Serikali imetoa miezi sita kuanzia sasa kwa Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari kuhakikisha hili

pic+drugs

Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu ametoa miezi sita kuanzia sasa kwa wakuu wa shule za msing bna sekondari kuhakikisha wanaanzisha madawati ya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuwasikiliza wanafunzi pindi wanapokuwa na shida kwa kutenga waalimu watakaoweza kuwasikiliza na kutatua changamoto zao.

Maagizo hayo ameyatoa wilayani Tarime mkoani mara wakati wa kilele cha cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani ambapo amesema mara nyingi watoto wa shule wamekuwa wakikosa sehemu ya kufikisha shida zao jambo ambalo linachangia kukua kwa vitendo vya ukatili huku pia akiwataka kupeleka ripoti ya wanafunzi walioacha shule kutokana na ujauzito kila baada ya miezi mitatu ili serikali iweze kupata takwimu sahaihi za wanafunzi hao.

Amesema takwimu zinaonyesha kuwa watoto wa kike 100 kati ya 27 walio chini ya umri wa miaka 18 sawa na asilimia 27 hupata mimba na kukatisha masomo yao ndio maana kauli mbiu ya mwaka huu inasisitiza kuwa tokomeza mimba za utotoni kufikia uchumi wa viwanda .

Akizungumzia mikakati mbalimbali iliyojiwekesa katika kutokomeza ndoa ukatili wa kijinsia na mimba za utotoni mkuu wa mkoa wa mara Dk Charles Mlingwa amesema licha ya mkoa huo kutajwa kuwa ni miongoni mws mikoa inayokabiliwa na tatizo hilo elimu imeendelea kutolewa na kuwachukulia hatua wale wanojishughulisha na vitendo vya tohara kwa watoto wa kike huku baadhi ya mangariba walioachana na kazi hiyo wakitoa ushuhuda.

Share on: WhatsApp

The post Serikali imetoa miezi sita kuanzia sasa kwa Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari kuhakikisha hili appeared first on Channel Ten.

Channelten

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Global Publishers

Walimu wakuu 90 shule za msingi, sekondari kuvuliwa vyeo kwa udanganyifu

1.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

2.Mkuu huyo akionesha msisitizo wa jambo wakati akifafanua hoja mbalimbali zilizokuwa zimeulizwa na wanahabari.Mkuu huyo akionyesha msisitizo wa jambo wakati akifafanua hoja mbalimbali zilizokuwa zimeulizwa na wanahabari.

3.Wanahabari wakichukua tukio hilo.Wanahabari wakichukua tukio hilo.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Salum Hapi, amesema kuwa walimu wakuu 68 wa shule za msingi na 22 shule za sekondari watavuliwa vyeo  kwa kosa la udanganyifu wa takwimu  za idadi za wanafunzi hewa tangu elimu itangazwe kuwa bure katika wilaya za Kinondoni na...

 

1 year ago

Ippmedia

Serikali yabaini uwepo wa wanafunzi hewa 52783 kwa shule za msingi,12415 kwa shule za sekondari

Serikali imebaini uwepo wanafunzi hewa 52,783 kwa shule za msingi na 12,415 kwa sekondari ambao wangeliingizia taifa hasara ya zaidi ya shilingi milioni 931 ambazo zingepelekwa mashuleni kwa ajili ya ruzuku kwa mwaka wa fedha 2016/17 huku ikitamka kuwachukulia hatua kali kwa watumishi watakaobainika kufanya njama za mchezo huo mchafu unaoliingizia taifa hasara.

Day n Time: Jumatano Saa 2:00 UsikuStation: ITV

 

2 years ago

Dewji Blog

Wakuu wa shule za msingi na sekondari 90 Kinondoni kuvuliwa vyeo

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Alli Hapi amemtaka mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuwavua madaraka wakuu wa shule za msingi 68, pamoja na kumuandikia barua Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwavua vyeo wakuu wa shule za sekondari 22.

Hapi alitoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kufanya uhakiki na kubaini kuna wanafunzi hewa zaidi ya 5000 katika shule za msingi na sekondari katika manispaa hiyo.

“Rais Magufuli alitoa agizo akiwa...

 

1 year ago

Ippmedia

Serikali yakamilisha 85% ya utengenezaji wa madawati kwa shule za msingi na 99.9% Sekondari.

Serikali yakamilisha zaidi ya asilimia 85 ya utengenezaji wa madawati kwa shule za msingi na asilimia 99.9 kwa shule za sekondari huku changamoto ya uhitaji wa vyumba vya madarasa ikijitokeza.

Day n Time: Jumapili saa 2:00 usikuStation: ITV

 

2 years ago

MillardAyo

AUDIO: Wakuu wa shule 90 za msingi na sekondari kuvuliwa madaraka Kinondoni

shule

Hivi karibuni Rais Magufuli katika ziara yake mkoani Mwanza aliwaonya walimu wanaotoa taarifa za uongo za wanafunzi ili kujipatia fedha nyingi za elimu bure. Sasa wilaya ya Kinondoni Dar es salaam imefanya ukaguzi kwa shule za msingi na sekondari ambapo imebaini wanafunzi 3462 katika shule za msingi 68 na 2534 katika shule za sekondari 22 […]

The post AUDIO: Wakuu wa shule 90 za msingi na sekondari kuvuliwa madaraka Kinondoni appeared first on millardayo.com.

 

2 years ago

Michuzi

WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WAAGIZWA KUWA NA KIWANGO CHA UFAULU KUANZIA ASILIMIA 14


Na Mathias Canal, Dodoma Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi amewaagiza wakuu wa shule za Sekondari zote za Wilaya hiyo kuhakikisha wanafikia ufaulu kuanzia asilimia 41% ili kuakisi hali ya ukuaji wa ufaulu nchini na kupata wanafunzi waliopikwa vyema darasani ili kuwa na wasomi wenye weledi pasina mashaka.

Dc Ndejembi amesema kuwa hatarajii kusikia shule mojawapo Wilayani humo ikiwa imeshika mkia Kiwilaya, Mkoa ana Taifa kwani kufanya hivyo ni kuonyesha jinsi ambavyo...

 

4 months ago

Channelten

Shule za Nyasi Kuondoka , Serikali imenuia kuhakikisha ndani ya miezi kumi na mbili ijayo

SHULE ZA NYASI

Serikali imenuia kuhakikisha kuwa ndani ya miezi kumi na mbili ijayo, shule zote zilizoezekwa kwa nyasi nchini zinaondoka,ili kuhakikisha mtoto wa kitanzania anapata elimu iliyo bora katika mazingira rafiki.

Mpango huo wa serikali umetangazwa mjini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo, wakati alipokuwa akifungua Mkutano wa wadau wa ubora wa elimu nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Tabora Bw. Khamis Lissu, ameshauri...

 

3 years ago

TheCitizen

Ruzuku ya shule za msingi, sekondari kuiumbua Serikali

Dar es Salaam. Ikiwa imebaki miezi miwili mwaka wa fedha wa 2014/2015 umalizike, Serikali imetoa asilimia tisa tu ya ruzuku kwa shule za msingi na asilimia 22 ya ruzuku kwa shule za sekondari na siyo asilimia 100 kama ilivyoahidi chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), imeelezwa.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani