SERIKALI YASITISHA UTOAJI WA MAENEO MAPYA YA UTAWALA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imesitisha zoezi la kutoa maeneo mapya ya utawala hadi itakapotangazwa vinginevyo. 
"Kwa sasa tumesitisha kutoa maeneo mapya ya utawala ili tuimarishe kwanza yale ya awali. Tunaimarisha kwanza miundombinu ya majengo ya ofisi,  nyumba za watumishi kwenye wilaya na Halmashauri mpya, zikitengamaa tutafanya maamuzi mapya, " alisema. 
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Ijumaa,  Agosti 11, 2017) katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Ulyankulu na Kaliua, wilayani Kaliua mkoani Tabora.  Alikuwa akijibu maombi ya wabunge wa majimbo ya Ulyankulu na Kaliua ambao walisema kuna haja ya kuigawa wilaya ya Kaliua ili kusogeza huduma kwa wananchi waishio kwenye kata zilizo mbali na tarafa. 
Akizungumzia kuhusu migogoro baina ya wanavijiji na maeneo ya hifadhi, Waziri Mkuu alisema Serikali bado inafanya uhakiki wa mipaka katika maeneo ya hifadhi na ikikamilisha zoezi hilo itatoa taarifa. 
Ili kuharakisha zoezi hilo,  Waziri Mkuu amewataka wananchi wanaoishi pembezoni mwa vijiji vinavyopakana na maeneo ya hifadhi, wasifanye upanuzi wowote hadi zoezi la kuhakiki mipaka ya hifadhi litakapokamilika.
"Tumeamua kuweka beacons katika maeneo yote ya hifadhi ili kubaini mipaka imepita wapi.  Wananchi mkiwaona watu wa hifadhi wanapita huko msigombane nao. Ni hatua ya awali ya kubaini maeneo ya mipaka. "
"Niwasihi wanavijiji wote, vijiji vilivyomo kwenye hifadhi visiendelee kupanua maeneo yake. Mbaki hivyo hivyo hadi Serikali itakapoamua vinginevyo, " alisema.  Alisema zoezi la uhakiki wa mipaka ya hifadhi likikamilika na taarifa kutolewa, Serikali itatoa uamuzi juu ya vijiji vilivyobainika kuwa ndani ya maeneo ya Hifadhi. Akiwa Kaliua, Waziri Mkuu alielezwa na Mbunge wa jimbo hilo,  Mheshimiwa Magdalena Sakaya kuwa wananchi wanashindwa kujenga makazi ya kudumu katika maeneo waliyopo kwa sababu wanatishiwa kwamba wapo hifadhini.  Waziri Mkuu alisema Serikali inafanya mapitio na ikilazimu itabidi ifanye marekebisho ya Sheria inayohusu Misitu ya Hifadhi pamoja na Sheria inayohusu masula ya Wakimbizi. 

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 months ago

Malunde

WAZIRI MKUU: SERIKALI HAINA MPANGO WA KUANZISHA MAENEO MAPYA YA UTAWALA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haina mpango wa kuanzisha maeneo mapya ya utawala hadi ikamilishe kuboresha miundombinu kwenye maeneo iliyoyaanzisha.
“Ili kutimiza azma hiyo, Serikali katika mwaka wa fedha 2017/2018 imetenga kiasi cha shilingi bilioni 412.38 kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, Serikali imetenga shilingi bilioni 16.985 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya majengo ya ofisi na makazi ya viongozi katika mikoa yote mipya,” amesema Waziri Mkuu.
Waziri...

 

9 months ago

Channelten

Changamoto ya maeneo ya kuzikia, Serikali yatakiwa kutenga maeneo mapya

E84A7900

Baadhi ya wakazi wa Kimara jijini Dar es salaam wameiomba Serikali kupitia Mamlaka za Mtaa kutenga upya maeneo ya kuzikia kwa kuwa maeneyo yaliyopo yamejaa, hali inayolazimu kuchimba maeneo yaliyokwishatumika miaka ya nyuma na kuzika upya wafu wengine.

Wakizungumza na channel wakazi hao wamesema kwa sasa heshima ya binadamu inakiukwa kufuatia ufinyu wa maeneo ya kuzikia, ambapo mara kwa mara wachimba makaburi wamekuwa wakikutana na miili ya binadamu iliyozikwa siku nyingi, hivyo kulazimika...

 

2 years ago

Michuzi

Serikali yasitisha tamko la utoaji wa Chakula Muhimbili.

Na Ally Daud-Maelezo

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , imesitisha tamko la utoaji wa vyakula kwa wagonjwa watakaolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kupisha utafiti wa kina kuhusu huduma hiyo ili kuweza kutoa kilicho bora kwa watanzania.

Akizungumza hayo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu amesema kwamba wameamua kusitisha mpango mpaka watapotangaza tena ili...

 

2 years ago

Global Publishers

Serikali Yasitisha Tamko la Utoaji wa Chakula Hospitali ya Muhimbili

1.Waziri-wa-afyaMaendeleo-ya-jamii-Wazee-na-watoto-Ummy-Mwalimu-akisoma-taarifa-yake.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Ummy Mwalimu. Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , imesitisha tamko la utoaji wa vyakula kwa wagonjwa watakaolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kupisha utafiti wa kina kuhusu huduma hiyo ili kuweza kutoa kilicho bora kwa Watanzania. Akizungumza hayo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Ummy Mwalimu amesema kwamba...

 

2 years ago

StarTV

Bomoabomoa  Serikali yasitisha katika baadhi ya maeneo

 

Hatimaye Serikali imeamua kusitisha bomoa bomoa katika baadhi ya maeneo hatarishi mkoani Dar es Salaam isipokuwa bonde la Msimbazi ambapo operesheni hiyo itaendelea na Serikali itawafidia na kuwatafutia makazi wale wote wenye vielelezo vinavyowaruhusu kuishi katika maeneo hayo.

Akitangaza uamuzi huo, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Januari Makamba amesema kusitishwa kwa operesheni hiyo kunapisha kufanya uhakiki mpya wa baadhi ya nyumba zilizowekewa alama ya kubomolewa...

 

12 months ago

Mwananchi

LHRC waitaka serikali kurasimisha maeneo mapya ya utalii

Bagamoyo. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeitaka serikali kurasimisha maeneo mapya ya utalii na kuboresha yaliyopo ili kukuza utalii wa ndani na wa kimataifa.

 

3 years ago

BBCSwahili

Sony yasitisha utoaji Sinema

Kampuni ya Sony imetangaza kusitisha mpango wake wa awali wa kutaka kutoa na kusambaza sinema dhidi ya Korea Kaskazini.

 

2 years ago

VOASwahili

Benki ya Dunia yasitisha utoaji mikopo kwa Uganda

Benki kuu ya dunia siku ya Jumatano ilitangaza kusitishwa kwa utoaji wa mikopo kwa serikali ya Uganda kutokana na kile ilichokiita matumizi mabaya ya mikopo ambayo imetolewa tayari. Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, na Benki hiyo, usitishwaji huo ulianza kutekelezwa tarehe 22 mwezi Agosti. World Bank imesema kuwa inatathmini upya masharti ya mikopo hiyo, pamoja na ripori za kukiuka kanuni zilizotolewa. Taarifa hiyoilieleza kuwa kumekuwa na visa vya kucheleweshwa kwa...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani