Shamim Mwasha na mumewe wafikishwa mahakamani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewapandisha kizimbani Shamim Mwasha na mume wake, Abdul Nsembo kwa tuhuma za kusafrisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70.
Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali, Costantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina, alidai  kuwa Mei Mosi mwaka huu kwa pamoja washtakiwa hao wakiwa meneo ya Mbezi Beach walisafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa gramu 232.70 huku wakijua kufanya hivyo...

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

1 week ago

Malunde

DCEA waeleza walivyomnasa Shamim Mwasha na mumewe akiwa darini kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya

Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema mfanyabiashara Abdul Nsembo maarufu kama Abdukandida ni papa (kinara) katika mtandao wa biashara ya dawa hizo na anajulikana katika nchi mbalimbali zikiwamo Brazil na Marekani.
Nsembo alikamatwa na DCEA Mei Mosi mwaka huu, usiku wa manane akiwa amejificha juu ya dari nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar es Salaam, mpaka sasa anaendelea kushikiliwa na mke wake Shamim Mwasha kwa kudaiwa kukutwa na gramu kati ya 560 hadi 700 za heroin...

 

2 years ago

Malunde

WEMA SEPETU NA WENZAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA DAWA ZA KULEVYA

wema sepetu
Sakata la Madawa ya kulevya limeendelea kugonga vichwa vya habari wiki hii ambapo Jumatatu hii Jeshi la polisi limedai toka lianze operesheni hiyo tayari limewakamata watuhumiwa 112 na kati ya hao 12 wamepandishwa mahakamani Jumatatu hii kwa ajili ya kiapo cha kutorudia matumizi ya Madawa ya kulevya baada ya kukiri kutumia.

Kati ya watu hao 12 ni pamoja na Wema Sepetu, Romy Jones, Petit Man, TID pamoja na wengine.
Aidha Wema Sepetu baada ya kiapo hicho atarudishwa polisi kwa ajili ya...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Shamsa Ford anena mazito kwa mumewe ambaye anapanda Mahakamani leo kwa tuhuma za dawa za kulevya

nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu huzuni,furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa na nk.ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi. Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya.Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati .Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndomaana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo...

 

3 years ago

StarTV

Wakenya saba wafikishwa mahakamani Mara kwa kosa la kufundisha bila kibali:

Askari wa Idara ya Uhamiaji mkoani Mara wamewakamata na kuwafikisha mahakamani raia saba wa Kenya kwa kosa la kuishi nchini na kufanya kazi ya Ualimu bila kibali.

Mwajiri wa walimu hao Charles Nyahula ambaye ni mmiliki wa Shule ya Vic Zone naye amepigwa faini ya Shilingi Milioni moja.

Hata hivyo Mkuu wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Mara Proches Kuoko amesema Idara hiyo inaendelea kuwasaka raia wa kigeni waliopo mkoani humo ambao wamekuwa wakifanya kazi bila vibali vya kuishi nchini.

 Wimbi la...

 

3 years ago

Bongo5

Video: Watanzania 400 wamefungwa nje ya nchi kwa kosa la kusafirisha Madawa ya kulevya

Serikali imesema watanzania 408 wanatumikia vifungo nje ya nchi na wengine kukabiliwa na adhabu ya kifo baada ya kusafirisha dawa za kulevya.
eca86bd9dddf141e387d29

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga alipokuwa akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Akizungumzia Watanzania waliokamatwa kwa dawa hizo Mahiga amesema wanakabiliwa na adhabu hizo katika magereza mbalimbali duniani baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya...

 

4 years ago

Dewji Blog

Shamim Mwasha atoa mada namna kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa kwenye semina ya taasisi ya Manjano

Mkurugenzi Mtendaji 8020 Fashion na  Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation Shamim Mwasha akitoa mada kwenye Semina ya kuwawezesha  wanawake kuwa wajasiriamali kupitia vipodozi vya Luv Touch Manjano iliyoandaliwa na Manjano Foundation kwa lengo la kuwajengea udhubutu wanawake  kufanya biashara pia namna ya kujiwekea akiba na kutumiza malengo yao. Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Ltd. Mkurugenzi wa Manjano Foundation, Mama Shekhar Nasser.

Washiriki wakimsikiliza...

 

3 years ago

Michuzi

WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA.

Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam yawafikisha mahakamani watuhumiwa wawili wanaotuhumiwa kwa uuzaji wa madawa ya kulevya hapa nchini na biashara haramu ya binadamu.
Watuhumiwa hao ni Mohamed Abdalla Omari miaka 37 mfanyabiashara na mkazi wa Tegeta Nyuki jijini Dar es Salaam, anatuhumiwa kwa kusafirisha madawa ya kulevya na usafirishaji haramu wa binadamu anatuhumiwa kwa kumsafirisha Mwinyi Mgobanya na kumweka rehani (Bond) huko Pakistani kisha...

 

3 years ago

Mwananchi

Dereva wa lori aina ya Mitsubish Fusso na utingo wake wamefikishwa mahakamani wakidaiwa kusafirisha kilo 346.58 za dawa za kulevya aina ya mirungi.

Dereva wa lori aina ya Mitsubish Fusso na utingo wake wamefikishwa mahakamani wakidaiwa kusafirisha kilo 346.58 za dawa za kulevya aina ya mirungi.

 

4 weeks ago

Michuzi

Mchungaji kizimbani kwa kusafirisha dawa za kulevya

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
 Mchungaji Henry Ogwany (44),  raia wa Nigeria na wenzake watatu,  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini zenye uzito wa zaidi ya kilogramu 19.

 Mchungaji Ogwanyi, amepandishwa kizimbani pamoja na mshitakiwa mwengine, Onyebuchi Ogbu (34), raia wa Nigeria anayeishi eneo la Msimbazi,  ambao kwa pamoja wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi huku...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani