SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA SEVENTY SEVEN HOTEL ARUSHA

Na Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

Wizara ya Fedha na Mipango imesema kuwa waliokuwa wafanyakazi wa Hoteli ya Seventy Seven ya mkoani Arusha, walioachishwa kazi mwaka 2000, wameshalipwa mafao yao kwa mujibu wa sheria na taratibu hivyo hawastahili kudai malipo yoyote ya nyongeza.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maaluum (CCM) Arusha, Mhe. Catherine Magige aliyetaka kujua ni lini Serikali itawalipa mafao waliokuwa wafanyakazi wa hoteli hiyo.

Mhe. Magige aliliambia Bunge kuwa waliokuwa wafanyakazi wa hoteli hiyo ambao waliachishwa kazi mwaka 2000, hawajalipwa mafao yao hadi sasa.

Akijibu swali hilo, Dkt. Kijaji alisema kuwa katika zoezi la ulipaji wa mafao kwa wafanyakazi hao Serikali ililipa Sh. 217,366,296 mwezi Januari, 2000 ambapo baadae walipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi hao kuwa wamepunjwa.

“Serikali baada ya kupokea malalamiko hayo, ilihakiki na baada ya kujiridhisha mwezi Agosti, 2000, ilitoa idhini ya kulipa tena kiasi cha Sh. 273, 816, 703 kwa ajili ya mapunjo ya mishahara na mafao ya wafanyakazi hao” aliongeza.

Hata hivyo, Mhe. Magige hakuridhishwa na majibu ya Dkt. Kijaji na alipopewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza alisema kuwa Serikali imewalipa wafanyakazi hao awamu ya kwanza tu na hawakupewa nyongeza yoyote licha ya kuwasilisha malalamiko hayo.

Mhe. Magige aliongeza kuwa Wizara ya Fedha ilishawahi kwenda kufanya uhakiki na kubaini kuwa kulikuwa na mapungufu, na Serikali iliipa jukumu la kusimamia malipo hayo Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo mpaka sasa bado haijalipa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii (MB), Mhe. Ramo Makani aliliomba Bunge limpe muda wa kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu ili aweze kutoa majibu sahihi.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 months ago

Bongo5

‘Wafanyakazi wa Hotel ya 77 Arusha hawatudai’ – Serikali

Wizara ya Fedha na Mipango imesema kuwa waliokuwa wafanyakazi wa Hoteli ya Seventy Seven ya mkoani Arusha, walioachishwa kazi mwaka 2000, wameshalipwa mafao yao kwa mujibu wa sheria na taratibu hivyo hawastahili kudai malipo yoyote ya nyongeza.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt Ashatu Kijaji, ameyaeleza hayo bungeni mjini Dodoma, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maaluum (CCM) Arusha, Mhe. Catherine Magige aliyehoji,

Je?, “ni lini Serikali itawalipa mafao...

 

2 years ago

Michuzi

Arusha Hotel to reopen as a Four Points by Sheraton hotel


The former Arusha Hotel, currently undergoing a major modernization and reconstruction, will reopen, according to a source from Arusha, as a Four Points by Sheraton hotel, brining another global hospitality brand to the city knows as 'The Safari Capital of East Africa'.While an exact reopening date has yet to be announced is it now known that the hotel will offer 108 suites and rooms for guests plus a range of amenities usually expected from a hotel operated under this brand.In Dar es Salaam...

 

3 years ago

Dewji Blog

Wyndham Hotel Group Opens Hotel in Dar es Salaam, First Hotel in Eastern Africa

150421w

First hotel on African continent to be operated by Wyndham Hotel Group under management contract, complementing the company’s existing franchised portfolio

 Wyndham Hotel Group (http://www.wyndhamworldwide.com), the world’s largest hotel company based on number of hotels and one of three hospitality business units of Wyndham Worldwide (NYSE: WYN), today announced the opening of the 139-room Ramada® Resort Dar es Salaam in Tanzania.

Complementing Wyndham Hotel Group’s existing portfolio of...

 

4 years ago

GPL

WAFANYAKAZI WA GLOBAL WAKIUKARIBISHA MWAKA 2014 NDANI YA JOHANNESBURG HOTEL

Wafanyakazi wa Global wakijiachia kwa kucheza muziki ndani ya Johannesburg Hotel usiku huu.…

 

2 months ago

Michuzi

WATOTO WENYE SARATANI WALA KRISMASS NA WAFANYAKAZI WA SOUTHERN SUN HOTEL





Wafanyakazi wa hoteli ya Southern Sun wakishiriki michezo na wazazi wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)  Father Christmas akitoa zawadi mmoja wa wazazi wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es...

 

3 years ago

BBC

'Seventy dead' in Kenya attack

At least 70 hostages have been killed in a militant attack on Garissa University College campus in north-eastern Kenya, officials say.

 

3 years ago

Daily News

Suspected Arusha hotel bombers in court


Suspected Arusha hotel bombers in court
Daily News
SIX people who are suspected to have taken part or at least had prior knowledge about the recent bombing incident at Varma Indian Restaurant in Arusha city, have appeared before the Resident Magistrate's Court here. Four of the accused, who were ...

 

3 years ago

TheCitizen

Popular Arusha businessman found dead inside hotel room

>Another renowned member of the Arusha business community suddenly died in a hotel room here at the weekend.

 

3 years ago

Vijimambo

KIKAKO CHA BARAZA LA UONGOZI WA KANDA YA KASKAZINI -KATIKA HOTELI YA THE NEW ARUSHA HOTEL

  Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman A.Mbowe akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini Mhe Israel Natse wakiwa wanaingia ukumbi wa JUMUIKA  Viongozi wa kuu wa Chadema Taifa pamoja na Kanda wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kikao cha baraza la kanda ya kaskazini kuanza
  Waheshimiwa wabunge wakiwa wanaimba wimbo wa Taifa  Katibu wa Kanda ya kaskazini Mhe Amani Golugwa akiwakaribisha wajumbe wa kikao cha baraza la Kanda ya Kaskazini , wajumbe wa kikao wametoka katika majimbo 33...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani