzi wake."Wakati tunafuatilia tukabaini mawasiliano kati yake na huyo mpenzi wake ya mara kwa mara wakati akiwa njiani akielekea Iringa,"amesema Mambosasa.
Amefafanua Polisi pamoja na kuchunguza mambo mbalimbali kuhusu mwanafunzi huyo walitumia utaalamu wao kufuatilia mawasiliano yake kwa kipindi ambacho anadai alikuwa ametekwa lakini walichoona alikuwa anawasiliana zaidi na mpenzi wake.
Pia amesema hata baada ya mwanafunzi kupelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa alipimwa na kubaini hakuna aina yoyote ya kinywaji ambacho alipewa wala hakuwa amepewa dawa za usingizi."Hakuna na majeraha ya aina yoyote kwenye mwili wake,"amesisitiza Mambosasa na kuongeza "Uchunguzi umebaini alikuwa kwa mpenzi wake na alimua kutoa taarifa hizo kwa lengo la kujitafutia umaarufu kwa umma".
Kutokana na mazingira hayo Mambosasa amesema kwa kuwa mwanafunzi huyo hakuwa ametekwa watamchukulia hatua za kisheria kama wahalifu wengine huku akitoa onyo kuwa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam halitavumilia mtu anayejitafutia umaarufu kwa njia ya aina hiyo na nyingine zinazofanana na hiyo.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Bongo5

Huddah amkana mwanaume aliyedai kuwa mpenzi wake, aliyemtangazia Diamond dau la $40,000 ili amuache Zari

Baada ya mwanaume aliyedai kuwa ni mpenzi wa Huddah kujitokeza na kuupinga uhusiano wa Diamond na Zari The Boss Lady wa Uganda, Socialite wa Kenya Huddah Monroe naye ameibuka na kukana kuwa hajawahi kuwa na uhusiano na njemba huyo. Huddah alipost ujumbe mrefu Instagram ambao baadae aliufuta, wa kuelezea jinsi alivyokutana na jamaa huyo aitwaye […]

 

2 weeks ago

Malunde

MWANAFUNZI WA UDSM ANAYEDAIWA KUTEKWA NA WASIOJULIKANA AFIKISHWA POLISI


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Juma Bwire akizungumza
MWENYEKITI wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amefikishwa makao makuu ya Polisi Mkoa wa Iringa Mjini Iringa kwa mahojiano zaidi wakati jeshi hilo likiendelea na uchunguzi wa taarifa zake za kutekwa na watu wasiojulikana mapema wiki hii.

Mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu wa kitivo cha Siasa na Utawala cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha Jumanne usiku akiwa jijini Dar...

 

2 months ago

Malunde

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA SUA AMUUA MPENZI WAKE KWA KUMNYONGANa Amina Juma, Mwananchi
Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamsaka mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Mwita Marwa (30) kwa tuhuma za kumuua kwa kumnyonga mpenzi wake Kibua Adam (39) baada ya kutokea kutokuelewana kati yao.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema tukio hilo lilitokea Januari 22 mwaka huu katika eneo la Modeco Manispaa ya Morogoro ambapo mwanafunzi huyo alitoweka baada ya tukio...

 

4 years ago

CloudsFM

POLISI AMRUBUNI MWANAFUNZI KUFANYA NAYE MPENZI,AMWACHA CHUMBANI KWAKE,NYUMBA YAKE YAUNGUA MOTO,MWANAFUNZI AFARIKI DUNIA

Wananchi wa Mlangali, Ludewa wakiwa wamekizingira kituo cha polisi Mlangali mara baada ya kuipeleka maiti ya mtoto aliyeteketea kwa moto katika kituo hicho.KIONGOZI wa mbio za mwenge Kitaifa awatuliza wananchi wa Mlangali wilaya ya Ludewa ambao baadhi yao waliandamana kituo cha polisi kushinikiza kutolewa kwa askari polisi aliyedaiwa kusababisha kifo cha mtoto ili auwawe.Kiongozi huyo aliwaomba wananchi wa Mlangali kutokubali kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na...

 

1 year ago

Mwananchi

Polisi anayedaiwa kumuua mpenzi wake adakwa Dar

Polisi mkoani Tanga  imefanikiwa  kumkamata askari  wake, Michael Komba anayedaiwa  kumuua askari mwenzake wa kike, Elizabeth Stephano aliyekuwa  mpenzi  wake.

 

12 months ago

Malunde

POLISI DAR YAMKAMATA KIJANA ALIYECHINJA MPENZI WAKE NA KUMUWEKA KWENYE DIABA

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limemkamata mtuhumiwa Musuguri David (29) anayedaiwa kumuua mpenzi wake Samira Masoud (34) kwa kumchinja kisha mwili wake kuwekwa katika diaba/jaba la maji kisa wivu wa mapenzi maeneo ya Kibamba.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kamishna Simon Sirro amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kutenda kosa hilo mnamo Machi 7 mwaka huku akidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kumfumania aliyekuwa mpenzi wake...

 

4 years ago

CloudsFM

POLISI IRINGA YASEMA MWANAFUNZI WA RUCO ALIKUWA ANATEMBEA HUKU MWILI UKIWAKA MOTO

Mwili wa Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College - RUCO) umesafirishwa jana kuelekea mkoani kwao kilimanjaro kwa mazishi.Wanafunzi kadhaa wa chuo hicho na baadhi ya wananchi wa manispaa ya Iringa waliogusa na tukio hilo walijitokeza katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako shughuli ya kuuga mwili huo ilifanyika.Jeshi la Polisi mkoani iringa linawashikilia watu wanne...

 

12 months ago

Zanzibar 24

Aliyemuua mpenzi wake kwa kumchinja atiwa mikononi mwa polisi

JESHI la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Musuguri Sylvester (29), mkazi wa Sinza, kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake.

Hayo yalisemwa jijini hapa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Kamishna wa Polisi, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kamanda Sirro alisema tukio hilo lilitokea Machi 31, mwaka huu saa saa nne usiku katika maeneo ya Sinza Shekilango jijini Dar es Salaam.

Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa...

 

9 months ago

Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Bayern Munich akamatwa na polisi kwa kumpiga mpenzi wake

Mshambuliaji wa Bayern Munich, Kingsley Coman anashikiliwa na polisi kutokana na kumfanyia vurugu mpenzi wake wa zamani.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani