TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LEO TAREHE 11.02.2017: • KIJANA MMOJA WAKIUME ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA AKIMWINGILIA KIMWILI MBUZI WILAYANI NYAMAGANA.

KWAMBA TAREHE 08.02.2017 MAJIRA YA SAA 09:00HRS ASUBUHI, KATIKA MTAA WA MABATINI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA ALIYEJULIAKANA KWA JINA LA JUMANNE NASSIBU MIAKA 20, MGOGO NA MKAZI WA MTAA WA MABATINI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA AKIMWINGILIA KIMWILI MBUZI JIKE, KITENDO AMBACHO NIKOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA TAREHE TAJWA HAPO JUU MAJIRA YA 6:00HRS ASUBUHI  MMILIKI WA MBUZI  AITWAYE BENEDICTOR BUNGA MIAKA 33, MKAZI WA MTAA WA MABATINI, ALIKWENDA KUWAFUNGA MALISHONI MBUZI WAKE SITA KWA KUTUMIA KAMBA. AIDHA INASEMEKANA KUWA ILIPOFIKA MAJIRA YA SAA TATU ASUBUHI (9:00HRS), MMILIKI WA MBUZI ALIKWENDA KUWACHEKI MBUZI WAKE ENEO ALIPOKUWA AMEWAFUNGA MALISHONI NA KUWAKUTA MBUZI WATANO BADALA YA SITA.

KUTOKANA NA KUKOSEKANA KWA MBUZI HUYO MMILIKI WA MBUZI HAO ALIPATWA NA HOFU HUKU AKIJUA MBUZI WAKE MMOJA AMBAYE HAMUONI ATAKUWA AMEIBIWA NDIPO ALIANZA KUTAFUTA VICHAKANI, GHAFLA  ALINADAI ALIMUONA MTUHUMIWA JUMANNE  NASSIBU VICHAKANI AKIWA ANAMWINGILIA KIMWILI MBUZI WAKE. INASEMEKANA KUWA MMILIKI WA MBUZI HUYO BAADA YA KUONA TUKIO HILO ALIPIGA YOWE AKIOMBA MSAADA NDIPO WANANCHI WALIFIKA NA KUMSAIDI KUMKAMATA MTUHUMIWA.

MTUHUMIWA YUPO POLISI HUKU MAHOJIANO DHIDI YA TUHUMA ZINAZOMKABILI YAKIENDELEA, PIA UTARATIBU UNAFANYIKA WA  KUPELEKWA MTUHUMIWA HOSPITALI,  ILI KUANGALIWA KAMA ANAAKILI TIMAMU,  PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA DHIDI YAKE.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WAJIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUTOA TAARIFA POLISI ZA WATU WENYE TABIA KAMA HIZO KWANI NI KOSA LA JINAI, ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAO.


IMETOLEWA NA.

DCP: AHMED MSANGI


KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Michuzi

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LEO TAREHE 3.12.2016

DCP AHMED MSANGI KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
  KUPATIKANA KWA SILAHA MBILI AINA YA AK 47, BASTOLA 1, BOMU LA KUTUPA KWA MKONO 1, NA VISU NA JAMBIA NA KUUAWA KWA WATU WAWILI WAZANIWAO KUWA NI MAJAMBAZI.


Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

 

3 years ago

Michuzi

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 18.08.2015. KUFANYA KAZI YA ULINZI NA USALAMA ILIYOKASIMIWA KWA JESHI LA POLISI.

MNAMO TAREHE 14.08.2015 MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHADEMA ALIKUJA MKOA WA MBEYA AKIWA AMEANDAMANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA CUF, NCCR – Mageuzi NA NLD KWA DHUMUNI LA KUMTAMBULISHA NA KUOMBA UDHAMINI WA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA KWA NAFASI YA URAIS.


KATIKA MSAFARA WAKE KUTOKA UWANJA WA NDEGE [SONGWE] KULIONEKANA GARI MOJA (PICHANI) AINA YA LAND CRUISER – PICK UP YENYE RANGI NYEUSI NA NDANI YAKE LILIKUWA LIMEBEBA VIJANA AMBAO WALIKUWA WAMEVAA MAVAZI MEUSI, KOFIA – BERETI NYEUSI NA MIWANI...

 

4 years ago

Michuzi

MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA KUSABABISHA AJALI NA KIFO

Na Sylvester Onesmo  wa Jeshi la Polisi Dodoma.   Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Jackson s/o Venance, umri miaka 33, kabila Mhaya, mfanyakazi wa NSSF Bukoba aliyekuwa akitembea kwa miguu pembeni mwa barabara ya Nyerere maeneo ya TRA Dodoma katika Manispaa na Mkoa wa Dodoma amefariki dunia alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T.399 CWG aina ya NISSAN iliyokuwa ikiendeshwa na Dotto d/o Onesmo, umri miaka 25, kabila...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani