- 1 Anachofikiria Edo Kumwembe Kuhusu Yanga Kuomba Ichangiwe Pesa
- 2 Simba Yaamua Kukaa Kimya
- 3 Timu Ya Simba Yaweka Kambi Morogoro
SIKU KAMA YA LEO
Apr 26, 2017POPULAR ON YOUTUBE
POLISI WATWANGANA RISASI TANGA...MMOJA AFARIKI

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), ambaye alikuwa lindo, jana alfajiri aliwashambulia mwenzake, raia na kutishia kumfyatulia risasi mkuu wake nje ya benki ya CRDB jijini Tanga na jitihada za kumdhibiti zikasababisha kifo chake.
Jeshi la Polisi limeahidi kutolea ufafanuzi tukio hilo mara baada ya kukamilisha uchunguzi wake.
Wakisimulia jinsi tukio hilo lilivyokuwa, wananchi wanaoendesha shughuli zao jirani na benki hiyo iliyo Tarafa ya Ngamiani, walisema mashambulizi ya risasi yalianza saa 11.30 alfajiri baada ya kusikika kelele ya msichana eneo la kuegeshea magari ya benki hiyo.
Walisema kelele hizo zilisababisha mmoja wa askari aliyekuwa zamu kuzunguka kushuhudia nini kinaendelea, ndipo akamkuta askari mwenzake aliyekuwa naye zamu akiwa na msichana, huku msichana huyo akipiga kelele.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, askari aliyefahamika kwa jina la Valerian Temba alimyang’anya mwenzake silaha aliyokuwa ameshika na kisha kumfyatulia risasi iliyomjeruhi mguuni.
“Mara askari waliokuwa wakilinda benki ya NMB ya jirani wakakimbilia eneo la tukio, lakini nao wakatishiwa kupigwa. Ndipo wakampigia simu mkubwa wao wa FFU ambaye alikuja haraka na kukuta tafrani hiyo, ”alisema mtu aliyejitambulisha kwa jina la Charles Mathias.
Shuhuda huyo alisema wakati tafrani hiyo ikiendelea, askari walizungushia kamba eneo lote la benki ya CRDB kama ishara ya kuzuia watu wasipite kwa kuwa Temba alikuwa ameelekeza bunduki akitishia kuua yeyote ambaye angemsogelea.
Mashuhuda hao walisema, mkuu wao FFU aliwasili na kumsihi askari huyo kusalimisha silaha lakini hakufanikiwa.
“Yule askari alisisitiza kuwa angemuua hata yeye (mkuu wake) endapo angemfuata,” alisema
Mashuhuda hao wameeleza kuwa askari huyo alianza kurusha risasi hovyo zilizoharibu magari na baadhi ya nyumba za jirani, ndipo askari wenzake walipoamua kumdhibiti ili asisababisha madhara zaidi.
Inadaiwa kuwa askari wenzake walifyatua risasi na moja ikamjeruhi na alifariki baadaye wakati akipata matibabu.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo, walisema waliposikia milio ya risasi walidhani ni sehemu ya mazoezi ya polisi ambao Jumamosi walikuwa wakiadhimisha Siku ya Familia.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe alisema atatolea maelezo ya tukio hilo mara baada ya jeshi la polisi kukamilisha uchunguzi kwa mujibu wa taratibu za kijeshi.
“Watu wanaeleza wanavyoona, lakini niseme tu kwamba fanyeni subira hadi tutakapokamilisha uchunguzi kama ambavyo taratibu za kijeshi zilivyo. Nitawaeleza kila kitu hakuna kitakachofichwa,” alisema Bukombe.Na Burhani Yakub, Mwananchi
Malunde
Habari Zinazoendana
2 years ago
StarTV16 Feb
Askari polisi aliyepigwa risasi na majambazi Tanga afariki
Askari wa jeshi la polisi Koplo George Braiton aliyepigwa risasi na majambazi wakati akikabiliana nao katika tukio la ujambazi lililotokea barabara ya sita na saba jijini Tanga amefariki dunia.
Koplo Braiton amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Tanga,Bombo, akiwa na watu wengine wawili waliopigwa risasi katika tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ACP.Mihayo Msikhela amesema kuwa bastola ilitumika kupoteza uhai wa Koplo George Braiton wa kituo cha...
4 years ago
Mwananchi03 Oct
Wanajeshi, polisi watwangana risasi
4 weeks ago
Malunde31 Mar
ALIYEPIGWA RISASI NA POLISI DAR AFARIKI

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema walipata taarifa kwamba kuna mtu anafanya matukio mbalimbali ya uhalifu wa kutumia silaha katika maeneo ya Mbagala Kibondemaji.
“Baada ya taarifa...
2 years ago
Ippmedia19 Jun
Mtu 1 anayesadikiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi mkoani Tanga
Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi sugu Benjamini Wallace Singano aliyekuwa na silaha ya kivita aina ya AK 47 yenye magazini mbili zinazoingia kila mojawapo risasi 30 ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa akijariribu kuwatoroka askari polisi mara baada ya kukamatwa na kuelezea kuwa yeye na wenzake walikuwa wakienda kufanya uhalifu.
Day n Time: Jumamosi saa 2 usikuStation: ITV
4 years ago
Habarileo03 Oct
Polisi, JWTZ watwangana
ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na askari Polisi wameshambuliana hadharani katika Stendi ya Mabasi mjini hapa na kusababisha uvunjivu wa amani na baadhi yao kujeruhiwa. Katika vurugu hizo za juzi saa 11 jioni zilizosababisha shughuli mbalimbali kusimama ikiwemo maduka kufungwa, askari kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.
3 years ago
Tanzania Daima06 Dec
Polisi, raia watwangana baada ya kufumaniana
WAKAZI wawili wilayani hapa, wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga baada ya kujeruhiwa katika mapigano kati yao na askari Polisi, baada ya kumshika ugoni mmoja wa...
2 years ago
StarTV07 Nov
Mlinzi mmoja afariki, mmoja ajeruhiwa Geita
Walinzi wawili wanaolinda katika baa ya Wacha Waseme na Lunguya mjini Geita wamejeruhiwa na vitu vyenye ncha kali ambavyo vimesababisha kifo cha mlinzi mmojawapo.
Mlinzi huyo aliyejulikana kwa jina moja la Michael amefariki dunia baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita.
Tukio hilo limejiri majira ya usiku wakati walinzi hao wakiwa wamelala katika lindo ambapo watu wasiojulikana wanadaiwa kuvamia na kuwashambulia na kuvinjwa katika baa ya lunguye na kuiba shilingi elfu tisini...
1 year ago
Michuzi
JESHI LA POLISI MKOANI KIGOMA LAKAMATA RISASI 408 ZILIZOKUWA ZIKIMILIKIWA NA MTU MMOJA WILAYANI KASULU MKOANI KIGOMA
JESHI la polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kukamata risasi 408 za bunduki zilizo kuwa zikimilikiwa na Mtu mmoja ambaye jina lake halikutajwa mkazi wa Kijiji cha Makere Wilayani kasulu Mkoani Kigoma.
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake leo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma,DCP Fredinand Mtui alisema mnamo tarehe 5Desemba majira ya 08:20 huko maeneo ya makere Center katika kijiji cha Makere askari wakiwa doria walipokea taarifa kutoka...
1 year ago
MillardAyo20 Dec
AyoTVMAGAZETI: Polisi na raia watwangana, Kaburi la Faru John layeyuka
Kila siku AyoTV inakuletea uchambuzi wa magazeti ya Tanzania, Ungana na Alice Tupa ameshazisoma zote kubwa za leo December 20 2016 ikiwa ni pamoja na Polisi na raia watwangana, Kaburi la faru John layeyuka VIDEO: Maxence Melo baada ya kupata dhamana Kisutu
The post AyoTVMAGAZETI: Polisi na raia watwangana, Kaburi la Faru John layeyuka appeared first on millardayo.com.