SIMBA WAJA JUU, WADAI WAMECHOKA KUONEWA NA TFF


Ofisa habari wa Simba  Hajji Manara akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kukaa na kupitia hukumu ya kupokwa alama tatu kwa timu ya Kagera na kupatiwa wao.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Wakati Maamuzi ya kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ikitarajiwa kulipua bomu muda wowote kutoka sasa juu ya hatma ya pointi tatu na mabao matatu waliyopewa Simba kufuatiwa malalamiko yao, Uongozi wa Simba umekuja juu na kuishutumu Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).
Sakata hilo limeendelea kushika hatamu .kutokana na Kamati hiyo kupokea barua ya kukata rufaa kutoka timu ya Kagera kupinga maamuzi ya kamati ya saa 72 kuipoka timu hiyo pointi na kuwapa Simba.
Katika maamuzi ya kamati hiyo iliyokaliwa jana ikiongozwa na Katibu Mkuu wa wa TFF Selestine Mwesigwa na kuita mashahidi akiwemo mchezaji husika Mohamed Fakhi, Mwamuzi wa mezani katika  mchezo huo wa African Lyon dhidi ya Kagera Jonesia Rukyaa, waamuzi wa pembeni pamoja na Meneja wa Kagera Mohamed Husein.
Kufuatia hilo,  Uongozi wa klabu ya Simba umesema hakukuwa na haja ya Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za wachezaji kuitisha kikao kwa ajili ya kujadili marejeo (Review) ya shauri la timu ya Kagera Sugar kwa madai kuwa haina uhalali huo.

Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya Kamati hiyo kukutana jana kwenye Hotel ya Protea kupitia shauri hilo ambapo mpaka sasa bado maamuzi yake hayajatangazwa.
Ofisa habari wa Simba  Hajji Manara ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari  kuwa licha ya kutokuwa sahihi kwa Kamati hiyo kuketi kwakua suala hilo lilitakiwa lipelekwe bodi ya ligi lakini pia kwa mujibu wa sheria za nchi shauri la mrejeo halipaswi kufanyika kwa kuita mashahidi wapya kama ilivyotokea jana.
Manara amesema haijawahi kutokea duniani kote kuwa mtuhumiwa anaitwa kwenye Review au mwamuzi wa nne (Fouth Official) ambaye hata haandiki ripoti anaitwa kutoa ushahidi kwenye kamati jambo ambalo halijawahi kutokea na zaidi ameitaka TFF kutenda haki kwani wamechoka kuonewa. "TFF endapo watashindwa kupata haki yao suala hilo litafika mbali kwa maelezo kuwa tumechoka kuonewa  kwani mara nyingi wamekuwa wakiipendelea Yanga,"
Manara amemshutumu Rais wa TFF Jamal Malinzi kuwa  Wanafahamu kinachoendelea kati yake na mwamuzi Donisia Rukyaa na  wanao ushahidi wa kutosha kuhusu wao.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

4 years ago

Mwananchi

Simba SC yaijia juu TFF

Uongozi wa Simba umelishukia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kulitaka liwarudishie fedha Sh25 milioni ambazo walikatwa kama gharama ya uharibifu wa viti kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Oktoba 31 mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 

4 years ago

BBCSwahili

Wapinzani Ukraine waja juu

Viongozi wa upinzani nchini Ukraine wamedai kufahamishwa ni jambo gani ambalo Rais Viktor Yanukovych, ameipatia Russia.

 

1 year ago

Habarileo

Wazee Yanga waja juu

ZIKIWA zimebaki siku nne kabla ya kufanyika mkutano wa dharura wa wanachama wa Yanga, Kamati ya Muafaka ya Wazee wa klabu hiyo imesema Yanga haiwezi kukodishwa kama masufuria ya kwenda shughulini.

 

3 years ago

Mtanzania

Masheikh waja juu Mahakama ya Kadhi

5Na WAANDISHI WETU
VIONGOZI wa dini ya Kiislamu wamepinga tamko lililotolewa na Jukwaa la Wakristo kuhusu sheria hiyo ya kuanzishwa Mahakama ya Kadhi na kudai kuwa matamko ya aina hiyo yanaweza kusababisha machafuko nchini.
Kauli hiyo zimekuja siku moja baada ya Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) kutoa waraka, likipinga muswada unaopendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni wakati wowote.

Akizungumza na MTANZANIA Imamu wa Msikiti wa Idrisa uliopo Kariakoo, jijini...

 

4 years ago

Tanzania Daima

Mawakili kesi ya Mwale waja juu

MAWAKILI wa utetezi kwenye shauri la utakatishaji fedha linalowakabili washitakiwa wanne akiwemo wakili maarufu, jijini hapa, Median Mwale, wameibua hoja juu ya uhalali wa kutumika kwa sheria ya kuzuia utakatishaji...

 

11 months ago

Mwananchi

Ukawa waja juu ushindi wa CCM

Viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamelalamikia kuchezewa rafu katika uchaguzi mdogo wa ubunge na madiwani baada ya CCM kuibuka na ushindi, wakiachia kata moja tu.

 

3 years ago

Habarileo

Wanazuoni Dodoma waja juu suala la Escrow

UMOJA wa wanazuoni wa Vyuo Vikuu Dodoma umeunga mkono kauli ya jumuiya ya wanazuoni vijana wa Tanzania ya kuponda ripoti ya kamati ya kudumu ya hesabu za serikali (PAC) na wamemwomba Rais Jakaya Kikwete asitekeleze maazimio hayo.

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani