Standard Chartered wazindua michuano ya kuwania tiketi ya kwenda kuiona Liverpool

Na Mwandishi wetu
Benki ya Standard Chartered jana ilizindua awamu ya tatu  ya michuano ya soka ya kuwania kombe lake. Michuano hiyo ya kuwania kombe la Standard Chartered 2018 huchezwa kwa dakika 10 kila upande ukicheza kwa dakika 5. Michunao hiyo inasaka timu itakayoenda kushuhudia kipute kinachopigwa na timu ya Liverpoool. Hii ni mara ya tatu kwa michuano hiyo ya kusisimua kufanyika katika ardhi ya Tanzania kuanzia mwaka 2010.

The Standard Chartered Group ndio wadhamini wakubwa wa Liverpool Football Club kuanzia mwaka 2010 hadi  2018/2019. Kwa kushirikiana na klabu hiyo benki ya Standard huendesha mashindano ya soka ya dakika 10 katika masoko yake makubwa ya Bara la Asia, Afrika na Mashariki ya kati. 

Pia michuano hiyo inawezesha kuchangia katika kuendeleza soka. Ikiwa katika mwaka wake wa saba tangu kuanzishwa kwake katika masoko hayo, mashindano hayo yameendelea kuwa na nguvu zaidi kukiwa na washindi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia.

Kenya ilitwaa ushindi mwaka 2016, Korea kusini (2015), Vietnam (2014), Thailand (2013) na Singapore (2012). Michuano hiyo kwa kaiwada ina sehemu tatu kuanzia nchi wenyeji, kikanda na fainali zake hufanyika viwanda vya Anfield – Uingereza. Mwaka huu benki hiyo imebadili mfumo wa michuano na kwamba mshindi atapata tuzo na kwenda Anfield.

Akizungumza wakati wa uzinduzi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank nchini Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, alisema kwamba mwaka huu kutakuwa tofauti na kwamba mshindi wa mashindano ya ndani yenye timu 32 atatwaa kombe na  kwenda kuangalia mtanange wa ligi kuu ya England.

Timu zitakazoshiriki ni pamoja na wateja wa benki hiyo na michuano hiyo itaanza Juni 23 mwaka huu. Mwaka jana mashindano hayo yalikuwa ya kikanda ambapo timu kutoka Tanzania, Kenya na Uganda zilichuana vikali na timu ya Tanzania ya Azania – Mikoani Traders  walishinda na kwenda kwenye fainali Anfield.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba akitoa utambulisho kwa meza kuu wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia kwenda kushoto ni Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa Kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu, Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo, Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani ( wa pili kushoto) akizungumzia ziara ya nyota na nahodha wa zamani wa Liverpool, Sami Hyypia anayetarajiwa kutua nchini Juni 20 wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu akielezea kuhusu safari yao ya Anfield ambapo aliongeza na kusema amefurahishwa na msimu huu ambapo mashindano hayo hayashirikisha timu za nchi jirani wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo akizungumzia  ujio wa Hyypia ambapo alisema ni nafasi adhimu kwa timu yake kunolewa na nahodha huyo wakati wakijiandaa na mashindano ya mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana, katika mkutano na waandishi wa habari kwenye hafla fupi iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) ya uzinduzi wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (kulia) akitoa salamu za TFF ambapo aliipongeza benki ya Standard Chartered nchini kwa kuinua soka la Tanzania kimataifa kupitia mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa mashinano hayo zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba.Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (wa kwanza kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani ( kushoto) wakizundua sanamu ya nyota na nahodha wa Liverpool, Sami Hyypia anayetarajiwa kutua nchini Juni 20 wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba ( wa kwanza kulia), Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu (wa pili kushoto) pamoja na Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo (wa tatu kulia).Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (wa kwanza kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani ( kushoto), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (wa kwanza kulia), Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu (wa pili kushoto) pamoja na Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo (wa tatu kulia) wakipata picha ya ukumbusho baada ya kuzindua sanamu ya nyota na nahodha wa Liverpool, Sami Hyypia anayetarajiwa kutua nchini Juni 20 wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Sehemu ya waandishi wa habari na wadau wa michezo waliohudhuria wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Michuzi

Benki ya Standard Chartered yazindua “Kombe la Standard Chartered Trophy — Njia kwenda Anfield 2015

Viongozi wa vitengo mbalimbali wa Benki ya Standard Chartered wakipigiga mpira kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa shindano la soka la “Kombe la Standard Chartered – Njia Kwenda Anfield” katika ofisi za Benki hiyo mapema leo. Kutoka kushoto kwenda kulia ni: Femi Alonge - Mkuu wa kitengo cha Wateja wa Makampuni Makubwa, Juanita Mramba – Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko, Mike Shio – Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Ruth Zaipuna – Mkuu wa Kitengo cha...

 

1 year ago

Michuzi

JOHN BARNES WA LIVERPOOL KUTUA NCHINI KUANGALIA KOMBE LA STANDARD CHARTERED  Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah (kulia) ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool akitoa uchambuzi wa timu hiyo kwenye barabara ya kuelekea Anfield wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba akizungumzia tukio adhimu la Benki ya Standard Chartered, Tanzania...

 

2 years ago

Michuzi

1 year ago

Mwananchi

Standard Chartered kuibeba Serengeti Boys

Serikali imeiomba Benki ya Standard Chartered kutia mkono wake kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' ambayo itashiriki fainali za Afrika kwa vijana wenyw umri huo zitakazofanyika Gabon mwaka huu.

 

2 years ago

Mwananchi

Standard Chartered yapata mkurugenzi mpya Mtanzania

Benki ya Standard Chartered Tanzania, imepata Mkurugenzi Mtendaji mpya ambaye ni Mtanzania, Sanjay Rughani.

 

3 years ago

Dewji Blog

Standard Chartered’s global network comes together to support the #GlobalGoals

standard chartered

The Bank is promoting the #GlobalGoals to clients and staff

Standard Chartered Bank has launched an extensive multi-channel communications to its 86,000 employees and millions of clients to spread the word about the Global Goals for Sustainable Development. The Bank is proud to be one of the Founding Partners of Project Everyone, which aims to raise awareness of the Goals, reaching seven billion people in seven days. This burst of activity is designed to highlight the Goals during this...

 

4 years ago

Michuzi

IPTL wins case against Standard Chartered Bank

THE High Court of Tanzania has temporarily restrained Standard Chartered Bank (Hong Kong) Limited and two other respondents from enforcing a decision issued by the International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID) over recalculation of power tariffs.
High Court Judge Fauz Twaib issued the interim order in favour of two applicants, Independent Power Tanzania Limited (IPTL) and Pan African Power Solution Limited (PAP) after considering lengthy and exhaustive submissions...

 

4 years ago

Michuzi

Standard Chartered Bank rewarding its Clients for Referrals:

 Standard Chartered Bank Tanzania Limited has launched an exciting campaign for its Priority Clients. Dubbed “Member get Member” campaign, the initiative is open to the Bank’s Priority Clients. Exciting prizes including trips to Rome, Paris, Cape Town, Johannesburg or Dubai, among others, await the Bank’s Clients who successfully refer new Priority Clients to the Bank. The new clients will also qualify to join the campaign which is ongoing until 31st July, 2014.  Standard Chartered Bank...

 

4 years ago

Michuzi

Standard Chartered Bank launches the Bundle Campaign

 Standard Chartered Bank’s Head of Retail Clients, Mike Shio, right, spins the wheel to pick the winner of the Bank’s Salary Solution Campaign raffle. Looking on are an official from the Gaming Board of Tanzania, Mrisho Milao, centre, and the Bank’s Head of Products, Omari Mtiga.  Standard Chartered Bank’s Head of Retail Clients, Mike Shio, right, spins the wheel to pick the winner of the Bank’s Salary Solution Campaign raffle. Looking on are an official from the Gaming Board of...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani