RAIS MAGUFULI KAULI ZAKO KUWA DARAJA LA WAPINZANI ?

Rais John Magufuli

Rais John Magufuli

NA JAVIUS KAIJAGE,

DESEMBA 31 mwishoni mwa   mwaka jana, Rais John Magufuli akiwa katika mapumziko  yake mafupi, alitua  mkoani  Kagera ikiwa zimepita siku 112 tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi.

Akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo, Januari  2, mwaka huu  katika  viwanja vya shule ya Sekondari   ya Ihungo  mjini Bukoba, Rais  aliwahutubia mamia ya wananchi waliofurika kumsikiliza.

Katika hotuba yake iliyojaa  msisimuko, Mheshimiwa Rais aliwapa pole wakazi wa Kagera kwa kukumbwa na janga kubwa la tetemeko  ambalo lilipoteza maisha ya watu na mali  huku wengine wakijeruhiwa.

Pamoja na pole aliyotoa Mheshimiwa Rais  katika hotuba, vile vile aliendelea kusisitiza kuwa Serikali yake anayoiongoza haitaweza kutoa msaada kwa mtu mmoja mmoja mfano chakula au kujenga nyumba bali kitakachofanyika ni ujenzi wa miundombinu.

Mkuu huyo wa nchi akiwa anajinadi  kwa kusema ‘Msema kweli ni mpenzi wa Mungu’’ aliwahimiza Wanakagera kutobweteka bali wafanye kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo  huku akiwaamuru wasaidizi wake aliowateua kwa makusudi  hususani wanajeshi kuhakikisha  wanawawajibisha wananchi.

Kutokana  na  afya ya akili,  baada ya hotuba ile, baadhi ya watu wakiwamo wasomi, wanasiasa na wananchi wa kawaida wamekuwa wakiitafsiri katika  mitazamo tofauti.

Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Bashiru Ally alisema kuwa katika mfumo wa siasa huru kuna  kutofautiana mitazamo kati ya wananchi, Serikali na viongozi wa siasa lakini ni wazi kuwa Rais alisimama katika msimamo wa Serikali yake na uwezo wa kutekeleza ahadi zake.

Kwa upande wake Dk. Benson Bana kutoka Chuo hicho cha Dar es Salaam alisema kuwa watu wanatafsiri vibaya maneno ya Mheshimiwa Rais aliyoyaongea mkoani Kagera hivi juzi. “Mheshimiwa ameongea ukweli kwa sababu ni sahihi kuwasaidia watu wengi kwa pamoja kuliko kumsaidia mtu mmoja mmoja,” alisema.

Naye Prof. Haji Semboja alisema kuwa kauli ya Rais ilikuwa ni kuwahimiza watu wa Kagera ambao  anajua wana uwezo wa mambo mengi ya kulima mazao mbalimbali kama vile  ya chakula na biashara  yanayoweza kuwapatia chakula cha kutosha.

Wakati wasomi hawa wakiwa na mitazamo hii, kwa upande wake Mwenyekiti  wa (Chadema), Freeman Mbowe ameikosoa hotuba ya  Rais Magufuli mkoani Kagera kwa kusema ” Hivi mtu ambaye amefiwa, nyumba imebomolewa, hana chakula, hana pesa unakwenda kutoa kauli za kibabe kwamba hutawapa chakula kwa kuwa Serikali haina shamba! hivyo si sawa sawa”

Mheshimiwa Mbowe akiwa kiongozi mkuu wa upinzani, kauli yake inaweza kuwa ya ukweli au ni namna ya kujitafutia umaarufu  ukizingatia katika siasa upinzani mara nyingi upo kwa lengo la kutaka kushika dola.

Katika awamu kadhaa zilizopita upinzani uliweza kuimarika kutokana na  matukio ya ufisadi. Nani hakumbuki kuwa Richmond ni miongoni mwa kashfa kubwa zilizoujenga upinzani hasa Chadema ?

Katika enzi hizi za ushindani kisiasa, chama makini  kama Chadema ikitokea kikakosa ajenda mahususi  za kuishitaki Serikali kwa wananchi kama inavyoonekana  sasa kwamba kutokana na uongozi wa JPM matukio ya ufisadi yanapungua kwa kasi, ni lazima utatafutwa udhaifu mwingine.

Ni kweli kiongozi anayetoa ahadi zinazotekelezeka ni  muungwana kuliko anayeahidi kukujengea ghorofa angani,  lakini kuna haja ya kuwa makini katika kauli maana  kutokana na ugumu wa maisha, wananchi wengi wanahitaji kujengwa kisakolojia kwa maneno ya hamasa   vinginevyo upinzani utatumia fursa  ya msongo wa mawazo yao kujinufaisha kisiasa.

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

11 months ago

MillardAyo

Ufafanuzi wa Rais Magufuli kuhusu ile kauli ya kutoteua Wapinzani (+video)

Rais Magufuli leo Ikulu Dar es salaam amemuapisha Mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira ambaye Mwenyekiti katika chama cha ACT Wazalendo. Baada ya kumuapisha, moja ya vitu alivizungumza Rais JPM ni kuhusu ile kauli yake ya kutoteua upinzani… kauli ambayo imekua ikisambaa kwenye video fupi baada ya kumteua Mama Anna Mghwira. Leo Ikulu Rais […]

The post Ufafanuzi wa Rais Magufuli kuhusu ile kauli ya kutoteua Wapinzani (+video) appeared first on millardayo.com.

 

1 year ago

Malunde

MBUNGE LEMA ASHANGAA KAULI YA RAIS MAGUFULI KUWA WABUNGE WA CCM NI WA WASALITIMBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameibuka na kueleza kushangazwa na kauli ya Rais Dk. John Magufuli kwamba wabunge wa CCM waliotaka kwenda kumwona gerezani walikuwa wasaliti.

Lemsa alisema anatarajia Spika wa Bunge, Job Ndugai, atatoa msimamo juu ya kauli ya kiongozi huyo wa nchi.
Kauli hiyo ya Lema imekuja siku moja baada ya Rais Dk. John Magufuli, kuripotiwa na chombo kimoja cha habari (si Mtanzania) kwamba alishangazwa na hatua ya baadhi ya wabunge wa CCM waliounda kamati ya kutaka...

 

2 years ago

Michuzi

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA RASMI DARAJA LA KIGAMBONI, ALIBATIZA JINA LA DARAJA LA NYERERE. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe huku viongozi wengine wakiushikilia kuashiria uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata picha ya kumbukumbu viongozi wengine baada ya  uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016. Rais wa...

 

2 years ago

Channelten

PICHA : Rais Magufuli na Rais wa Rwanda Paul Kagame wazindua daraja la Kimataifa

20160406052341 20160406052339

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame wamezindua daraja la Kimataifa la Rusumo nchini Rwanda.

2820c6bc-0186-4338-88b7-53bf1ea0daed 6eb9e665-98d9-483d-8a7f-87c16e94c544

 

2 years ago

MillardAyo

PICHA 7: Rais Magufuli na Rais Kagame walivyoweka baraka zao kwenye daraja la Lusumo

.

Ni safari ya kwanza ya nje ya nchi kwa Rais Magufuli toka alipoteuliwa kuwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania October 2015, kasafiri kwa gari kwenda Rwanda ambapo kwenye siku yake ya kwanza yeye pamoja na Rais Kagame wamezindua daraja la Rusumo kwenye mpaka wa Tanzania na Rwanda.  ULIIKOSA YA RAIS MAGUFULI KUNUNULIA WATU […]

The post PICHA 7: Rais Magufuli na Rais Kagame walivyoweka baraka zao kwenye daraja la Lusumo appeared first on TZA_MillardAyo.

 

9 months ago

Mwananchi

Rais Magufuli amtofautisha Zitto na wapinzani wengine

Rais Magufuli amewasili kwenye chanzo cha mradi mkubwa wa maji na amezindua mradi utakaozalisha  lita 42 milioni kwa siku utakaomalizika   Novemba 30, mwaka huu.

 

2 years ago

StarTV

Rais Magufuli awataka wapinzani kuondoa tofauti zao

 

Rais wa awamu ya Tano Dokta John Pombe Magufuli amevitaka vyama vya upinzani nchini kuondoa tofauti zao na badala yake washirikiane pamoja katika kuwatumikia watanzania ili kufanikisha azma ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kuapishwa rasmi na kuwa rais wa Jamhri ya muungano wa Tanzania awamu ya tano Katika Sherehe zilizofanyika JIjini Dar es Salaam.

Kushushwa kwa  Bendela ya Rais inaonesha kufikia ukomo kwa uongozi wa Serikali ya awamu ya nne na sasa...

 

2 years ago

StarTV

UVCCM yawashauri wapinzani kutoubeza Utendaji wa Rais Magufuli

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM umevishauri vyama vya upinzani hususani UKAWA kutobeza utendaji wa Rais wa awamu ya tano Dokta John Magufuli na badala yake wamuunge mkono kwa maendeleo ya nchi.

vlcsnap-2016-05-19-11h46m55s165

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhamasihaji Sera, Utafiti na Mawasiliano wa UVCCM Abubakar Asenga alipozungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam.

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wamesema siasa za kupinga maendeleo kwa sasa...

 

1 year ago

Mwananchi

KAKAKUONA : Rais Magufuli, wafanye wapinzani jicho lako la pili

Kama ningeteuliwa kuwa mshauri wa Rais katika masuala ya siasa, ushauri wangu wa kwanza kwa Rais John Magufuli, ungekuwa kuruhusu mikutano ya ‘kitaifa’ ya vyama vya siasa.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani