RAIS MAGUFULI AMPONGEZA KENYATTA KUCHAGULIWA KUWA RAIS WA KENYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Agosti, 2017 amempongeza Rais Mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta baada ya jana kutangazwa mshindi wa nafasi ya Urais na Tume Huru Ya Uchaguzi Kenya ( IEBC).

Tume Huru ya Uchaguzi Kenya ilitangaza Kenyatta kuwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 (54.27%) dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga 6,762,224 (44.74%), kufuatia matokeo hayo Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametoa pongezi kwa Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine tena.

"Nakupongeza Ndg.Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema" alisema Rais Magufuli kupitia mtandao wake wa Twitter

Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) ilisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki na kudai kuwa umekuwa ni uchaguzi wa kipekee kwa Kenya kwani watu waliojitokeza kujiandikisha na kupiga kura ni wengi zaidi ukilinganisha na chaguzi zilizofanyika kipindi cha nyuma.

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

9 months ago

Malunde

RAIS MAGUFULI AMPONGEZA PAUL KAGAME KUCHAGULIWA TENA KUWA RAIS WA RWANDA

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametangazwa mshindi wa Urais wa nchi hiyo baada ya kushinda katika uchaguzi Mkuu uliofanyika August 4, 2017 na kumrudisha madarakani kwa muhula wa tatu.

Baada ya ushindi huo Rais wa Tanzania John Magufuli ametumia ukurasa wake twitter kumtumia salamu za pongeni Rais Kagame.
”Nakupongeza Mhe. Paul Kagame kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Rwanda kwa kipindi kingine. Kwa niaba ya Watanzania wote nakutakia mafanikio mema.
"Tutaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano na uhusiano...

 

2 years ago

Michuzi

Rais wa Ireland Mhe. Michael D. Higgins ampongeza Dkt John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais


 SALAMU ZA PONGEZI
Rais wa Ireland, Mheshimiwa Michael D. Higgins amemtumia Salamu za Pongezi  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika Salamu zake hizo, Rais Higgins amesema Ireland na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri na wa kirafiki kwa miaka mingi, hivyo ana matarajio kwamba katika kipindi cha uongozi wa Rais Magufuli, uhusiano huo utaimarishwa zaidi.


“Ireland na Tanzania zimekuwa na mipango ya maendeleo na...

 

2 years ago

Bongo5

Rais wa (CAF), Issa Hayatou ampongeza Ravia Idarous kuchaguliwa kuwa Rais wa Soka Zanzibar (ZFA)

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), Issa Hayatou amemtumia salamu za pongezi Ravia Idarous Faina kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) mwishoni mwa juma lililomalizika.

hayatou

Katika salamu zake, Hayatou amesema kwa niaba ya CAF, Kamati ya Utendaji na yeye binafsi wanampongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA).

CAF wanaimani na uzoefu wa Ravia katika uongozi, kuwa ataendeleza uongozi bora kwa faida ya maendeleo ya soka...

 

2 years ago

Bongo5

Rais Magufuli ampongeza Rais Kenyatta kwa ujenzi wa barabara ya kisasa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta wamezindua barabara ya Southern Bypass huku Rais Magufuli akisema wananchi wanahitaji maendeleo na hayo ndio yenyewe.

14915571_1440392175989331_5633888333426358079_n

Akizungumza katika sherehe hiyo, Rais Magufuli amempongeza Rais Kenyatta na serikali yake kwa kujenga barabara hiyo ambapo amesema haitawasaidia wananchi wa Kenya tu, bali pia itawasaidia wananchi wa Afrika Mashariki wanaotumia barabara zinazopitia...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Rais Kenyatta amuandalia dhifa Rais Magufuli Ikulu nchini Kenya

11Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi.12Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akizungumza katika dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Nairobi.15Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo huku akiwa amewashika mikono kwa pamoja Rais wa...

 

2 years ago

Channelten

Rais Magufuli na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta leo wamezindua barabara

3

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya Bw. Uhuru Kenyatta leo wamezindua barabara ya Southern By-pass iliyojengwa kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi nchini Kenya.

Sherehe ya uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 28 na inayounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi imefanyika katika eneo la Karen nje kidogo ya Jiji la Nairobi, ambapo Rais Magufuli amempongeza Rais Kenyatta na Serikali yake...

 

2 years ago

Dewji Blog

VIDEO: Hotuba ya Rais Magufuli na Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwasili Kenya

Rais John Pombe Magufuli amewasili nchini Kenya kwa ziara ya siku mbili ambapo baada ya kuwasili amezungumza na mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na baada ya hapo wamelihutubia taifa la Kenya kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Baadhi ya mambo ambayo wameyazungumza ni pamoja na ushirikiano wa Kenya na Tanzania, usalama wa kupambana na ugaidi kwa mataifa ya Tanzania na Kenya kushirikiana, kuboresha mawasiliano ya Tanzania na Kenya pamoja na kujadili mambo mbalimbali ambayo...

 

2 years ago

CCM Blog

RAIS DK. MAGUFULI KATIKA DHIFA YA ALIYOANDALIWA NA RAIS UHURU KENYATTA NCHINI KENYA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi.

 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akizungumza katika dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Nairobi. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigonganisha glass na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru...

 

2 years ago

Ippmedia

Rais Magufuli na Rais kenyatta wazindua barabara ya Southern Bypass nchini Kenya.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli na rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wamezindua barabara ya Southern Bypass iliyojengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Nairobi nchini Kenya.

Day n Time: Jumanne Saa 2:00 Usiku Station: ITV

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani