POLISI SHINYANGA WANASA WANNE WAKISAFIRISHA BANGI KWA COASTER

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linawashikilia watu wanne kwa tuhuma ya kukamatwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi kwenye viroba vitano ikiwa na uzito wa kilo 98 kutoka kata ya Kagongwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwenda Jijini Dar es salaam.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Aprili 16, 2018,Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa polisi Simon Haule alisema watu hao walikamatwa Aprili 15,2018 majira ya saa 12 asubuhi katika geti la maliasili barabara ya Kahama - Tinde kata ya Itogwanholo wilaya ya Kipolisi Msalala. 
Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Simon Juma Kashindye (46) mkazi wa Nyanshimbi Shinyanga vijijini, Lameck Nicombolwe (44) Kulwa Nelson (21), na Shabani Nurdin(20), wote hao watatu wakiwa wakazi wa Jijini Dar es salaam.
Alisema watu hao walikamatwa wakisafirisha bangi hiyo kwa kutumia gari lenye namba za usajili T 872 CVS Coaster mali ya Precabi mkazi wa Dar es salaam. 
“Bangi hii kama mnavyoiona imefungwa kwenye viroba 5 na ina uzito wa kilo 98 na watuhumiwa hawa walikuwa wakisafirisha kwenda Jijini Dar es salaam kwa kutumia gari hiyo ya abiria, na tunaendelea kuwashikilia kwa mahojiano zaidi na uchunguzi ukikalimika watafikishwa mahakamani kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema Haule. 
“Na uchunguzi ukikamilika na watu hawa watafikishwa mahakamani kuchukuliwa hatua kali za kisheria, na mahakama ndiyo itatoa amri ya bangi hii kuharibiwa, nasi ndipo tutakapoiteketeza kwa moto,” aliongeza. 
Naye mmoja wa watuhumiwa hao Lameck Nicombolwe ambaye ni dereva wa gari hilo alisema wao walikodiwa kuleta msiba katika Kata hiyo ya Kagongwa, ndipo wakapata tenda ya kupakia bangi hiyo na kuambiwa kuwa ni tumbaku, lakini walishangaa mhusika wa mzigo huo ghafla anashuka kwenye gari na kutokomea huku wao wakikamatwa. 
Aidha kufuatia tukio hilo Kamanda alitoa wito kwa wananchi mkoani Shinyanga kuachana na tabia ya kujihusisha na biashara haramu pamoja na kushirikiana na jeshi hilo kutoa taarifa za wahalifu ili wapate kushughulikiwa mapema na mkoa ubaki kuwa salama.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi Simon Haule akielezea namna walivyokamata dawa za kulevya aina ya Bangi.Askari polisi wakiangalia bangi hiyoAskari polisi wakifungua viroba vitano walivyo vikamata vikiwa na bangi.Bangi ikiwa kwenye kiroba.Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi Simon Haule akihoji watuhumiwa waliokamatwa na bangi.Lameck Nicombolwe ambaye ni dereva wa gari hilo akijiteteaWatuhumiwa waliokamatwa na madawa hayo ya kulevya aina ya bangi wakijieleza.Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kamishina msaidizi wa Polisi Simon Haule, akionyesha gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T. 872 CVS Mali ya Precabi mkazi wa Jijini Dare es salaam ambayo imetumika kusafirisha bangi.Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi Simon Haule akitoa taarifa hiyo ya kukamata bangi kwa vyombo vya habari.Baadhi ya waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga wakiwa katika wakichukua matukioBaadhi ya waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga wakiwa wakiandika dondoo.Picha zote na Marco Maduhu - Shinyanga News Blog

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

4 years ago

Mwananchi

Polisi wanasa magunia 20 ya bangi Longido

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na askari wa Kampuni ya Jumuiya ya Jamii wamefanikiwa kukamata magunia 20 ya dawa za kulevya aina ya Bangi yaliyotelekezwa kwenye Kijiji cha Olteres wilayani Longido.

 

4 years ago

Tanzania Daima

Wanaswa wakisafirisha bangi kwenye basi

JESHI la Polisi mkoani hapa linawashikilia watu watano kwa kosa la kukutwa wakisafirisha bangi magunia matano katika gari la abiria aina ya Toyota Coaster. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini...

 

3 weeks ago

Malunde

RAIS MAGUFULI: SITAKI JESHI LA POLISI LITUMIKE KUFYEKA BANGI ....KWA NINI MKAFYEKE BANGI?

 Rais John Magufuli ameagiza askari kuwakamata wazee, wanawake, vijana na watoto wa maeneo yanapobainika mashamba ya bangi akieleza kuwa wakikamatwa watasema ukweli na watazifyeka wenyewe.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Aprili 7 wakati akizungumza na wakazi wa Arusha Uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya kuzindua kituo cha polisi na nyumba 31 za polisi.
Rais Magufuli amesema kazi ya kufyeka mashamba ya bhangi ni ya wananchi wenyewe wanaolima bhangi hizo na kwamba askari hawakuajiriwa kwenda...

 

5 months ago

Zanzibar 24

Wachina wakamatwa wakisafirisha mawe yanayosadikika kuwa na madini Shinyanga

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu sita wakiwemo raia wanne wa China kwa kosa la kusafirisha na kuhifadhi mawe yanayosadikiwa kuwa na madini kinyume cha sheria. Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Simon Haule watuhumiwa walikamatwa Disemba 6,2017 saa saba mchana katika kata ya Ibadakuli wilaya ya Shinyanga na askari wa usalama barabarani wakati wakikagua roli lenye namba za usajili T 209 AVH lililokuwa limebeba mawe hayo yaliyochongwa mfano wa...

 

2 years ago

GPL

MEXICO YAHALALISHA BANGI ITUMIKE KWA WATU WANNE TU

Mahakama Kuu nchini Mexico. Mwanaharakati anayeunga mkono matumizi ya bangi nchini Mexico, Lucha Libre aliyevaa Maski, akishangilia mara baada ya Mahakama Kuu nchini humo kuruhusu matumizi ya bangi. Mmoja wa wavuta bangi raia wa Mexico akivuta msokoto wa bangi nje ya jengo la Mahakama Kuu ya nchi hiyo jana. Mmoja wa wanaharakati na watumiaji wa zao la mmea wa bangi.… ...

 

2 years ago

Mwananchi

Shinyanga wanasa wahamiaji haramu 283

  Idara ya Uhamiaji imewakamata watu 283 wanaotuhumiwa kuingia nchini kinyumea cha sheria na 103 kati ya hao tayari wamefukuzwa nchini.

 

2 years ago

Channelten

Watuhumiwa wanne wa Ujambazi waliohusika na mauaji ya polisi wanne CRDB wameuwawa na Polisi

mbade2

Watuhumiwa wanne wa Ujambazi waliohusika na mauaji ya polisi wanne na kupora bunduki 4 aina ya SMG katika tukio lililotokea Mbande katika tawi la benki la CRDB hivi karibu wameuwawa na Polisi na kupata silaha nyingine aina ya SMG ambayo iliporwa na majambazi hao na kufanya idadi ya silaha zilizopatikana kufikia nne.

Kamishna wa Polisi kanda Maalum DSM Simon Sirro amesema katika Operesheni ya kuwasaka majambazi hao,walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye aliwapeleka katika Msitu wa...

 

2 years ago

Mtanzania

Polisi yanasa 9 kwa kulima bangi

bangiNa WALTER MGULUCHUMA –

SUMBAWANGA

 

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, George Kyando, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Pascha Ramadhani (48), Elisi Ulaya (45), Wilbeth Ramadhani na George Kapombe (43).

Wengine ni Radislaus Ntinda (33), Festus Misala (38), Cletus Kanyama (27), Lodrick Kanyama (56) na Flowin Misali (25). Watuhumiwa wanatarajia kupandishwa kizimbani baada ya upelelezi kukamilika.

Alisema pamoja na operesheni hiyo, ushirikiano mzuri kutoka kwa...

 

1 year ago

Dewji Blog

Polisi Arusha yatoa onyo kwa wanaolima bangi

Jeshi la Polisi mkoani hapa lipo kwenye mkakati wa kuwachukulia hatua viongozi wote wanaoishi au kufanyia kazi katika maeneo ambayo yatabainika wananchi wa maeneo yao wanalima bangi bila wao kuwachukulia hatua zozote au kutoa taarifa kwa vyombo husika.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu kamishna (DCP) Charles Mkumbo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya operesheni iliyofanyika katikati ya wiki iliyopita katika kijiji cha Kismiri Juu, kata ya...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani