RIPOTI YA UCHUNGUZI KIFO CHA MWANAFUNZI ALIYEPIGWA RISASI NA POLISI YAZUA TAFRANI MUHIMBILI


Ndugu wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi, jana walisusia kwa muda kuchukua mwili wa binti huyo wakishinikiza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kueleza sababu za kifo chake.


Jambo hilo lilizua sintofahamu kabla ya kutulizwa kwa kuelezwa kwa mdomo na madaktari kuwa alipigwa risasi kichwani.

Jana asubuhi, ndugu hao walikusanyika katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili wakisubiri uchunguzi ukamilike ili...

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Michuzi

Ndalichako,Masauni watoa mkono wa pole kwa wafiwa kifo cha Mwanafunzi aliyepigwa risasi

  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Injinia Hamad Masauni  wakimfariji Mama Mzazi wa marehemu  Aqwilina jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar,Mwanafunzi  huyo wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuiya maandamano ya chama cha CHADEMA.Kufuatia kifo cha Mwanafunzi huyo Serikali imesema...

 

1 year ago

Malunde

SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA MWANAFUNZI ALIYEPIGWA RISASI NA POLISI DAR

Serikali imetoa pole kwa familia ya mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi Februari 16,2018 na kuahidi kugharamia mazishi yake.


Akizungumza leo Februari 18,2018 na vyombo vya habari, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema pamoja na katibu mkuu wa wizara watahakikisha wanasimamia shughuli zote za msiba huo.

Amesema Akwilina alikuwa katika majukumu yake ya kawaida akipeleka barua yake ya mafunzo kwa...

 

1 year ago

Michuzi

UCHUNGUZI WAANZA KUBAINI WALIOMUUA KWA RISASI MWANAFUNZI CHUO CHA USAFIRISHAJI

*Wizara ya Mambo ya Ndani yaelezea kinachoendelea*Rais Magufuli aagiza waliohusika wachukuliwe hatua 
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imewahakikishia Watanzania kuwa uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Aqwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi utafanyika kwa haraka na weledi mkubwa na kufafanua waliohusika na kifo hicho kwa namna yoyote ile hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Imesema tukio la mwanafunzi huyo...

 

1 year ago

Michuzi

SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI MWANAFUNZI ALIYEPIGWA RISASI

*Waziri Ndalichako asema Taifa limepata pigo kubwa, aomba utulivu
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SERIKALI kupitiza Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imesema itagharamia mazishi ya mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) Aqwilina Akwiline ambaye amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam
Imesema kifo cha mwanafunzi huyo ni pigo kubwa kwa familia, Serikali,Wizara ya Elimu,wanafunzi, ndugu, jamaa na marafiki...

 

3 years ago

RFI

Uganda yaagiza uchunguzi kuhusu raia wake aliyepigwa risasi Marekani

Serikali ya Uganda inaitaka Ubalozi wake jijini Washington DC nchini Marekani, kuchukuza na kutoa maelezo ya kina mazingira yaliyosababisha raia wake Alfred Olango kupigwa risasi na kuuawa na polisi mjini California siku ya Jumatano.

 

2 years ago

Ippmedia

Familia ya mwanafunzi aliyepigwa risasi na askari yalalamikia mtoto kutelekezwa.

Familia ya mwanafunzi iliyepigwa risasi na askari wa jeshi la polisi, wamelalamikia jeshi hilo kwa kutelekeza mgonjwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili bila kushiri katika matibabu ya mwanafunzi huyo ambaye mpaka sasabado hajaondolewa risasi katika sehemu ya mwili wake.

Day n Time: ijumaa Saa 2:00 UsikuStation: ITV

 

1 year ago

Malunde

USALAMA WAIMARISHWA KIJIJI ATAKACHOZIKWA MWANAFUNZI AKWILINA ALIYEPIGWA RISASI


Vyombo vya ulinzi na usalama vimeimarisha usalama katika eneo atakalozikwa mwanafunzi wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline katika kijiji cha Olele wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

Uchunguzi uliofanywa na MCL Digital saa 2:00 hadi saa 4:30 asubuhi leo Ijumaa Februari 23, 2018 umebaini uwapo wa askari wengi wakiwamo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na askari kanzu.
Mbali na askari kanzu, wameonekana maofisa usalama wa Taifa na polisi waliovalia kiraia, wakiwa...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Ripoti ya kifo cha AKWILINA ilyo tolewa na hospitali ya Muhimbili

Madaktari wa hospitali ya Muhimbili Jumanne hii mchana wamefikia uamuzi wa kutoa sehemu ya ripoti ya uchunguzi wa mwili wa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyepigwa risasi na Polisi Februari 16, 2018.

Hatua hiyo imekuja baada ya ndugu wa binti huyo kususa kupokea mwili wa mwanafunzi huyo uliokuwa ukifanyiwa uchunguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) bila kuelezwa nini kilichomuua.

Wakizungumza mara baada ya maafikiano baina yao na madaktari,...

 

1 year ago

Malunde

WAOMBOLEZAJI WAPORWA MABANGO WAKIAGA MWILI WA MWANAFUNZI ALIYEPIGWA RISASI DAR


Baadhi ya waombolezaji ambao walijitokeza kuaga mwili wa marehemu Akwilina aliyekuwa anasoma katika Chuo Cha Usafirishaji (NIT ) jijini Dar es Salaam wamepokonywa mabango mbalimbali ambayo yalikuwa na jumbe mbalimbali kuhusiana na kifo hicho. 
Waombolezaji hao ambao wengine walikuwa wameshika mabango kuhoji uhalali wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba na IGP Sirro kuendelea kuwepo ofisini mpaka sasa licha ya mauaji hayo kutokea.
Walijitokeza vijana mbalimbali ambao...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani