SERIKALI YAKIRI KUINGIZWA MKENGE SAKATA LA AIRTEL,TTCL

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango jana tarehe 11 Januari, 2018 amewasilisha taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza umiliki wa kampuni ya simu Airtel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyeagiza kufanyika kwa uchunguzi huo tarehe 20 Desemba, 2017.

Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, Dkt. Mpango amesema Serikali imejiridhisha kuwa ubinafsishaji wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kwenda Celtel, baadaye kuhamishiwa Zain na sasa Airtel ulifanyika kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu.

Kufuatia ukiukwaji huo Dkt. Mpango amesema Serikali inayomiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni ya Airtel imeamua kufanya mazungumzo na kampuni ya Airtel inayomiliki asilimia 60 ya hisa ili nchi iweze kupata haki yake.

“Lakini niwaambie Watanzania yale ambayo tumeyaona ni machafu sana, ni mambo ya hovyo kabisa, nchi yetu kwa kifupi tuliingizwa mkenge, ni fedha nyingi zimepotea kwa hiyo sisi katika majadiliano haya lengo letu litakuwa ni kuhakikisha Watanzania wanapata haki yao” amesema Dkt. Mpango.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amepokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa tarehe 25 Novemba, 2017 wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi (Mloganzila) kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.

Baadhi ya maagizo hayo ni kupunguza baadhi ya idara na madaktari katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kuhamishia Mloganzila na hospitali za mikoa kuhamishwa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mhe. Ummy Mwalimu amewasilisha taarifa hiyo akiwa ameongozana na viongozi wakuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKHI), Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi (MUHAS).

Katika hatua nyingine, Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amekamilisha kanuni za sheria ya madini namba 7 ya mwaka 2017 na kuwasilisha vitabu vya kanuni hizo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Akiwa na Naibu Mawaziri wa Madini Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo na Mhe. Doto Mashaka Biteko, Prof. Kabudi amesema kanuni hizo zimekamilika siku moja kabla ya tarehe ya mwisho iliyotolewa na Mhe. Rais Magufuli na kubainisha kuwa sasa sheria inaweza kuanza kutumika.

Kwa upande wao Naibu Mawaziri wa Madini wamewataka Watanzania na wadau wote wa sekta ya madini kushirikiana na Serikali kutekeleza sheria hiyo na wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kutoa msukumo wa kukamilishwa kwa kanuni hizo.

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

4 months ago

Malunde

SAKATA LA AIRTEL BALAA....TTCL WAJILIPUA

IKIWA imepita siku moja tangu Rais John Magufuli amwagize Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, kuchunguza undani wa suala la umiliki wa kampuni ya simu ya Airtel, siri zaidi kuhusiana na kile kilichofanyika katika ‘dili’ za mauziano zimeanza kuanikwa.
Akizungumza mjini Dodoma juzi, Rais Magufuli alimtaka Dk. Mpango kuchunguza  undani wa kampuni ya Airtel baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa kampuni hiyo inapaswa kuwa chini ya umiliki wa Kampuni ya Simu (TTCL),  ambayo ni ya serikali....

 

4 years ago

Mwananchi

UWEKEZAJI: Serikali, Airtel wavutana hisa za TTCL

>Kumekuwa na mvutano mkali baina ya Serikali na Kampuni ya simu za mkononi ya Bharti Airtel kuhusu hatima ya asilimia 35 ya hisa ambazo kampuni hiyo inamiliki ndani ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

 

1 year ago

Habarileo

Serikali nusura kuingizwa ‘chaka’ la bilioni 4.1/-

SERIKALI imechelewa kuwalipa mawakala wa usambazaji wa pembejeo kutokana na hesabu zao kwenda kinyume na hali halisi.

 

2 years ago

TheCitizen

Airtel signs deal with TTCL

Airtel Tanzania (Airtel)  has signed an agreement with Tanzania Telecommunications Company Limited (TTCL) to complete the sale of its 35% shareholding in the fixed line business to the Government of Tanzania.

 

3 years ago

StarTV

Uchaguzi serikali za mitaa, Serikali yakiri kuwepo na kasoro lukuki.

Na, Winifrida Ndunguru

Dar Es Salaam.

15 December 2014

 

 

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA: Serikali yakiri kuwepo na kasoro lukuki.

 

 

Serikali imekiri kuwepo kwa kasoro luluki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika nchini kote Jumapili wiki hii likiwemo suala zima la mkanganyiko wa jina la mgombea kuonekana katika chama kingine.

 

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Hawa Ghasia, amesema kutokana na kasoro hizo ameitaka mikoa...

 

2 years ago

Mwananchi

Bharti Airtel yafunga virago TTCL

Kampuni ya simu za mkononi ya Bharti Airtel  leo imesaini na kuingia makubaliano ya kuachia hisa zao 35% walizokuwa wakimiliki katika kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ili Serikali iweze kumiliki kampuni hiyo kwa asilimia 100.

 

4 years ago

TheCitizen

Govt, Airtel fail to agree on TTCL shares

>Discussions between the government and a mobile phone company, Bharti Airtel, with regard to the fate of Airtel’s 35 per cent shares in Tanzania Telecommunications Company Ltd (TTCL) are stuck, The Citizen has learnt.

 

2 years ago

Michuzi

Ubia wa TTCL na Bharti Airtel Wafikia Kikomo


Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Profesa Tolly Mbwete (katikati) hati ya mauzo ya hisa asilimia 35 za Kampuni ya Bharti Airtel Afrika. Serikali imezinunua rasmi hisa za kampuni hiyo ndani ya TTCL ambapo leo wamesaini mkataba wa mauziano wa hisa hizo. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria akishuhudia.
Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (kushoto waliokaa) akitiliana saini na Ofisa ...

 

2 years ago

Michuzi

BHARTI AIRTEL COMMITS TO TANZANIA AS IT EXITS TTCL

Airtel Tanzania (Airtel) announced that it has signed an agreement with Tanzania Telecommunications Company Limited (TTCL) to complete the sale of its 35% shareholding in the fixed line business to the Government of Tanzania.
Airtel Africa’s Executive Chairman, Christian de Faria said, “The completion of the sale of Bharti Airtel’s shareholding in TTCL to the Government marks the end of a long and mutually beneficial journey in fixed line telecommunications.
Airtel remains committed to...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani