Serikali kurejesha deni la shilingi bilioni 3.2 za Shirika la Posta

Serikali imeahidi kuwa italirejeshea Shirika la Posta Tanzania kiasi cha shilingi bilioni 3.2, ambazo zilitumika kuwalipa wastaafu wa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki, punde ifikapo tarehe 30, mwezi Juni mwaka huu.

Ahadi hiyo imetolewa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Ludewa, Mhe. Deo Ngalawa (CCM), aliyehoji,

Serikali ilikuwa na mpango gani wa kuwalipa Wastaafu hawa yenyewe, moja kwa moja bila ya kutumia fedha za mfuko wa Shirika hilo?. Huku mbunge huyo akitaka kujua kwanini Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mwaka 2016 ilifungia akaunti za Shirika la Posta Nchini, kutokana na kulidai Shirika hilo kiasi cha Shilingi Milioni 600, ikiwa Shirika hilo linaidai Serikali kiasi cha Shilingi Bilioni 5.

Dkt. Kijaji alisema watumishi wote wa Shirika hilo wamekwisha jiunga na mifuko ya Hifadhi ya Jamii, na wanachangia katika mifuko mbalimbali hivyo wakistaafu mifuko hiyo itakuwa ikiwalipa mafao yao na si Serikali tena. Huku akiongeza kwa kusema kuwa Serikali itaendelea kulipa madeni hayo kadri fedha zitakapopatikana, watahakikisha ifikapo Juni 30 mwaka huu fedha zote zinazodaiwa na Shirika hilo zitakuwa zimelipwa.

Mhe. Ngalawa katika swali la msingi , alitaka kujua mpango wa Serikali wa kulirejeshea Shirika hilo fedha ambazo lilitumia kuwalipa Wastaafu waliokuwa Shirika la Posta na simu la Afrika Mashariki, kunusuru Shirika hilo.

Akijibu hoja hiyo Dkt. Kijaji alisema, “Shirika limekuwa likitumia fedha zake kuwalipa Wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki, huku ikiwasilisha madai Serikalini ili lipate kurejeshewa fedha zake.”

“Hadi sasa Shirika limelipa Shilingi Bilioni 5.9 na Serikali imesharejesha kiasi cha Shilingi Bilioni 2.7, alisema malipo hayo yamekuwa yakilipwa kwa awamu ambapo kwa mwezi Novemba 2016 kiasi cha Tsh. Milioni 700,000,000 zililipwa, na Disemba 2016 Tsh. 1,000,000,000 zililipwa, na Januari 2017 Sh. 1,000,000,000 zililipwa.

Aidha Dkt. Kijaji amesema Serikali itaendelea kurejesha kiasi kilichobaki cha Shilingi bilioni 3.2 kadri fedha zitakavyopatikana.

Na Emmy Mwaipopo

Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!Share on Whatsapp

Bongo5

Read more


Habari Zinazoendana

1 week ago

Mwananchi

Serikali kurejesha deni la Sh 3.2bn za Shirika la Posta

Serikali imeahidi kuwa italirejeshea Shirika la Posta Tanzania kiasi cha shilingi bilioni 3.2 ambazo ilizitumia kuwalipa wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki ifikapo kufikia 30 Juni mwaka huu itakuwa imelipa kiasi cha Sh3.2bilioni zinazodaiwa na Shirika la Posta Tanzania.

 

5 months ago

Zanzibar 24

Waliotafuna shilingi bilioni 3 shirika la Posta sasa matatani

Watendaji wa Shirika la Posta watafuna kijanja Shilingi bilioni 3 kwa kisingizio cha malipo ya mafuta ya magari ambayo yalikuwa hayatembei yalikuwa kwenye matengenezo.

Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Luteni Kanali Mstaafu Dkt. Haroun Kondo ameuagiza uongozi wa shirika kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahusika.

Kwa mujibu wa Dkt. Kondo, ubadhirifu ndani ya shirika hilo umevuka mipaka na kamwe hauwezi kuvumilika ambapo ametaja baadhi ya mianya ya wizi kuwa ni katika uendeshaji na...

 

7 months ago

Channelten

IPTL yapinga TANESCO kulipishwa Deni la Shilingi Bilioni 311

screen-shot-2016-09-25-at-4-04-05-pm

Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL) imepinga maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICSID) , yenye kuiamuru TANESCO kuilipa Standard Chartered Bank Hong Kong, kiasi cha dola za kimarekani milioni 148.40 kwa madai kuwa benki hiyo imetumwa na IPTL kudai deni hilo.

IPTL imekanusha kuitambua  Standard Chartered Bank ya Hong Kong kama wadai wao, na kueleza kuwa wanashangaa kwa nini benk hiyo inasimama na kuanza kuwadai Tanesco deni...

 

5 months ago

Ippmedia

Bodi ya wakurugenzi shirika la Posta watakiwa kuwachukulia hatua wafanyakazi waliotafuna Bilioni 3.

Menejimenti ya shirika la Posta imetakiwa kuwachukulia hatua wafanyakazi wake waliolisababishia shirika hilo hasara ya shilingi bilioni tatu kwa kulipa malipo yenye utata ikiwemo magari yaliyoharibika zamani kuonekana bado yanatumika na kujazwa mafuta kila siku.

Day n Time: Alhamisi saa 2:00 usikuStation: ITV

 

1 week ago

Michuzi

SERIKALI KULILIPA SHIRIKA LA POSTA SH. BIL 3.2

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali imeahidi kuwa italirejeshea Shirika la Posta Tanzania kiasi cha shilingi bilioni 3.2 ambazo ilizitumia kuwalipa wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki ifikapo kufikia 30 Juni mwaka huu itakuwa imelipa kiasi cha Sh. Bil.3.2 zinazodaiwa na Shirika la Posta Tanzania

Ahadi hiyo imetole Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na MIpango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa...

 

1 year ago

Michuzi

SHIRIKA LA POSTA KUZINDUA HUDUMA YA "POSTA MLANGONI" APRILI 5 MWAKA HUU.

SHIRIKA la Posta Tanzania linatarajia kuzindua huduma  mpya POSTA MLANGONI ambapo kila mwananchi atapelekewa kufurushi, taarifa au bidhaa zilizotumwa kwa kupitia Ofisi za Posta.
Hayo yamesemwa na  Kaimu Posta Master Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Fortunatus Kapinga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Shirika hilo litaanza na kata 48 ya Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar Unguja kata 2 na Pemba kata 4.
Kapinga amesema kuwa kata za Tanzania...

 

1 year ago

Dewji Blog

Shirika la Posta Tanzania laadhimisha Siku ya Posta Barani Afrika


Mkuu wa Uhusiano Shirika la Posta Tanzania (TPC), Wilfred Miigo, akitoa utambulisho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Posta Barani Afrika jana jijini Dar es Salaam. Katikati waliokaa ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Fortunatus Kapinga, kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika, Janeth Msofe na kulia ni Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika, John Lukonge. (Picha zote na Kassim Mbarouk- www.bayana.blogspot.com)

Kaimu Meneja Shughuli za Biashara za Fedha, Mourus Obwana,...

 

3 years ago

Mwananchi

Serikali kulipa riba Sh5 bilioni deni la miezi sita

Serikali italazimika kulipa hasara ya zaidi ya Sh5.2 bilioni (Dola za Marekani milioni 3.1) ambazo ni riba ya malimbikizo ya malipo ya miezi sita kwa Kampuni ya Jacobsen Elekron AS inayotekeleza awamu ya kwanza ya mradi wa umeme wa Kinyerezi, Dar es Salaam.

 

7 months ago

Channelten

Serikali yapata hasara ya Shilingi Bilioni 23.14

__800x800_54fe7f13b0908

Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma PPRA, umebaini serikali kupata hasara ya takribani shilingi bilion 23.14 kutokana na ukiukwaji wa sheria na taratibu za manunuzi ya umma kwenye mikataba 49 kutoka kwenye taasisi nane za umma.

Sababu kubwa ya hasara hiyo, PPRA imezielezea kuwa ni udhaifu katika kuandaa mipango na kufanya upembuzi yakinifu uliosababisha ongezeko la gharama za miradi, matumizi ya nyaraka za zabuni zisizo sahihi, bei kubwa isiyoendana na ile ya soko na udhaifu katika...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani