RAIS MAGUFULI AWANYEMELEA WATUMISHI SERIKALINI WENYE VYETI FEKI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John Pombe Joseph Magufuli,amejinasibu kutenda haki mara atapopata ripoti ya watumishi wa Serikali,waliogushi vyeti.
Kuna madai ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa kutumia vyeti vya kufoji,ambapo sasa Rais Magufuli, amefunguka kwa kusema sasa anasubiri ripoti ya wahusika hao ili aitendee kazi.

Rais Magufuli amesema hayo, wakati akizindua majengo ya Hostel za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM),kwa kudai kumekuwa na changamoto kubwa katika kila sekta hivyo sasa anasubiri hiyo ripoti ili aweze kuifanyika kazi na kutenda haki katika jambo hilo.

Anasema;"Naisubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wana vyeti vya kufoji ili niifanyie kazi." 

Mbali na hilo Rais Magufuli ameitaka Taasisi ya TCU kuacha kuwapangia wanafunzi vyuo bali wanafunzi wanapaswa kuwa huru kuchagua aina ya vyuo ambavyo wao wanataka kwenda kusoma.

Amefafanua kwa kusema kufanya hivyo itatoa nafasi kila chuo kuwa na wanafunzi wa kutosha huku wanafunzi pia wakienda kusoma sehemu ambazo wao wanahitaji kwenda kusoma na si kuwapangia.

"Mtu amefaulu ana sifa zake anataka kuja kusoma Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam afaidi mabweni ya Magufuli analazimishwa kupelekwa kwenye ka chuo ambako wala hakana jina hata ukitafuta kwenye mtandao hakaonekani, akasome pale wakati hawana hata mabweni na saa zingine hata walimu hawana, tunawatesa watoto hawa,”

“… na saa zingine wakuu wa vyuo vile wamekuwa na tabia ya kwenda kwenye uongozi wa TCU ingawa sina ushahidi wapangiwe idadi wa wanafunzi wanaowataka kwenye vyuo hivyo,”“….sifahamu wanapangiwa kwa rushwa,lakini wapo pia kuna ushahidi na baadhi ya viongozi wa vyuo fulani fulani waliofunga safari kwenda TCU kwa ajili ya kuomba wapangiwe wanafunzi au kutoa shukrani, au hata kwenda kuwasalimu tu" alisema Rais Magufuli.

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Global Publishers

Video: Kiama cha wenye Vyeti feki, Watumishi Hewa Kimewadia! – Rais Magufuli

Rais Magufuli amesema haya wakati akizindua rasmi mabweni ya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo.

Wataalam walisema mradi huu ungegharimu bil.150 mpaka bili.170 kukamilisha, ilikuwa ni lugha ya kukatisha tamaa.

Tatizo la makazi liliwasumbua wanafunzi wengi UDSM. Kuna waliolazimika kuoa au kuolewa ili tu wapate makazi ya kuishi.

Wengi waliokuwa wakipanga vyumba mitaani, walipanga katika maeneo hatarishi huku wengine wakilala kwa zamu.

Nashukuru tuliweza kupata eneo la kujenga hapa, si kama...

 

2 months ago

Malunde

WATUMISHI WALIOONDOLEWA KAZINI KWA VYETI FEKI HAWANA MADAI YOYOTE SERIKALINI
Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora imesema watumishi wote waliondolewa katika utumishi wa umma kwa sababu ya kukosa vyeti vya kidato cha nne hawana madai yoyote Serikalini.

Kauli hiyo imetolewa leo, Februari 12, 2018 na Kaimu Katibu Mkuu katika ofisi hiyo, Mathias Kabunduguru katika kikao cha wakurugenzi wa utawala na rasilimali watu wa wizara zote, makatibu tawala, wasaidizi mkoa na wakuu wa idara za utumishi na utawala.

Amesema zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma...

 

12 months ago

Zanzibar 24

Rais Magufuli awataka kuacha kazi wenye vyeti feki ifikapo mei 15

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaagiza watumishi 9932 waliobainika wana vyeti feki kuwacha kazi ifikiapo Mi 15 la sivyo wakamatwe na kushtakiwa.

Magufuli ameyasema hayo leo April 28,2017 katika mji mkuu wa Dodoma wakati akikabidhiwa na Waziri Angella Kairuki orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki.

Alisema Rais Magufuli “Hizo nafasi 9932 zitangazwe ili wasomi hawa waanze kuziomba. Hawafanya 9932 leo ni tarehe 28 ninajua wanajijua lakini na majina yao...

 

2 years ago

MillardAyo

VIDEO: Prof. Lipumba basi tena, Giza nene latanda wenye vyeti feki serikalini

LIPUMBA

AyoTV kila asubuhi itakua inakuletea uchambuzi wa magazeti ya Tanzania kuhakikisha zote kubwa za siku unazipata, za leo August 22 2016 ziko hapa kwenye hii video. ULIKOSA ALICHOKISEMA MBATIA KUHUSU UKAWA KUUNDA CHAMA KIMOJA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

The post VIDEO: Prof. Lipumba basi tena, Giza nene latanda wenye vyeti feki serikalini appeared first on millardayo.com.

 

12 months ago

Zanzibar 24

Watumishi wenye vyeti feki hatma yao inakaribia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo anatarajiwa kupokea taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma katika Ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

Taarifa hiyo itawasilishwa na waziri wa Nchi Afiri ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mh. Angellah Kairuki.

 

The post Watumishi wenye vyeti feki hatma yao inakaribia appeared first on Zanzibar24.

 

11 months ago

Zanzibar 24

Lowassa: Watumishi wa Umma wenye vyeti feki waangaliwe kwa sura ya huruma

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA,, Edward Lowassa asema watumishi 9,932 wa umma wenye vyeti feki inabidi waangaliwe kwa sura ya huruma.

Lowassa aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema anatoa pongezi kwa mambo mengi mazuri yaliyofanywa, lakini katika sakata la vyeti feki, kuwa wapo walioitumikia serikali kwa muda mrefu, na kama wakifukuzwa tu pasipo kulipwa mafao yao basi itakuwa si ubinadamu.

Aidha alizungumzia kuhusu kuzuiliwa kwa kongamano lililokuwa...

 

11 months ago

Michuzi

SERIKALI KUAJIRI WATUMISHI WA KADA YA AFYA KUZIBA PENGO LA WENYE VYETI FEKI

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kuajiri watumishi wa idara ya afya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi ambao wameondolewa katika utumishi wa umma kwa kukosa sifa ya kuwa na vyeti halisi baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo jana wakati wa maadhimsho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambapo kitaifa imefanyika katika hospitali ya St....

 

9 months ago

Malunde

SERIKALI YAMWAGA AJIRA 10,184 KUZIBA NAFASI ZA WATUMISHI WENYE VYETI FEKI


OFISI ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetangaza kutoa vibali vya ajira 10,184 ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, imefahamika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais, Utumishi, Florence Temba, ilieleza kuwa agizo hilo linazihusu Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala wa Serikali, pamoja na Taasisi na Mashirika ya Umma.
Ilimnukuu Waziri...

 

10 months ago

Malunde

SERIKALI KUPANDISHWA VYEO WATUMISHI NA AJIRA MPYA KUZIBA PENGO LA WENYE VYETI FEKI


SERIKALI imetangaza neema kwa halmashauri zote nchini ikisisitiza kuwa watumishi watapandishwa vyeo na ajira mpya zitatolewa kujaza nafasi za wote waliogundulika kuwa na vyeti feki.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokutana na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Alisema sasa serikali imepanga kutoa ajira maalumu kwa kila...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani