RAIS MAGUFULI ATAKA TAASISI ZA AGA KHAN KUPUNGUZA GHARAMA ZA MATIBABU


Rais John Magufuli akiagana na kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia duniani, Prince Karim Al-Hussayni Aga Khan baada ya kufanya naye mazungumzo alipomtembelea Ikulu, Dar es Salaam jana. (Picha na Ikulu).
***RAIS John Magufuli ametoa mwito kwa Taasisi za Aga Khan kupunguza gharama za huduma zake kwa wananchi ili waweze kumudu, hasa ikizingatiwa kuwa zimekuwa zikipata msamaha wa kodi kutoka serikalini.
Rais Magufuli alisema hayo jana alipokutana Ikulu Dar es Salaam na Kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia Duniani, Karim Aga Khan ambapo alimshukuru kwa taasisi zake kutoa huduma za kijamii hapa nchini.
Pia Rais Magufuli alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ipo tayari kuendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano na Aga Khan na amemuomba kiongozi huyo kuendelea kupanua wigo wa huduma za taasisi zake, ikiwa ni pamoja na kuwekeza mjini Dodoma yaliko makao makuu ya Serikali.
Akizungumza na Rais, Aga Khan alisema Jumuiya ya Ismailia imedhamiria kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kupanua hospitali ya Aga Khan iliyopo Dar es Salaam na kujenga chuo kikuu kikubwa katika Afrika Mashariki mkoani Arusha.
Aga Khan alisema kuwa upanuzi wa hospitali ya Aga Khan, utahusisha kuongeza idadi ya vitanda vya wagonjwa kutoka 72 vya sasa hadi kufikia vitanda 172, utaimarisha matibabu ya moyo, kansa na utaongeza ufundishaji wa madaktari na wataalamu wengine wa afya.
Kuhusu chuo kikuu kitakachojengwa Arusha, Aga Khan alisema Jumuiya hiyo imedhamiria kujenga chuo kikuu kikubwa ambacho kitafundisha viongozi si tu wa Tanzania na Afrika Mashariki, bali pia Afrika nzima ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko na maendeleo ya Afrika.
Kwa upande wa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Aga Khan, alisema kuwa yeye haamini kuwa yeye ni kipaumbele kwa vyombo vya habari kujikita katika masuala ya siasa. Badala yake, alisema anaamini kuwa vyombo vya habari vina wajibu mpana zaidi wa kujikita katika masuala ya maendeleo hususani katika nchini zinazoendelea, na kwamba Aga Khan ipo katika mchakato wa kujikita katika wajibu huo kwa kuwa na waandishi wa habari na wachambuzi mahiri.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Maseneta wa Baraza la Seneti la Marekani, ambao ni wajumbe wa kamati ya mazingira inayoshughulikia hifadhi ya taifa, wanyamapori na misitu ya Marekani, ambao wamekuwepo hapa nchini kwa siku tatu kwa lengo la kutembelea hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.
Maseneta hao ni James Inhofe, Mike Enzi, David Perdue, Luther Strange, Tim Scott na John Thune. Baada ya mazungumzo hayo, Seneta James Inhofe na Seneta Mike Enzi walimshukuru Rais Magufuli kwa kukutana nao na kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Marekani kuja kuwekeza nchini.
Walikiri kuwa Tanzania inazo rasilimali nyingi ambazo ni fursa muhimu ya kukuza uchumi. Mazungumzo kati ya maseneta hao na Rais Magufuli, yalihudhuriwa pia na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dk Inmi Patterson.
Chanzo-Habarileo

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Dewji Blog

Rais Kikwete amkabidhi H.H. The Aga Khan hati ya chuo kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar

ag6

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki na Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana tayari kwa  kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam.

ag2

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza  Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana akiongea baada ya kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam.

ag3

Rais Jakaya Mrisho Kikwete...

 

3 years ago

Vijimambo

RAIS KIKWETE AMKABIDHI H.H. THE AGA KHAN HATI YA CHUO KIKUU CHA AGA KHAN KILICHOPO DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki na Kiongozi wa madhehebu yaIsmailia duniani Mtukufu Aga Khana tayari kwa kumkabidhi hati ya ChuoKikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulujijini Dar es salaamRais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Kiongozi wa madhehebu yaIsmailia duniani Mtukufu Aga Khana akiongea baada ya kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaamRais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi...

 

3 years ago

GPL

RAIS KIKWETE AMKABIDHI H.H. THE AGA KHAN HATI YA CHUO KIKUU CHA AGA KHAN KILICHOPO DAR ES SALAAM‏

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana baada ya kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza  Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana akiongea baada ya kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23,...

 

4 years ago

Michuzi

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AIFAGILIA TAASISI YA AGA KHAN KWA KUSAIDIA MAENDELEO YA JAMII

Mzee Mwinyi akiwa ameketi meza kuu na viongozi wa Tasisi hiyo ya Aga Khan Sheikh Mkuu, Muft wa Tanzania akiingia ukumbini Makamu wa Rais wa Taasisi ya Aga Khan Tanzania, Kanal Khimj akitoa manano ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Mzee Mwinyi kuzungumza Mzee Mwinyi akizungumza "Hekima ikiongezeka Maneno yanapungua", akisema Mzee Mwinyi mwishoni mwa hotuba yake iliyojaa hekima. Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

 

3 years ago

Dewji Blog

Canadian Prime Minister Stephen Harper and Aga Khan Open the Ismaili Centre Toronto and Aga Khan Museum

11 DSC_0460 (PM Harper and HH the Aga Khan waving to crowds outside the Ismaili Centre, Toronto - AKDN Zahur Ramji)

PM Harper of Canada and HH the Aga Khan waving to crowds outside the Ismaili Centre, Toronto – AKDN / Zahur Ramji).

The Right Honourable Stephen Harper, Prime Minister of Canada, and His Highness the Aga Khan formally opened the Ismaili Centre Toronto and Aga Khan Museum today.

These projects, which are initiatives of the Aga Khan, the 49th hereditary Imam of the Shia Ismaili Muslims and founder and Chairman of the Aga Khan Development Network, are intended to foster knowledge and...

 

2 years ago

Habarileo

Aga Khan kuokoa hadi bil 25/- za matibabu nje

SERIKALI imezindua ujenzi wa jengo la Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam ambao ukikamilika, utawezesha kutolewa kwa matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza yakiwamo ya saratani, moyo na figo na hivyo kusaidia kuokoa Sh bilioni 20 hadi 25 zinazotumika kila mwaka kwa ajili ya rufaa za wagonjwa wanaotakiwa kutibiwa nje ya nchi.

 

3 years ago

GPL

CANADIAN PRIME MINISTER STEPHEN HARPER AND AGA KHAN OPEN THE ISMAILI CENTRE TORONTO AND AGA KHAN MUSEUM‏

PM Harper of Canada and HH the Aga Khan waving to crowds outside the Ismaili Centre, Toronto - AKDN / Zahur Ramji).…

 

4 years ago

GPL

WAZIRI WA AFYA, DR. SEIF, AZINDUA KITUO CHA MATIBABU YA SARATANI HOSPITALI YA AGA KHAN‏

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Dk. Seif Seleman Rashid akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya matibabu ya saratani kwa mara ya kwanza katika Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam. Uzinduzi huo uliohudhuriwa na mtoto kutoka familia ya familia ya Aga Khan, Zahra ulifanyika katika ukumbi uliopo hospitalini hapo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh, Dk. Seif Seleman Rashid (kulia) akibadilishana mawazo na mtoto...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani