Serikali yaunga mkono juhudi za TFF kuinua soka la vijana

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema kwamba inaunga mkono juhudi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika programu za maendeleo ya vijana, hususani nia yake ya dhati kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan mwaka 2020.

Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omari ndiye aliyesema hayo mara baada ya kusikia program za TFF kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Makamu Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki.

“Nimesikia program mbalimbali za TFF, naona zinakuja wakati mwafaka. Nimewapongeze kwa mipango yenu mizuri kwa sababu inaleta matumaini. Jambo kubwa ambalo linanisukuma na kuwapongeza ni kuwa na program ya vijana, hatuwezi kufanikiwa kama hatutakuwa na program ya vijana.

“Serikali inatambua haya yote mnayofanya. Na ili kuboresha, Serikali imetenga shule 55 ambazo zitakuwa ni maalumu kwa ajili ya vijana, lengo ni kupata vipaji bora ambavyo vitakuwa vikiendelezwa, huku wakiwa wanapata elimu.

“Watanzania wana kiu kubwa ya mafanikio, lakini tunafikaje katika katika safari hii tunayoianza leo? Tutafika tu, iwapo kutakuwa na ushirikiano licha ya kutoangalia aina ya usafiri ambao tutatumia,” alisema Singo huku wadau wa mpira wa miguu wakimsikiliza kwa makini.

Aliendelea, “Nasikia mmeunda Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu hususani vijana. Ni jambo zuri, lakini rai yangu ni kwamba watakaunda kamati ya mfuko huo wawe watu respected ili wananchi waipende na ikiwa hivyo itafanikiwa. Sisi Serikali tutafanya kazi bega kwa bega na kamati hiyo. Jambo kubwa, ni kwamba lazima tukutane mara kwa mara.”

Kabla ya Mkurugenzi Singo kuzungumza, Makamu Rais wa TOC, Ndugu Tandau, alipongeza pia harakati za kuanza mapema akisema: “Shukrani TFF kwa kuthamini TOC. Ni vizuri tumeanza mapema. Michuano ya Olimipiki ni mikubwa na inahitaji timu zenye viwango vya juu kufanikiwa kufuzu.”

Alieleza hadhara iliyohudhuria hafla hiyo, kuwa TOC inakuwa na Mawasiliano ya maandalizi Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki inayoitwa ‘Olympic Solidarity Program’ ambayo hutoa sehemu ya fungu ya maandalizi na kwamba TFF haina budi kuwasilisha program yake kwa ajili ya kuingia kwenye bajeti ambayo inaitwa ‘Team Support Grant’.

“Sasa tuwe kitu kimoja toka huu mwanzo na mambo yaende kwa uwazo na kupeana taarifa kila wakati,” alisema Tandau.

Awali kabla ya viongozi hao kuzungumza, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kinachofanywa sasa na Shirikisho si kutafuta miujiza kwenye matokeo badala yake ni kujenga timu (Maandalizi) kwa dhana kwamba, “Timu za Taifa haziokotwi kama embe dodo.”

“Mhe. Mkurugenzi, kujenga timu hizi ni gharama kubwa. Hata matunda ambayo tunasubiri moshi mweupe ya timu ya vijana, hayakutokea hivi hivi ni maandalizi. Si ajabu kabla ya mwisho wa wiki hii tukaona moshi mweupe,” alisema Malinzi.

Alisema ili vijana wa Tanzania waweze kufanya vema, hakuna budi wadau wakiwamo Serikali, Kampuni, Mashirika ya umma na watu binafasi kusapoti mbio hizo za kwenda Tokyo, Japan pamoja na timu nyingine za taifa. “Programu nzima ni gharama kubwa,”

Kadhalika, ili kutekeleza program hiyo, Rais Malinzi alizungumzia utulivu katika kufanya kazi kwa sasa kwa kuwa historia inaonesha kuwa kumekuwa na nia ovu ya baadhi ya wadau kutaka kutibua mambo mazuri yanayofanywa na uongozi wa mpira wa miguu.

“Naomba tuelekeze mafanikio yetu kwa kushirikiana na kuutendea haki mpira wa miguu kwa kushirikiana kwa sababu soka ni furaha na ili kufanikiwa linahitaji juhudi za pamoja,” alisema Malinzi.

Dewji Blog

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Michuzi

SERIKALI YATENGA SHULE 55 , YAUNGA MKONO JITIHADA ZA TFF KUINUA MICHEZO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema kwamba inaunga mkono juhudi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika programu za maendeleo ya vijana, hususani nia yake ya dhati kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan mwaka 2020.
Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omari aliyasema hayo mara baada ya kusikia program za TFF kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Makamu Rais wa Kamati ya...

 

3 months ago

Michuzi

TATU MZUKA YAUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUBORESHA NA KULINDA USAFI WA MAZINGIRA NCHINI

 kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka mwishoni mwa wiki imeadhimisha miaka 56 ya Uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach,Kinondoni jini Dar Es Salaam.Akizungumza wakati wa shughuli hizo za usafi,Mratibu wa mawasiliano kutoka kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka ,Kemi Mutahaba amesema kuwa wameamua kufanya usafi kwa kushirikiana na baadhi ya Wadau kwa kujitolea,lengo...

 

1 year ago

Mwananchi

Serikali yaunga mkono TFF kuifuta Geita

Serikali imeunga mkono uamuzi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), kuifuta Geita Gold Sport, huku ikasema upo mlango wa kukata rufaa nje ya shirikisho hilo.

 

3 months ago

Michuzi

China Yaunga Mkono Juhudi Za Rais Magufuli

Na Mwandishi Maalum, Beijing
China imeahidi kushirikiana na Tanzania kikamilifu katika miradi ya kipaumbele ambayo Serikali ya AwamuyaTano imepanga kuitekeleza ili kufikia azma yake ya uchumi wa viwanda ifikapo 2020 na baadaye uchumi wa Kati ifikapo 2025.
Hayo yalibainishwa leo jijini Beijing na Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming na baadaye kukaririwa tena na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mipango (NDRC), Bw. Ning Jizhe walipofanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Waziri wa...

 

2 years ago

StarTV

CWT Iringa yaunga mkono juhudi za Rais Magufuli kupambana na ubadhirifu

CHAMA cha walimu Tanzania CWT tawi la Iringa kimesema jitihada zinazofanywa na uongozi wa awamu ya tano ya rais Dr.John Pombe Magufuli  zinapaswa kuungwa mkono na watanzania wote wenye fikra pevu na nia njema ya maendeleo ya Taifa.

Zuio la posho kwa watumishi wa serikali, matumizi holela ya fedha za umma pamoja na kutafuta njia mbadala ya namna ya kusherekea siku ya Uhuru na maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani, ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuwa na tija  kwa jamii badala ya manufaa ya...

 

6 months ago

Michuzi

TAHLISO YAUNGA MKONO JUHUDI ZINAZOFANYWA NA JPM KUPIGANIA NA KUZILINDA RASILIMALI ZA NCHI


Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO) limesema linaunga mkono juhudi kubwa zinazoonyeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli kupigania na kuzilinda rasilimali za nchi kwa maslahi ya Taifa jambo ambalo litasaidia kuchangia kwa kasi harakati za kimaendeleo.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Tahliso, Stanslaus Kadugalize katika taarifa yake kwa vyombo vya habari nchini ambapo alisema tokea Serikali ya awamu ya tano iingie madaraka inakaribia kutimiza...

 

1 year ago

Mwananchi

Serikali yaunga mkono Msumbiji

Wakati zaidi ya Watanzania 2,420 wakiwa wamerejeshwa nchini, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kimataifa na Kikanda, Dk Augustine Mahiga amesema wamefukuzwa huko kihalali na wengine ni kutokana na uhalifu nchini humo.

 

4 years ago

Dewji Blog

Serikali yaunga mkono jitihada za wadau wa Michezo

IMG_6504 bacelona

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Juliana Yassoda (Katikati) akiongea na Wanahabari (Hawapo pichani) kuhusu  makocha wa Timu ya Barcelona  kutoka nchini Hispania  ambao wako nchini kwa ajili ya  mafunzo ya makocha yatakayofanyika kwa muda wa siku mbili, wa kwanza kulia ni Balozi wa Spain nchini Mh. Luis Manuel Ceuesta Civis, mafunzo hayo yanatolewa kwa ushirikiano na Kiwanda cha Bia cha Tanzania Breweries.

Na Genofeva...

 

7 months ago

Michuzi

MGOMBEA URAIS TFF FREDRICK MWAKALEBELA AJA NA MAMBO KUMI YA KUINUA SOKA NCHINI


 Mgombea Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela akizungumza na waandihi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa akunadi sera zake.
Na Mwandishiwetu , Dar es Salaam
Mgombea Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela ametaja mambo kumi atakayo fanya katika kuinua mpira hapa nchini kama atapata ridhaa ya kuwa Rais wa TFF.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati uzinduzi wa kampeni yake Mwakalebela amesema kuwa kwa kwanza...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani