RAIS DK. ALI MOHAMED SHEIN ATUNUKU NISHANI KWA WATU 74


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewatunuku Nishani ya Mapinduzi na Nishani ya Utumishi uliotukuka watunukiwa 74.

Hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar ambayo imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa vyama na serikali pamoja na wananchi ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa kutokana na uwezo wake aliopewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Mambo ya Rais namba 5 ya mwaka 1993, na kama ilivyotangazwa katika Tangazo la Kisheria namba 5 la mwaka 2018 kupitia Gazeti Rasmi la Serikali la tarehe 9 Januari 2018 ametunuku Nishani za Mapinduzi 43 na Nishani za Utumishi wa Umma, Maafisa wa Idara Maalum za SMZ na Wananchi mbali mbali.

Nishani ya Mapinduzi hutolewa kwa mtu ambaye aliasisi au alishiriki au aliyatukuza na aliyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambapo Mtunukiwa huwa ni Kiongozi au mtu mwengine aliyehai au aliyefariki ambaye aliiletea sifa Zanzibar katika fani mbali mbali na kuonesha maadili mema ya kusifika na kuigwa.

Nishani ya Utumishi uliotukuka inatolewa kwa Mtumishi wa Umma au Idara Maalum za SMZ aliyehai au aliyefariki ambaye ametimiza Utumishi wake kwa muda wa miaka isiyopungua 20 mfululizo na kwa Mtumishi wa Idara Maalum za SMZ miaka isiyopungua 20 ya kuwa Ofisa na katika kipindi chote hicho amekuwa na tabia njema.

Mtumishi huyo awe ametumikia Taifa kwa Uzalendo wa hali ya juu na kufanya kazi kwa kujitolea, uwajibikaji, uadilifu, ujasiri na umakini katika kusimamia majukumu na utendaji kazi.

Katika sherehe hizo Nishani ya Mapinduzi imetunukiwa kwa makundi ya Viongozi na Wananachi wenye sifa Maalum ambao ni Jaji Augostino M. Ramadhan, Marehemu Col  mstaafu Juma Abdalla Saddala (Mabodi), Bwana Ramadhan Abdalla Shaaban, Bwana Ali Ameir Mohammed, Bwana Ali Mohammed Shoka, Marehemu Kassim Ali Kassim, Bwana Rajab Baraka Juma, Bwana Khamis Ahmada Mussa, Marehemu Dk. Ishau Abdalla Khamis.

Bwana Ali Salum Ahmed, Marehemu Shema Mohamed Sheha, Bwana Issa Mohamed Suleiman, Marehemu Enoch Timoth Bilal, Bibi Fatma Said Ali, Damian Z. Lubuva, Mwalimu Haji Ameir, Bwana Mbarouk Rashid Omar, Bwana Issa Ahmed Othman, Bwana Mohamed Khamis Abdalla, Bwana Abdulsalam Issa Khatib, Marehemu Christabella Susan Majaaliwa, Marehemu Shaha Kombo Shaha, Marehemu Amina Said Ferouz.Bwana Ramadhan Abdalla Ali.

Marehemu Abdulrahman Mwinyi Kombo, Bwana Hassan Mussa Takrima, Marehemu Zaina Khamis Rashid, Marehemu Mosi Jecha Pili, Bwana Maulid Salum Abdalla, Bwana Haji Machano Haji, Marehemu Rajab Kheir Yussuf, Bwna Said Matar Mwinyi, Bwana Salum Nassor Said (Mkweche).

Marehemu Khatib Hassan Mzibondo, Marehemu Mej. (mst) Mosi Kassim Mosi. Lt Col (mst) Songoro Abdi Waziri, Bwana Hafidh Badru Juma, Bibi Nasra Juma Mohamed, Bibi Mwanaacha Hassan Kijore, Bibi Maryam Mohamed Hamdani, Bwana Makame Faki Makame, Marehemu Ally Salum Basalam,

Kwa upande wa nishani ya utumishi uliotukuka wakiwemo watumishi wa Serikali, Mahkama na Baraza  la Wawakilishi kwa kuanzia watumshi wa Serikali ni Marehemu Othman Bakar Othman, Marehemu Sheikh Harith Bin Khelef, Marehemu Ramadhan Hamad Hilika, Marehemu Mkadam Juma Nassib, Bwana Saleh Sadik Osman, Marehemu Juma Khiari Simai, Bwana Kassim Maalim Suleiman.

Wengine ni Bwana Juma Haji Juma, Bwana Juma Bakari Juma, Yussuf Khamis Yussuf, Masururu Saad Feruzi, Lt Col (mst) Mohamed Abdalla Mohamed (REX), Bwana Hassan Rehani Hassan, Bwana Mohamed Nassor Mohamed Alhansy, Marehem Shaaban Seif Said.

Mhandisi Rama Keis Mgeni, Ameir Issa Haji, Ahmada Khamis Hilika, Bibi Salama Mzee Majaliwa Marehemu Khalil Abass Mirza, Marehemu Mwalimu Sheikh Burhan Iddi Sonjo, Kassim Makame Biwi, Marehemu Dk. Thani Filfil Thani, Marehemu Abdulkadir Ali Mussa, Marehemu Alice Alban Ali, Marehemu Jessey E. Amor.

Aidha, Dk. Shein aliwatunuku nishani watumishi wa Mahakama akiwemo Marehemu Jaji Saleh Abdallah Dahoma, Marehemu Sheikh Ali Khatib Mranzi, Marehemu Abass Hassan Mirza na kwa upande wa utumishi wa Baraza la Wawakilishi ni Bibi Moza Abdalla  Jabir.

CCM Blog

Read more


Habari Zinazoendana

10 months ago

Michuzi

RAIS WA ZANZIBAR DK,SHEIN ATUNUKU NISHANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindizi Dk,Ali Mohammed Shein akimvisha nishani ya Mapinduzi Bwana Aboud Talib Aboud katika hafla ya kutunuku nishani ya Mapinduzi,nishani ya Utumishi uliotukuka na nishani ya Ushujaa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindizi Dk,Ali Mohammed Shein katikati akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi na waliotunukiwa nishani mbalimbali katika hafla ya kutunuku nishani ya...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Rais Dk. Ali Mohamed Shein Atoa pongezi kwa serikali ya China na India

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amepongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Serikali ya India katika kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeleo na kukuza uchumi wake.

Dk. Shein aliyasema hayo wakati  alipokuwa na mazungumzo na Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar  Xie Xiaowu na Balozi Mdogo wa India Mhe. Tek Chand Barupal kwa nyakati tofauti walipofika Ikulu...

 

3 years ago

Vijimambo

Risala ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kutoka kwa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa Risala ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa Wananchi na Waislamu wote nchini katika Risala hiyo amewataka Wananchi kuwa amani na Utulivu na kuwaombea kwa Mola wetu kuwajaalia Rehma baraka za Mwezi Mtukufu wa Ramadhan pia amewataka kufanya ibada kwa wingi katika kipindi chote cha mwezi huu,(Picha na Ikulu.)
RISALA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN YA RAIS WA
ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI,
MHESHIMIWA...

 

2 years ago

Mwananchi

MC-MKONGWE : Rais Ali Mohamed Shein jinasue

Nasua au kujinasua ni ‘kutoa au ondoa mtegoni kitu kilichonaswa’. Imekuwa sasa kama kawaida kwa mizozo mizito ya kugombea ushindi, ambao hatimaye unapatikana kwa malalamiko mengi huko Zanzibar.

 

3 years ago

Michuzi

RAIS KIKWETE ATUNUKU NISHANI KWA WATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassa Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman wakiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa wa nishani za Jamhuri ya Muungano daraja la kwanza, Utumishi wa muda mrefu na maadili mema daraja la kwanza na Utumishi wa muda mrefu na maadili mema daraja la pili na Ushupavu Jumanne Juni 23, 2015 katika ukumbi mpya wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam.   Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu...

 

4 months ago

CCM Blog

RAIS WA ZANZIBAR DKT.ALI MOHAMED SHEIN ATOA PONGEZI KWA TIMU YA ZANZIBAR HEROES RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameendelea kutoa pongezi kwa timu ya Taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’ kwa kuirudishia Zanzibar heshima yake na sasa imekuwa inasemwa vizuri kutokana na jinsi timu hiyo ilivyoonesha kiwango safi cha kusakata soka.


Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar katika chakula maalum cha mchana alichowaandalia wachezaji wa Timu ya Zanzibar Heroes pamoja na viongozi wake wote baada ya...

 

3 years ago

Michuzi

ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR DK.ALI MOHAMED SHEIN- UJERUMANI


1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Maritim Hotel Bw.Wissmann katika Mji wa  Wurzburg Nchini Ujerumani jana alipowasili katika Mji huo akiwa katika ziara ya Kiserikali ambapo atahudhuria ufunguzi wa maonesho ya Muziki yanayojumuisha wasanii kutoka nchi za Afrika na Mabara mengine (kulia) Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Philip Marmo, [Picha na Ramadhan Othman.]2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani