Rais Jacob Zuma apewa saa 48 kujiuzulu

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa saa 48 kujiuzulu, wadhfa wake huo.

Kwa mujibu wa shirika la Utangazaji la Afrika Kusini -SABC- na vyanzo vingine vya habari, hatua hii inakuja baada ya mlolongo wa mazungumzo yaliyofanywa na chama tawala cha nchini humo ANC.

Duru zinasema ANC kilifanya mazungumzo marefu baadaye kuwatuma watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa chama ana kwa ana ya kwamba Zuma ajiuzulu mwenyewe au chama kimng’oe madarakani.

Lakini haijulikani bado kwamba Rais Zuma alipokeaje ujumbe huo.

Hatua hii ya ANC inaonekana ndio njia rahisi zaidi ya chama hicho kumng’oa rais Zuma madarakani badala ya kusubiri utaratibu wa bunge ambao ungeweza kuwa mrefu na wenye madhara zaidi kwa chama cha ANC.

Rais Jacob Zuma ambaye anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa, alishindwa uongozi wa chama tawala Desemba mwaka jana.

Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa anaongoza shinikizo za kumuondoa Zuma katika nafasi yake hiyo ya Urais, na hatimaye kushika pia nafasi hiyo.

Ramaphosa ameahidi pia kupambana na rushwa iliyokithiri na kukijenga upya chama cha ANC, wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi mwakani.

The post Rais Jacob Zuma apewa saa 48 kujiuzulu appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

5 days ago

BBCSwahili

Zuma apewa saa 48 kujiuzulu

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa saa 48 kujiuzulu. wadhfa wake huo

 

5 days ago

Malunde

RAIS APEWA SAA 48 KUJIUZULU

Wanachama wa ANC waliogawanyika
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa saa 48 kujiuzulu, wadhfa wake huo.
Kwa mujibu shirika la Utangazaji la Afrika Kusini -SABC- na vyanzo vingine vya habari, hatua hii inakuja baada ya mlolongo wa mazungumzo yaliyofanywa na chama tawala cha nchini humo ANC.
Duru zinasema ANC kilifanya mazungumzo marefu baadaye kuwatuma watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa chama ana kwa ana ya kwamba Zuma ajiuzulu mwenyewe au chama...

 

4 days ago

BBCSwahili

Rais Jacob Zuma: Sijafanya makosa yoyote na sioni sababu ya kujiuzulu

Bwana Zuma alizungumza baada ya chama tawala cha ANC kumpatia makataa ya kujiuzulu mwisho wa siku la sivyo akabiliwe na kura isiokuwa na imani dhidi yake siku ya Alhamisi

 

1 year ago

MillardAyo

Maamuzi ya Bunge la Afrika Kusini juu ya Rais Jacob Zuma kutakiwa kujiuzulu

South African President Jacob Zuma delivers his State of the Nation address at Parliament in Cape Town February 9, 2012. Zuma on Thursday promised to keep the country's powerful mining sector "globally competitive", the latest comment from a senior government official to knock down the prospects of nationalising the mines.  REUTERS/Mike Hutchings (SOUTH AFRICA - Tags: POLITICS ENERGY BUSINESS INDUSTRIAL)

November 10 2016 wabunge wa Bunge la Afrika Kusini wamefuta kabisa pendekezo la kupiga kura ya kutokua na imani dhidi ya Rais wa Afrika Kusini wa nchi hiyo Jacob Zuma pamoja na kuwepo madai ya hivi karibuni kuhusu ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka kwa kiongozi huyo. Kwa mujibu wa Radio France International, Uchunguzi uliofanywa na tume […]

The post Maamuzi ya Bunge la Afrika Kusini juu ya Rais Jacob Zuma kutakiwa kujiuzulu appeared first on millardayo.com.

 

10 months ago

Channelten

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema hakuzaliwa na urais na anaweza hata kujiuzulu akilazimika na chama chake

849x493q70Ranjeni-SONA2017-1

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema hakuzaliwa na urais na anaweza hata kujiuzulu endapo italazimika kufanya hivyo na chama chake.

Zuma amewaambia wafuasi wake wakati akitimiza miaka 75 hapo jana na kuwa chama chake cha ANC kinaweza kuamua kumwondoa madarakani ikiwa kinataka kufanya hivyo.

Kauli hii ya Zuma imekuja baada ya maandamano makubwa katika miji kadhaa jijini Pretoria kumshinikiza Zuma kujiuzulu baada ya kumfuta kazi aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye alikuwa anakubalika sana...

 

3 days ago

Malunde

Breaking News :JACOB ZUMA ATANGAZA KUJIUZULU URAIS


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametangaza kujiuzulu.

South Africa's embattled President Jacob Zuma has resigned his office with immediate effect.
He made the announcement in a televised address to the nation on Wednesday evening.
Earlier, Mr Zuma's governing ANC party told him to resign or face a vote of no confidence in parliament on Thursday.
The 75-year-old has been under increasing pressure to give way to Deputy President Cyril Ramaphosa, the ANC's new leader.
Mr Zuma, who has been in power...

 

3 years ago

Vijimambo

RAIS JACOB ZUMA AKUTANA NA RAIS KIKWETE IKULU-MAKAMU WA RAIS AMSINDIKIZA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini leo ikulu jijini Dar es Salaam

 

2 years ago

Channelten

Rais Jacob Zuma kushtakiwa?

 

zuma3

Wabunge nchini Afrika kusini watawasilisha hoja ya kumshitaki rais Jacob Zuma baadaye leo ikiwa ni baada ya mahakama kuu ya nchi hiyo kutoa hukumu kwamba rais huyo alikiuka katiba kwa kutumia mamilioni ya dola fedha za umma kukarabati nyumba yake ya binafsi.

Chama kikuu cha upinzani, The Democratic Alliance, kilitoa wito wa Zuma ashitakiwe baada ya mahakama ya katiba kutoa hukumu wiki iliyopita.

Lakini Zuma huenda akanusurika na changamoto hiyo, wakati bunge la nchi hiyo litahitaji wingi...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani