SERIKALI WILAYANI HANDENI YAPIGA MARUFUKU UUZAJI HOLELA WA MKAA

Serikali wilayani Handeni imepiga marufuku uuzaji holela wa mkaa ili kudhibiti matumizi mabaya ya rasilimali za misitu NA kuwataka wananchi kutumia vituo rasmi kuuza na kununua mkaa. 
Marufuku hiyo ilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alipokuwa akizindua vituo maalumu vilivyotengwa kwaajili ya kuuzia mkaa (mkaa centre) vinavyotarajiwa kuwa mazingira rafiki kwa vijana wanojihusisha na biashara za mikaa wilayani hapa. 
Mh Gondwe alisema "ni marufuku kuanzia sasa mtu yeyote kuuza mikaa kwenye maeneo ambayo sio vituo rasmi, mkaaa utauzwa na kununuliwa kwenye vituo vilivyopangwa atakayekiuka hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”. Aliongeza kuwa lengo kuu la kuweka vituo vya kuuzia mkaa ni kudhibiti matumizi mabaya ya rasilimali za misitu; Kulingana na sera ya ukusanyaji mapato,kwa kutumia vituo hivi serikali itaweza kupata mapato yake ambayo hapo awali kulikua na utoroshaji na ukwepaji wa kulipa kodi kwa wavunaji na wauzaji wa mikaa.
Mkuu wa wilaya aliwataka wavunaji wa mkaa kuunda vikundi ambavyo vitawatambulisha na kusaidia kuwa na umoja utakaopelekea kupata vibali halali vya uvunaji wa mazao ya misitu. Alisema kuwa utaratibu huo utasaidia kuwepo kwa uvunaji endelevu ambao utahusisha kupanda miti na kuvuna tofauti na ilivyokuwa awali watu wanavuna miti bila kupanda miti mingine ili kufidia ile iliyovunwa hali itakayoiepusha Handeni kuwa jangwa na kuharibu vyanzo vya maji.
Aliwaeleza wananchi kuwa vituo hivyo vitasaidia kuwa na bei elekezi ambayo itawanufaisha wafanyabiashara wote tofauti na awali ambapo kulikua na ushindani mkubwa uliopelekea wengine kujaza lumbesa ili kupata wateja kwa haraka. Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe na wataalamu wakipata maelekezo mafupi juu ya moja ya kituo cha kuuzia mkaa cha Manga.
Mkurugenzi akionesha baadhi ya vibakuli vilivyokamatwa ambavyo vilitengenezwa na mti aina ya mkarambati tayari kwa kusafirisha kuelekea nchini Kenya kwa mauzo.Meneja wa wakala wa Misitu Tanzania wa Wilaya ya Handeni akizungumza na wafanyabiashara wa mazao ya misitu ya Mkaa wakati wa Uzinduzi.Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe na Meneja wa wakala wa Misitu wa Wilaya Bw. Elias Mwaijere wakitoka kuzindua kituo cha wauza mkaa cha MangaMkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akizungumza na wafanyabiashara wa mkaa wakati wa Uzinduzi . Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe akizungumza na wafanyabiashara wa Mkaa.
Alda sadango,Afisa habari Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Habarileo

Handeni wapiga marufuku mkaa kuuzwa holela

SERIKALI wilayani Handeni imepiga marufuku uuzaji holela wa mkaa ili kudhibiti matumizi mabaya ya rasilimali misitu na kuwataka wananchi kutumia vituo rasmi kuuza na kununua mkaa.

 

1 year ago

Mwananchi

Uuzaji mkaa holela waikosesha Serikali Sh2 trilioni kwa mwaka

Imebainika kuwa Serikali inapoteza mapato ya zaidi ya Sh2 trilioni kwa mwaka kupitia biashara ya mkaa, huku misitu ya asili ikiharibiwa kutokana na ukataji miti kwa ajili ya nishati hiyo, kuni na ujenzi.

 

2 years ago

StarTV

Serikali yapiga marufuku uuzaji matunda yaliyokatwa

Serikali imetoa tahadhari ya ugonjwa wa kipindupindu kuendelea kuwa tishio kwa baadhi ya mikoa nchini tangu ugonjwa huo uliporipotiwa Agosti 15 mwaka huu.

Tahadhari hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipozungumza Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema kusambaa kwa ugonjwa wa Kipindupindu nchini kunaendelea kwa kasi tangu iliporipotiwa kwa mara ya kwanza mwaka huu Agosti 15,...

 

2 years ago

Bongo5

Serikali yapiga marufuku uuzaji wa ardhi zinazomilikiwa kimila

Serikali imepiga marufuku uuzaji wa ardhi zinazomilikiwa kimila kupitia mikataba ya muda mrefu kwa watu binafsi au taasisi, kwa kuwa sehemu kubwa ya ardhi inayomilikiwa na vijiji kwa sasa ndio imegeuzwa shabaha kubwa ya wawekezaji wa nje na wa ndani.

LUKUVI3535

Maneno hayo yalisemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, wakati akihojiwa katika kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ kinachorushwa na TBC 1. Alisema kuwa kuanzia sasa hakuna kijiji chochote kitakachoruhusiwa kuwasilisha...

 

1 year ago

Channelten

Pombe inayofungwa kwenye Viroba Serikali yapiga marufuku uzalishaji, uuzaji, uingizaji na matumizi

Serikali imepiga marufuku uzalishaji, uuzaji, uingizaji nchini na matumizi ya pombe inayofungwa kwenye viroba, ambapo kuanzia machi mosi mwaka huu atakayebanika kutumia atawajibishwa kwa kulipa faini, kufungwa jela au vyote kwa pamoja.

Uamuzi huo wa serikali ni kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaotokana na kuzagaa kwa vifungashio hivyo, kudhibiti upatikanaji rahisi wa pombe hiyo kunakosababisha kuongezeka kwa matumizi ya pombe kali hadi kwa watoto ambapo pia amesema kutumika kwa viroba...

 

2 years ago

Michuzi

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UUZAJI, UNUNUZI WA KARAFUU KWA ‘VIKOMBE’ KUEPUSHA WIZI NA UKATAJI MIKARAFUU.

 Mkulima wa karafuu wilaya ya Wete akionyesha matawi ya mkarafuu yaliyokatwa na wezi shambani kwake kwa lengo la kuiba karafuu.


Na Ali MohamedSERIKALI imepiga marufuku uuzaji na ununuzi wa karafuu usio rasmi (vikombe) kuepusha wizi wa karafuu mashambani na ukataji wa mikarafuu unaofanywa na baadhi ya watu kutokana na kuzoeleka kwa biashara hiyo. 
Wakizungumza katika nyakati tofauti Wakuu wa Wilaya za Unguja na Pemba wamesema hakuna ruhusa kwa mtu yoyote kuuza au kununua karafuu mbichi au kavu...

 

1 year ago

Michuzi

UONGOZI HANDENI WAPIGA MARUFUKU UFUGAJI HOLELA


Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe  na Mkurugnzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe wamepiga marufuku ufugaji holela. Tamko hilo limetolewa baada ya uongozi wa kijiji cha Chogo Kata ya Kabuku Ndani kuomba Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji kuwasaidia kuondoa wafugaji waliovamia katika kijiji chao na kuharibu mazao ya kilimo ya wananchi wa kijiji hicho.
Akizungumza na wananchi hao Mkuu wa wilaya aliwaeleza wananchi kuwa kila sehemu kuna taratibu na...

 

10 months ago

BBCSwahili

Tanzania yapiga marufuku uuzaji wa mahindi nje

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameonya kuwa ulanguzi wa chakula nje ya taifa hilo unatishia usalama wa chakula nchini humo.

 

2 years ago

StarTV

Uuzaji Ardhi Kiholela  Serikali  ya Wilaya  Kinondoni yapiga marufuku  

Serikali imepiga marufuku kuuza maeneo katika kata tatu zilizopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kutokana na kukithiri kwa migogoro ya ardhi.

Kata hizo ni Mabwepande, Wazo na Bunju zenye mitaa saba ambayo ni Boko, Mji mpya, Mbopo, Kihonzile, Bunju B, Mabwepande na Nyakasange.

 Kauli hiyo ilitolewa  Dar es Salaam , Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati alipokutana na viongozi wa kamati ya ardhi kwa lengo la  kutoa maazimio yao kuhusu utatuzi wa migogoro ya ardhi ndani ya...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani