Safari za Treni ya Mwakyembe zaongezwa sasa treni kusimama Kamata awamu ya jioni kuanzia Jumatatu!

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kuongezwa kwa safari moja ya ziada kwa kila awamu ya usafiri huo kuanzia siku ya Jumatatu Aprili 25, 2016. Hivyo basi awamu ya asubuhi na ile ya jioni itakuwa na safari 4 badala ya 3 za sasa, halikadhalika muda wa kuanza safari nao umebadilishwa. Kwa awamu ya asubuhi treni ya kwanza itaondoka Ubungo Maziwa kuja kituo kikuu cha Dar es Salaam saa 12:15 ambapo itawasili saa 12:55. Safari ya mwisho ya nne itaondoka Ubungo Maziwa saa 5:15...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

4 years ago

Michuzi

HUDUMA YA TRENI YA DELUXE KUSIMAMA KATIKA KITUO CHA NGURUKA KUANZIA TRENI ITAKAYOANDOKA DAR JUMAPILI IJAYO MEI 17, 2015

Uongozi wa Kampuni  ya Reli Tanzania  –TRL unachukua  fursa hii kuwataarifu wateja wetu wote na Watanzania kwa ujumla na hasa maeneo ya kituo cha Reli cha Nguruka mkoani Kigoma, kuwa treni yetu maarufu ya Deluxe itasimama kituoni hapo kuteremsha na kupakia  abiria.
Kwa taarifa hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na Wakazi wa maeneo yanayozunguka kituo cha  Nguruka, shime  wajitokeze kwa wingi kukata tiketi za safari kwa mujibu wa mahitaji yao . Halikadhalika safari za deluxe zitakuwa wiki...

 

4 years ago

Michuzi

ABIRIA WA TRENI MKOANI DODOMA KUTUMIKA KITUO KIDOGO CHA KATOSHO BADALA YA STESHENI YA TRENI YA KIGOMA KWA TRENI ZA ABIRIA KUANZIA FEBRUARI 18, 2015

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitka kutangaza kuwa treni za abiria za kwenda Kigoma hazitofika katika stesheni ya Kigoma badala yake zitatumia kituo kidogo cha Katosho.
Kwa mujibu wa wa taarifa ya Uongozi wa TRL lilitolewa Februari 16, 2015 uamuzi wa treni  kutofika katika stesheni ya Kigoma  unatokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mjini  Kigoma na hivyo kuzoa mchanga ambao umefunika tuta la reli katika eneo la  stesheni ya Kigoma.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo abiria wote...

 

5 years ago

Tanzania Daima

ĎTreni ya Mwakyembeí kurejea Jumatatu

UONGOZI wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), imesitisha huduma ya usafiri wa treni jijini Dar es Salaam, maarufu kama ‘ Treni ya Mwakyembe’ hadi keshokutwa itakaporejea kama kawaida. Kwa mujibu...

 

3 years ago

Michuzi

UONGOZI WA KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL) LASITISHA HUDUMA YA TRENI YA JIJI MAARUFU KAMA TRENI YA MWAKYEMBE.

Shimo katika tuta la reli  eneo la Buguruni kwa Mnyamani  ambalo limesababishwa na mvua inayoendelea kunyesha hapa nchini ambapo ukarabati wa eneo hilo unaendelea ili kufanikisha usafiri kurejea hapo kesho.

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL) Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa huduma ya treni ya jiji maarufu kama Treni ya Mwakyembe awamu ya jioni ya leo Februari 09, 2016. 
Taarifa imefafanua kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na maji ya mvua kuchimba shimo kubwa...

 

5 years ago

Michuzi

Huduma ya Treni ya Jiji yaahirishwa kuanzia leo hadi Jumatatu Novemba 17, 2014

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania -TRL unasikitika kuwatangazia kuwa kuanzia leo jioni saa 10 hakutakuwepo huduma ya usafiri wa treni ya Jiji maarufu kama ' treni ya Mwakyembe' hadi siku Jumatatu Novermba 17, 2014 huduma itakaporejea kama kawaida.
Ufafanuzi wa sababu za kusitishwa huduma umeeleza kuwa kichwa kimojawapo ambacho hutoa huduma kimepelekwa Karakana Kuu ya Morogoro kwa ajili ya ukarabati maalum na kwamba kinatarajiwa kurejeshwa Dar es Salaam jioni ya siku ya...

 

4 years ago

Michuzi

TRL YASITISHA SAFARI ZA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA KUANZIA LEO

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL umetangaza kusitishwa huduma za safari ya treni abiria kuanzia leo Ijumaa Machi 06, 2015 kufuatia eneo la tuta la reli kati ya stesheni za Kilosa na Kidette kuharibika kwa mafuriko ya mvua inayonyesha hivi  sasa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Wahandisi na Mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio wakifanya tathmini ya jinsi zoezi la ukarabati utakavyofanyika na kwa muda gani.
Ikifafanua zaidi taarifa imeeleza kuwa tathmini ya mafundi hao...

 

4 years ago

GPL

SAFARI YA TRENI YA DELUXE KWENDA KIGOMA YAAHIRISHWA HADI KESHO JUMATATU

Uongozi  wa Kampuni ya Reli  Tanzania  (TRL) unasikitika kuwataarifu abiria  wa treni ya Deluxe ya kwenda  Kigoma leo Mei 17, 2015 saa 2 usiku kuwa safari hiyo imeahirishwa  hadi kesho Jumatatu Mei 18, 2015 saa 2 usiku. Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa  zinatokana na ajali mbili mfululizo za treni za mizigo. Ajali ya kwanza ilitokea asubuhi saa 1:30 maeneo ya Stesheni ya Ngeta mkoa wa Pwani na ya pili saa 5...

 

3 years ago

Michuzi

SAFARI ZA MAJARIBIO ZA TRENI YA PUGU KUANZA, JUMATATU NA JUMANNE KUWA BURE

Huduma ya 2 ya treni ya Jiji kutoka Pugu kwenda kituo kikuu cha Dar es Salaam kuanza kesho Jumatatu Agosti 01, 2016 saa 12 asubuhi.
Aidha taarifa Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL ) inafafanua huduma hiyo ya majaribio ya siku 2 Jumatatu na Jumanne itakuwa bure kwa Wakazi wa vituo husika.
Vituo hivyo pamoja na Pugu stesheni ni Mwisho wa Lami, Gongo la mboto, FFU Mombasa, Banana (Njia panda Segerea) na Karakata. Vingine ni pamoja na Vingunguti Mbuzi, SS Bakhressa, Kamata na Kituo...

 

4 years ago

Michuzi

TAARIFAKUHUSU KUAHIRISHWA SAFARI YA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA HADI KESHO JIONI JULAI 25, 2015


Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika  kuwataarifu wananchi na abiria waliokuwa wasafiri na treni ya leo Ijumaa Julai 24, 2015 kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi kesho saa 11 jioni. Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa safari hiyo ni ajali ya treni ya mizigo iliyotokea leo Ijumaa Julai 24, 2015  saa 8:15 alasiri maeneo  ya  Stesheni  za Mazimbu –Mkata mkoani  Morogoro ambapo ilihusisha mabehewa matano ya  treni ya  mizigo iliyokuwa...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani