Spika: Lijualikali bado mbunge

Mbunge Lijualikali (katikati) akiwa katika purukushani na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi.

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amesema mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali, anaendelea na wadhifa wake huo baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kufanya fujo.

Akizungumza na RAIA Mwema, Ndugai alisema kwa mujibu wa Katiba, Mbunge atakoma kuwa mbunge endapo atafungwa jela kwa muda wa zaidi ya miezi sita.

“ Ukisoma Katiba ya Tanzania Ibara ya 70 na 71, zikisomwa kwa...

Raia Mwema

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Michuzi

Mbunge Wa jimbo la Kilombero Mhe. Peter Lijualikali kuendelea kuwa mbunge licha ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela - Kailima


Mjadala umeshika kasi mitaani, mitandaoni na kila mahali baada ya Mahakama ya wilaya ya Kilombero kumhukumu kutumikia kifungo cha miezi sita jela bila faini Mbunge Wa jimbo la Kilombero Mhe. Peter Lijualikali (30) kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Mbunge huyo, akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na mwenzie Stephano Mgata (35) walitenda kosa hilo Machi 1, 2016 saa 4 asubuhi Kwenye kikao cha Baraza la Madiwani katika...

 

9 months ago

Malunde

MBUNGE LIJUALIKALI AKAMATWA NA POLISI

Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali na viongozi watatu wa Chadema wilayani Malinyi wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya kusanyiko lisilo halali.

Mbunge huyo amekamatwa jana Alhamisi saa 12:40 jioni akitoka kwenye kikao cha ndani cha chama hicho kilichofanyika katika Kijiji cha Makerere wilayani Malinyi.

Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Alfonce Mbassa alisema baada ya kumaliza kikao, mbunge huyo na viongozi wengine walipanda kwenye...

 

1 year ago

Dewji Blog

Mahakama yamwachia mbunge wa Kilombero, Lijualikali

Mahakama Kuu ya Dar es Salaam imetengua hukumu aliyopewa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali ambaye alihukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani.

Uamuzi wa mahakama umekuja baada ya kukuta Lijualikali hana kosa na hivyo kutengua hukumu iliyotolewa katika mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Kilombero, Morogoro.

Lijualikali awali alihukumiwa kifungo cha miezi sita baada ya kukutwa na kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki huku aliyekuwa dereva wake, Stephano Mgatta akihukumiwa...

 

1 year ago

Bongo5

Chadema kukata rufaa hukumu ya Mbunge Lijualikali

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakikubaliani na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero dhidi ya Mbunge, Peter Lijualikali na kwamba imepanga kukataa rufaa katika Mahakama Kuu.

Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi hii katika Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema Lijualikali ni mfungwa wa kisiasa na amefungwa kwa sababu ya vita ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Upinzani.

Lissu alisema,...

 

1 year ago

MillardAyo

Gereza aliko mbunge Peter Lijualikali labainishwa

Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com. Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo ni pamoja na hii ya kwenye gazeti la Nipashe, yenye kichwa cha habari ‘Gereza aliko […]

The post Gereza aliko mbunge Peter Lijualikali labainishwa appeared first on millardayo.com.

 

9 months ago

CHADEMA Blog

Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali akamatwa na Polisi

Polisi wamemkamata mbunge wa jimbo la Kilombero, Mh. Peter Lijualikali, jioni ya leo, alhamis, 28/09/2017, baada ya kumaliza kikao cha ndani cha chama mjini Malinyi Ulanga.

 

6 months ago

Malunde

MBUNGE WA CHADEMA LIJUALIKALI AKAMATWA TENA NA POLISIMbunge wa jimbo la Kilombero kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Peter Lijualikali amekamatwa na maofisa wa polisi muda mfupi baada ya kuahirishwa kwa kesi yake yenye mashtaka nane likiwemo la kuchoma moto ofisi ya kijiji.

Lijualikali amekamatwa ndani ya mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro na maofisa hao na kupelekwa katika kituo cha polisi mkoa wa Morogoro kwa kile kilichodaiwa na maofisa hao kuwa wanataka kumhoji zaidi.

Wakati Mbunge huyo akikamatwa alionekana kupigwa...

 

6 months ago

CHADEMA Blog

MBUNGE LIJUALIKALI AKAMATWA NDANI YA MAHAKAMA MOROGORO

By Hamida Shariff, Mwananchi hshariff@mwananchi.co.tz Mbunge wa jimbo la Kilombero kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Peter Lijualikali amekamatwa na maofisa wa polisi muda mfupi baada ya kuahirishwa kwa kesi yake yenye mashtaka nane likiwemo la kuchoma moto ofisi ya kijiji. Lijualikali amekamatwa ndani ya mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro na maofisa hao na kupelekwa

 

1 year ago

Mwananchi

Mbunge Lijualikali, dereva wake jela miezi sita

Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali na Dereva wake, John Kibasa wamehukumiwa kwenda jela miezi sita bila faini kwa kosa la kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi mwaka 2015.

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani