RAIS MAGUFULI KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA BARRICK GOLD LEO JUMATATU OKTOBA 23


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 23 Oktoba, 2017 atawatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Barrick Gold.

Tanzania na Barrick Gold Corporation zilifikia makubaliano tarehe 19 Oktoba, 2017 na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi...

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Channelten

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited

Rais-John-Magufuli-750x375

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

Prof. Thornton ambaye amesafiri kwa ndege binafsi kutoka nchini Canada hadi Tanzania amekutana na Rais...

 

2 years ago

Michuzi

BREAKING NYUZZZZ....: Rais Dkt. Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya Canada Profesa John L. Thorton

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya Canada Profesa John L. Thorton Ikulu jijini Dar es salaam. Katika mkutano huo, uliohudhuriwa pia na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Paramagamba Kabudi na Balozi wa Canada hapa nchini, Ian Myles umemalizika kwa mafanikio makubwa ambapo pande zote zimekubaliana kukaa meza moja kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali katika sekta ya madini. Habari kamili yaja punde

 

2 years ago

Michuzi

WAJUMBE WA KAMATI MAALUM ILIYOUNDWA NA RAIS DKT.MAGUFULI WAENDELEA NA MAJADILIANO NA TIMU KUTOKA KAMPUNI YA BARRICK GOLD CORPORATION

Wajumbe wa kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiendelea na majadiliano na timu kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation leo Septemba 7, 2017 kuhusu madai ya Tanzania juu ya upotevu wa fedha nyingi katika biashara ya madini ya dhahabu inayofanywa na kampuni hiyo hapa nchini. Majadiliano hayo yanafanyika jijini Dar es salaam

 

2 years ago

Channelten

Rais Magufuli leo amekutana na Mkurugenzi wa Masoko ya Afrika wa Kampuni ya Boeing na kufanya mazungumzo

2

Rais John Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Masoko ya Afrika wa Kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Boeing yenye makao yake nchini Marekani Bw. Jim Deboo ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kununua ndege kubwa kutoka kampuni hiyo.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James.

Baada ya Mazungumzo hayo Rais Magufuli amesema...

 

2 years ago

Malunde

MAJADILIANO KATI YA TANZANIA NA KAMPUNI YA BARRICK GOLD CORPORATION YAMEANZA DAR LEO

Majadiliano kati ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli na wawakilishi kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo nchini yameanza leo, Julai 31 jijini Dar es Salaam. 


Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kamati ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.
Imesema kamati kutoka Barrick inaongozwa na Ofisa Mwendeshaji Mkuu, Richard...

 

2 years ago

Channelten

Majadiliano kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick Gold Coporation yameanza leo DSM

unnamed

Majadiliano kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Wawakilishi kutoka Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo hapa nchini yameanza leo Jijini Dar es Salaam.

Kamati Maalum ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi na Kamati ya kutoka Barrick Gold Corporation inaongozwa na Afisa Mwendeshaji Mkuu
Bw. Richard...

 

2 years ago

Michuzi

KAMATI MAALUM YA MAKINIKIA YA TANZANIA YAANZA MAZUNGUMZO NA BARRICK GOLD CORPORATION JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufanya mazungumzo na uongozi wa Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo hapa nchini akiulaki ujumbe wa kampuni hiyo kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo leo tarehe 31 Julai, 2017 Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU   
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa...

 

2 years ago

Channelten

Rais Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Dangote

dangote

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani