SIMBA, YANGA VITANI Z’BAR LEO

yanga-na-simba

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

MACHO na masikio ya mashabiki wa mchezo wa soka, leo yatakuwa katika Uwanja wa Amaan mjini Unguja, kufuatilia pambano la nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baina ya timu kongwe za Simba na Yanga.

Timu hizo zinakutana katika nusu fainali ya pili itakayochezwa majira ya saa 2:15 usiku, baada ya mchezo wa nusu fainali ya kwanza ambayo itazikutanisha Azam FC dhidi ya Taifa  Jang’ombe kupigwa kuanzia majira ya saa 10:15 jioni.

Simba wanaoongoza katika Kundi B kwa kufikisha pointi 10, watakutana na watani wao wa jadi Yanga wanaoshika nafasi ya pili Kundi A, huku Azam ambao ni vinara wa Kundi A wakivaana na Taifa Jang’ombe waliopo nafasi ya pili Kundi B.

Timu hizo zinakutana katika hatua hiyo baada ya Simba kuinyuka Jang’ombe Boys mabao 2-0, wakati Yanga ilijihakikishia kucheza nusu fainali mapema licha ya kuchapwa mabao 4-0 na Azam.

Hii ni mara ya tano kwa timu hizo kongwe kukutana katika ardhi ya Zanzibar zikicheza  michuano tofauti, huku michuano ya Kombe la Mapinduzi ikiwa ni mara ya pili tangu walipokutana mwaka 2011.

Katika mechi nne ambazo timu hizo zimekutana, Simba wameonekana kuwa na historia nzuri ya kushinda mara tatu huku mahasimu wao Yanga wakishinda mara moja.

Hata hivyo, Yanga watavaana na Simba wakiwa wamepania kuendeleza ubabe na rekodi yao ya ushindi kama walivyofanya katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.

Msimu uliopita Yanga walishinda mabao 2-0 dhidi ya Simba katika mzunguko wa kwanza na kufanikiwa kutoa kipigo kingine kama hicho walipokutana kwenye duru ya pili, lakini msimu huu walitoka sare ya bao 1-1.

Akizungumzia mchezo wa leo, Kocha mkuu wa Simba, Mcameroon Joseph Omog, alisema anafahamu ugumu wa mechi hiyo kwani mara nyingi timu hizo zinapokutana zinakuwa zimejiandaa vizuri na kukamiana, huku akisisitiza kuwa matarajio yao ni kutinga hatua ya fainali.

“Nashukuru tumefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali, lakini tutapambana kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi ili kupata pointi tatu muhimu licha ya mchezo huo kuwa wa ushindani mkubwa,” alisema Omog.

Naye kocha mkuu wa Yanga, Mzambia George Lwandamina, alisema kwenye soka lolote linaweza kutokea, hivyo wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo wa leo na kutinga hatua ya fainali baada ya kuyafanyia kazi makosa yaliyosababisha wafungwe na Azam mabao 4-0.

Kipigo cha Yanga katika mchezo dhidi ya Azam kilisababishwa na washambuliaji wake kukosa umakini katika ufungaji pamoja na udhaifu wa safu ya ulinzi ambayo haikuwa imara.

Kwa upande wake kocha msaidizi wa Azam, Iddy Cheche, alisema malengo yao ni kutwaa Kombe la Mapinduzi mwaka huu licha ya kukabiliwa na mchezo mgumu watakapoivaa Taifa Jang’ombe.

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Habarileo

Simba,Yanga vitani leo

TIMU za Simba na Yanga leo zinashuka dimbani kwa nyakati tofauti kucheza nusu fainali za michuano ya Kombe la Mapinduzi. Simba ambao ndio mabingwa watetezi wa taji hilo, iliyokuwa katika Kundi B itakwaana na timu ngumu ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza kwenye Uwanja wa Amaan hapa.

 

3 years ago

Mwananchi

LIGI KUU BARA: Kumekucha Simba, Yanga, Azam vitani leo

>Miamba ya soka nchini, Yanga na Simba baada ya kushindwa kutambiana wiki iliyopita leo itasaka ushindi wa ugenini dhidi ya Stand United na Prisons huku mabingwa watetezi Azam wakiwa nyumbani kuwavaa JKT Ruvu.

 

2 years ago

Habarileo

Yanga, Simba vitani

VIGOGO vya soka Tanzania Bara, Yanga na Simba leo vinashuka kwenye viwanja tofauti kusaka pointi tatu muhimu katika mechi za duru la pili la Ligi Kuu.

 

2 years ago

Habarileo

Azam, Yanga, Simba vitani

LEO ni vita ya namba. Baada ya mapumziko ya mwezi mmoja michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea kutimua vumbi katika viwanja sita tofauti, huku Simba, Azam FC na Yanga kila moja ikiingia katika vita ya namba kusaka pointi tatu muhimu.

 

3 years ago

Mtanzania

Yanga, Azam, Simba vitani

Pg 32 Okt 17NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

LIGI Kuu ya Tanzania Bara inaendelea leo kwa mechi sita katika viwanja tofauti huku Yanga ikiikaribisha Azam FC katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga, Azam na Simba zitakuwa zikicheza kusaka ushindi katika mechi zao ili zijiweke katika nafasi nzuri katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga ina pointi 15 sawa na Azam lakini inaongoza kwa kupachika mabao 13 huku Azam ikiwa na mabao 9, hivyo kila moja itakuwa ikisaka ushindi ili kuongoza...

 

2 years ago

MwanaHALISI

Wabunge wa Simba na Yanga vitani

WABUNGE wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni mashabiki wa klabu za Simba na Yanga, wanatarajia kucheza mchezo maalum wa mpira wa miguu wenye lengo la kukusanya fedha zitakazosaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, anaandika Aisha Amran. Mchezo huo utakaochezwa siku ya Jumapili ya wiki hii, tarehe 25 Septemba ...

 

2 years ago

Mwananchi

NUSU FAINALI CHALENJI: Yanga, Simba vitani Ethiopia

Licha ya Tanzania kutolewa katika mashindano  ya Chalenji yanayoingia nusu fainali leo, bado macho na masikio ya mashabiki wa soka nchini yatakuwa  kwa nyota wa Yanga, Simba na Azam wanaoziwakilisha Rwanda, Uganda.

 

2 years ago

Habarileo

Yanga, Azam vitani leo

YANGA na Azam leo zinashuka kwenye viwanja tofauti katika michezo ya Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali.

 

2 years ago

Habarileo

Yanga vitani Angola leo

LEO ni fursa nzuri kwa Yanga kung’ara kimataifa wakati itakapokuwa mjini Dundo, Angola katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC) dhidi ya Sagrada, Esperanca ya huko.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani