Serikali kufanya marekebisho ya sheria zinazoibana tasnia ya sanaa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema wizara yake inapitia upya sheria zenye mapungufu zinazo gandamiza sekta zilizochini ya wizara yake ili katika kipindi cha Bunge la Bajeti zifanyiwe marekebisho.

Nape ameyasema hayo leo katika hafla fupi ya kuwaaga wasanii wa WCB wakiongozwa na Nasib Abdul ‘Diamond’ wanaokwenda nchini Gabon kutumbuiza katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

“Wizara inapitia upya sheria zinazosimamia sekta zilizo chini ya wizara hii iili ziweze kuwa rafiki kwa wawekezaji hasa katika tasnia ya sanaa ili izidi kukua,” amesema.

Hata hivyo, Nape amesema tasnia ya sanaa inazidi kukua na kuitangaza nchi kimataifa.

“Sanaa yetu inazidi kukua na ndiyo maana wasanii wetu wanapata nafasi za kutumbuiza katika mashindano makubwa ,” amesema.

Dewji Blog

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Channelten

Serikali yakusudia kufanya marekebisho ya sheria ya manunuzi

Screen Shot 2016-04-04 at 12.35.21 PM

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Injinia GERSON LWENGE amesema serikali inakusudia kufanya marekebisho ya sheria ya manunuzi ili halmashauri zinunue mabomba ya maji kutoka viwanda vya hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda.

Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha mabomba ya maji cha Pipe Industry Company Limited kilichopo eneo la Vingunguti wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam, Waziri Lwenge amesema serikali ya awamu ya tano imedhamiria...

 

1 year ago

Michuzi

MAHAKAMA YATOA MAELEKEZO KWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KUFANYA MAREKEBISHO MOJA YA KIFUNGU CHA SHERIA YA MITANDAO

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa kupinga sheria ya mtandao iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 ili kulinda maslahi ya Taifa ya kupambana na kutoa mwelekeo wa kukabiliana na makosa ya mtandao.
Hukumu hiyo ya kihistoria ilitolewa na jopo la majaji watatu, Prof. John Ruhangisa, Winfrida Korosso na Lugano Mwandambo mara baada kuona hoja zilizowalishwa na wakili wa kujitegemea Jebra Kambole kuwa hazina msingi.
Hata hivyo, mahakama hiyo...

 

1 year ago

Michuzi

SERIKALI KUFANYA MAPITIO YA SHERIA YA SEKTA YA SANAA NA BURUDANI –WAZIRI NAPE

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.


WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema wanatarajia kufanya mapitio ya sheria zinazohusu sekta ya sanaa na burudani nchini ili kutoa fursa kwa taasisi binafsi kuwekeza zaidi.
Katika kufanya mapitio hayo wataangalia jinsi ya kufanyia kazi sheria mbovu zinazokandamiza sekta ya sanaa na burudani nchini na kuziondoa kabisa ili kuleta manufaa kwa wasanii na wadau wanaohusika na sanaa.
Nape ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam...

 

1 year ago

Ippmedia

Serikali yawasilisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali.

Serikali imewasilisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali unaolenga kufanya marekebisho na kutoa adhabu ya kifungo cha miaka sita na faini ya shilingi milioni tano kwa mkuu wa taasisi ya umma, shirika la umma, idara au wakala wa serikali atayeingia mkataba wa mkopo pasipo kupata kibali cha waziri wa fedha.

Day n Time: Jumatano Saa 2:00 UsikuStation: ITV

 

12 months ago

Mwananchi

SMZ yaahidi kufanya marekebisho ya sheria zinazowakwaza wanahabari

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema Serikali ya Zanzibar (SMZ) ipo tayari kufanya marekebisho ya sheria ambazo zinawakwaza wanahabari katika utendaji wao wa kazi ili kulinda na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari visiwani humo.

 

3 years ago

Michuzi

SERIKALI KUPELEKA BUNGENI MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itawasilisha Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wenye sehemu 14 likiwemo suala la Mahakama ya Kadhi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, jana jioni (Jumatano, Machi 11, 2015) Waziri Mkuu alisema Serikali inakusudia kuwasilisha muswada huo kwenye mkutano ujao wa Bunge unaotarajiwa kuanza Jumanne ijayo, (Machi 17).
Hata hivyo, Waziri Mkuu amewasihi Watanzania waondoe hofu iliyoenezwa na tetesi...

 

1 year ago

Michuzi

MSEMAJI WA SERIKALI: MUSWADA WA SHERIA ZA HABARI UTAIPA TASNIA HESHIMA

Na Jovina Bujulu-MAELEZO,Dar es Salaam

WANATASNIA ya habari nchini wametakiwa kuukubali muswada wa sheria wa huduma ya habari unaotarajia kuwasilishwa hivi karibuni Bungeni kwa kuwa umekusudia kuifanya taaluma hiyo kuaminika kwa jamii.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Hassan Abbas Jijini Dar es salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari vilivyopo Jijini humo.
Alisema kwa muda mrefu wadau wa Habari na wanatasnia wenyewe wamekuwa na kiu ya kupata sheria mpya baada...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Serikali ipo tayari kubadilisha sheria zinazobana tasnia ya Habari

Serikali imesema ipo tayari kushirikiana na wadau katika sekta ya habari kubadilisha baadhi ya sheria na kanuni zinazoongoza tasnia ya habari ambazo zinaonekana kubana na kukandamiza tasnia hiyo kwa kwendana na mabadiliko ya wakati na teknolojia.

 

Waziri wa Habari,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa kauli yake wakati wa ziara yake aliyoifanya katika vyombo vya habari vya IPP yenye lengo la kuangalia changamoto ambayo sekta hii ambayo inakabiliana nazo. Waziri huyo amesema wakati umefika...

 

1 year ago

StarTV

WLAC imeiomba Serikali kulipa kipaumbele suala la marekebisho ya sheria ya mirathi.

Kituo cha Msaada wa Sheria kwa wanawake WLAC kimeiomba Serikali kulipa kipaumbele suala la marekebisho ya sheria ya mirathi ya kimila kutokana na sheria iliyopo kuwa ya kibaguzi na kandamizi wanawake na watoto hali inayosababisha kushindwa kujikwamua kiuchumi.

Hatua hiyo imejitokeza kutokana na ongezeko la mashauri ya Mirathi ya wanawake na watoto yaliyoripotiwa katika kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani