SERIKALI YALIPA MADENI YA WALIMU TANZANIA


Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imelipa madeni ya fedha za likizo kwa walimu 86,234 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/17.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Stella Manyanya wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
“Serikali inaendelea kulipa madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha za likizo kwa walimu/Watumishi katika sekta ya Elimu”,Aliongeza Mhe.Manyanya.
Amesema kuwa katika kipidi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi mwezi Juni, 2016 jumla ya shilingi bilioni 22,629,352,309 zililipwa kwa walimu 63814, na pia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 hadi kufikia mwezi Machi, 2017 jumla ya shilingi bilioni 10,505,160,275 zimelipwa kwa walimu 22420.
Aidha katika malipo haya jumla ya shilingi 13,415,410 zimelipwa kwa ajili ya madeni ya fedha za likizo kwa watumishi wa chuo cha ualimu Korogwe.Akizungumzia upande wa upandishaji madaraja Mhe.Manyanya amesema kuwakwa sasa uhakiki wa watumishi unaendela na ukikamilika watapandisha madaraja kama inavyotakiwa.
Aidha amesisitiza kuwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imekuwa ikiwapandisha vyeo watumishi wake wenye sifa kila mwaka ambapo katika mwaka 2015/16 Wizara iliwapandisha vyeo watumishi 2272 kati yao watumishi 71 ni wa chuo cha ualimu korogwe.
Uhakiki wa madeni ya miaka ya nyuma unaendelea kuratibiwa na mamlaka husika na taratibu za malipo zitakamilishwa kwa wale wanaostahili.Na Daudi Manongi-MAELEZO.

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Habarileo

‘Serikali yalipa madeni yote ya walimu’

SERIKALI imetoa ufafanuzi kuhusu madeni ya walimu kwa kusema imeshalipa yote ya mwaka jana na kwa mwaka huu, orodha inaandaliwa. Orodha kwa ajili ya madeni ya mwaka huu, inasubiriwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) kabla ya malipo kufanyika.

 

1 year ago

Michuzi

SERIKALI YALIPA MADENI YA FEDHA ZA LIKIZO KWA WALIMU 86,234 NCHINI.

Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imelipa madeni ya fedha za likizo kwa walimu 86,234 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/17.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Stella Manyanya wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
“Serikali inaendelea kulipa madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha za likizo kwa walimu/Watumishi katika sekta ya Elimu”,Aliongeza Mhe.Manyanya.
Amesema kuwa katika...

 

7 months ago

Michuzi

SERIKALI YALIPA MADENI YA NDANI BILIONI 190 KATIKA KIPINDI KIFUPI

Benny Mwaipaja, KAGERA
Serikali imelipa madeni ya wazabuni, wakandarasi na malimbikizo ya wafanyakazi yanayofikia kiasi cha shilingi bilioni 190 katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu baada ya kufanya uhakiki wa madeni halali inayodaiwa na wafanyakazi na watoa huduma mbalimbali.
Hayo yamesemwa Mjini Bukoba mkoani Kagera na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Ashatu Kijaji (Mb), wakati akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa mkoa huo akiwa katika...

 

3 years ago

Mtanzania

Serikali yalipa walimu bil 1.9/-

Asifiwe George na Imani Nathaniel (RCT), Dar es Salaam

CHAMA cha Walimu Tanzania Mkoa wa Dar es Salaam, kimesema Serikali imeanza kulipa deni la madai ya walimu kiasi cha Sh 1,936,572,146.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CWT wa mkoa huo, Amina Kisenge, alisema kwa kipindi cha  kuanzia mwaka 2013 hadi Julai 2015 walikuwa wanaidai Serikali kiasi cha Sh 3,916,432,471.

Alisema kwa sasa deni lililobaki ni Sh  1,979,860,325 ambazo bado walimu wanadai.

Alisema pamoja na...

 

3 years ago

Mwananchi

Serikali yaanza kulipa madeni ya walimu

Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, imeanza kulipa madeni ya walimu yanayofikia Sh162.1 milioni.

 

1 year ago

Mwananchi

Serikali imalize kulipa madeni ya walimu

Gazeti hili toleo la jana kulikuwa na habari iliyomnukuu Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba akitishia kuwa chama hicho kitatangaza mgogoro na Serikali iwapo haitawalipa madai yao ya zaidi ya Sh800 bilioni.

 

3 years ago

Habarileo

CWT yaitaka serikali ilipe madeni ya walimu

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimeitaka Serikali kutekeleza ahadi ya kulipa madeni ya fedha za walimu ambayo yamewasilishwa serikalini ili kuepusha kutokea msuguano katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

 

4 years ago

Habarileo

Serikali yataja mikakati ya kulipa madeni ya walimu

SERIKALI imeweka bayana mikakati yake ya kukabiliana na deni la walimu, ambao ni sehemu kubwa ya watumishi wake.

 

4 years ago

Habarileo

Serikali yatenga fungu nono kulipa madeni ya walimu

FUNGU nono limetengwa kwa ajili ya walimu wanaodai malimbikizo ya mishahara na masurufu.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani