SIMBA YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI MCHEZO NA AL MASRY...MVUA YATIBUA


Klabu ya soka ya Simba imelazimishwa sare nyumbani na timu ya Al Masry ya Misri kwenye mchezo uliomalizika muda mfupi uliopita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo huo ulikuwa na ushindani tangu dakika za mwanzo baada ya Simba kupachika bao la kuongoza dakika ya 9 kupitia kwa John Bocco kwa mkwaju wa Penalti baada ya mlinzi wa Al Masry kuunawa mpira.
Dakika ya 11 Al Masry walisawazisha kupitia kwa Ahmed aliyefunga kwa jitihada binafsi kufuatia walinzi wa Simba kufanya makosa kwenye eneo la hatari. Dakika ya 26 Al Masry waliongeza bao kupitia kwa Abdalrauf aliyefunga kwa penalti baada ya James Kotei kuunawa mpira.
Kipindi cha pili Simba walijitahidi kushambulia ambapo dakika ya 74 mshambuliaji Okwi alifanikiwa kuipangua ngome ya Al Masry kabla ya mlinzi mmoja kuunawa na Simba kupata penalti ambayo ilipigwa na Okwi na kuisawazishia Simba.
Baada ya Okwi kufunga bao la kusawazisha, Mvua kubwa ikanyesha jijini Dar es salaam hali iliyosababisha umeme kukatika na taa kuzimika kwenye uwanja wa taifa hivyo mechi kusimama kwa muda kabla ya hali kuwa shwari na mechi kuendelea, ambapo mechi imeisha kwa sare ya 2-2.

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

MillardAyo

KRC Genk yalazimishwa sare nyumbani, Samatta akitokea benchi

gnkwbe-770x317

KRC Genk wakati wanasubiria kucheza mchezo wao wa mchujo wa mwisho ili kufuzu Europa League hatua ya Makundi, usiku wa August 13 ilicheza mchezo wake wa tatu wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya klabu ya Waasland Beveren katika uwanja wa Luminus Arena. Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu kwa KRC Genk kucheza toka kuanza kwa Ligi […]

The post KRC Genk yalazimishwa sare nyumbani, Samatta akitokea benchi appeared first on millardayo.com.

 

1 year ago

Bongo5

Manchester United yashindwa kutamba nyumbani, yalazimishwa sare na Stoke City

Klabu ya Manchester United imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Stoke City katika mechi ambayo Manchester United iliotawala mchezo kwa kipindi cha mda mrefu.
5472

Baada ya kipa wa Stoke kuokoa mashambulio mengi katika kipindi cha kwanza cha mechi,United ilijiweka kifua mbele baada ya mchezaji wa ziada Anthony Martial kufunga bao la kwanza.

Ilikuwa pigo kubwa kwa Stoke ambayo ilikuwa haijafanya shambulio lolote katika ngome ya United.

Lakini baada ya Jon Walters kupiga krosi, Allen alifika...

 

3 years ago

Dewji Blog

Simba yalazimishwa sare

2+copy

Beki wa Simba, Nassor Chollo, (no 2) akiruka kumdhibiti mshambuliaji wa Polisi Moro, Danny Mrwanda, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na sufianmafoto.com)

Na Mwandishi wetu

TIMU ya Simba, jana ilizidi kuchechemea katika Ligi Kuu Tanzania bara, baada ya kuvuna sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Morogoro katika mechi kali iliyochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Hiyo ni sare ya pili kwa Simba chini ya kocha...

 

3 weeks ago

Malunde

SIMBA YALAZIMISHWA SARE YA 3 - 3 NA STAND UNITED

Baada ya klabu ya soka ya Simba leo kulazimishwa sare ya mabao 3-3 na Stand United, imekuwa ndio mechi ya kwanza kwa mlinda mlango wa klabu hiyo Aishi Manula kuruhusu mabao mengi kwenye mechi moja.
Simba ambayo ilikuwa ikiwakosa nyota wake washambuliaji Emmanuel Okwi na John Bocco wote kwa pamoja kwa mara ya kwanza imeshuhudiwa ikifunga mabao na kusawazishiwa.
Mabao ya Simba yalifungwa na Asante Kwasi, Laudit Mavugo, Nicolas Gyan huku yale ya Stand United yakifungwa na Tariq Seif, Aroon...

 

1 year ago

Habarileo

Man United yalazimishwa sare

MANCHESTER United imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Bornemouth kwenye mchezo mkali wa Ligi Kuu ya England uliofanyika jana.

 

11 months ago

BBCSwahili

Manchester United yalazimishwa sare ya 1-1 na Anderlecht

Manchester United wameshindwa kuondoka na ushindi ugenini dhidi ya Anderlecht baada ya kulazimishwa suluhu ya 1-1 katika hatua ya robo fainali.

 

4 years ago

GPL

ARSENAL YASHIKWA EPL, YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA EVERTON

Mesut Ozil akiifungia Arsenal bao la kuongoza katika dakika ya 80 ya mchezo. Ozil akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao.…

 

1 year ago

MillardAyo

VIDEO: Real Madrid yalazimishwa sare UEFA, Cheki matokeo ya mechi za Nov 2 2016

1q

Usiku wa November 2 2016 hatua ya makundi round ya nne ya michuano ya UEFA Champions League iliendelea kama kawaida kwa michezo nane kuchezwa, Real Madrid wao walikuwa wageni wa Legia Warsaw katika uwanja wa Wojska Polskiego. Real Madrid wakiwa ugenini wamelazimishwa sare ya kufungana magoli 3-3, magoli ya Real Madrid yalifungwa na Gareth Bale […]

The post VIDEO: Real Madrid yalazimishwa sare UEFA, Cheki matokeo ya mechi za Nov 2 2016 appeared first on millardayo.com.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani