TAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) YAPIMA MOYO WA MTOTO ALIYE TUMBONI MWA MAMA YAKE

Na Veronica Romwald, Dar es SalaamTAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mara nyingine tena imefanya upimaji wa moyo wa mtoto aliye tumboni mwa mama yake, kuchunguza magonjwa mbalimbali ya moyo.Upimaji huo umefanywa katika taasisi hiyo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Watoto wa JKCI, Naiz Majani.Akizungumza na waandishi wa habari, Dk. Naiz amesema kuna faida lukuki iwapo mjamzito ataamua kufanya kipimo maalumu."Tunatumia Ultra sound kama kawaida kufanya kipimo hiki, lakini inakuwa ina tofauti kidogo... hatutumii mionzi yoyote, hivyo hakuna madhara anayoweza kuyapata mama au mtoto wake aliye tumboni," amesema. 
Ametaja faida hizo kuwa ni kupunguza idadi ya vifo vya watoto wanaozaliwa na magonjwa ya moyo, na kuwaondoa kwenye masumbufu wanayoweza kuyapata kutokana na kuchelewa kupata matibabu."Kwa mara ya  kwanza tuliwafanyia kipimo hicho wajawazito 25 mwishoni mwa mwaka jana ambapo watano kati yao mimba zao zilikutwa na matatizo.
 Dk. Naiz akionesha jinsi wanavyofanya upimaji kuchunguza magonjwa ya moyo wa mtoto aliyeko tumboni. 
Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi (pichani) akielezea dhumuni  la kuanzisha huduma hiyo ili kugundua matatizo mapema.Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

1 week ago

Michuzi

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YATOA HUDUMA YA UPIMAJI WA MOYO KWA MTOTO ALIYEPO TUMBONI KWA MAMA YAKE (FETAL ECHO)

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi akiongea na waandishi wa habari kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ikiwemo upimaji wa kina mama wajawazito moyo wa mtoto aliyepo tumboni (Fetal ECHO) ili kuangalia kama una magonjwa au la. Kutolewa kwa huduma hiyo kutasaidia kufahamu afya ya mtoto aliyepo tumboni ikiwa ni pamoja na hali ya moyo. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani...

 

4 months ago

Michuzi

Binti aliyefanyiwa upasuaji wa moyo na kuwekea Valve asherehekea siku yake ya kuzaliwa na Wagonjwa wa Moyo waliolazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea zawadi za pampers ambazo zitatumika kwa watoto waliolazwa kutoka kwa Mary Mabano ambaye mwaka 2008 alifanyiwa upasuaji na madaktari wa Taasisi hiyo na kuwekewa Valve moja ambayo inamsaidia kupitisha damu vizuri baada ya upasuaji huo amepona na amejaliwa kupata mtoto mmoja. Siku ya jana tarehe 28/12/2016 Mary alikuwa anatimiza umri wa miaka 23 na aliamua kusherehekea siku hiyo na wagonjwa wa moyo.

 

5 months ago

Michuzi

Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) na taasisi ya Open Heart International OHI waendelea na upasuaji wa moyo


Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari wenzao wa Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo kwa njia ya kufungua kifua na kuziba tundu la moyo. Kulia ni Dkt. Bingwa wa Upasuaji Hussein Hassan akifuatiwa na madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Dk. Godwin Godfrey (kushoto) na Dkt. Benjamin Bierbach.
Madaktari bingwa wa moyo pamoja na wauguzi kutoka...

 

1 year ago

Michuzi

TAASISI YA UPASUJI MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI), KUENDESHA KAMBI YA UPASUAJI MOYO KUANZIA LEO JUMATATU APRILI 25

Taasisi ya Upasuaji Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) itaendesha kambi maalumu mbili za upasuaji moyo kwa kushirikiana na watalaam kutoka nje.
Kambi ya Kwanza: Itaanza leo Aprili 25 hadi 30, 2016. Na kufanya upasuaji wa wagonjwa 25 hadi 30. Kambi hii itashirikisha wataalam toka Australia kupitia Open Heart International.
Kambi ya Pili Itaanza Aprili 30 hadi Mei 7 ambayo itafanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 70. Kambi hii inashirikisha wataalam kutoka Saudi Arabia na London kupitia Al-Muntada...

 

3 months ago

Michuzi

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA APOLO, BANGALOLE YA NCHINI INDIA WAWAFANYIA WAGONJWA UPASUAJI WA MOYO

 Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Madaktari  wa Hospitali ya Apolo, Bangalole ya nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kumuwekea  milango miwili ya moyo ya chuma (Aortic na Mitral Valuves) ambayo itamsaidia kupitisha damu vizuri katika moyo. Kutoka kulia ni Dkt. Sathyaki Nambala, akifuatiwa na Dkt. Bashir Nyangasa  na kushoto ni Dkt. Lebighe Khan.Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete...

 

1 month ago

Michuzi

Kiongozi Mkuu wa Madhebu ya Bohora Duniani akamilisha ahadi ya kuleta madaktari wa Moyo nchini katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Saifee ya nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo . Katika ziara aliyoifanya nchini mwishoni mwaka jana kiongozi Mkuu wa Madheebu ya Bohora Duniani Mtakatifu Dkt. Syedna Aliqadr Mufaddal Saifuddin alimuahidi Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuleta madaktari wa Moyo nchini ambao watashirikiana na Madaktari wa JKCI kufanya upasuaji kwa...

 

8 months ago

Michuzi

TAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete yafanya upasuaji mkubwa wa moyo kuweka betri kwa mara kwanza


TAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es salaam leo imefanya upasuaji mkubwa na  kuweka betri katika moyo wa mtu wa makamo kwa mafanikio. Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Profesa Mohamed Janabi ameiambia Globu ya Jamii jioni hii kwamba ana furaha kwa kufanikiwa kwa upasuaji huo ambao  amesema umefanyika  mara ya kwanza  kufanyiwa  mtu wa makamo nchini Tanzania.“Tumeweka kifaa hicho ambacho kitaalamu kinajulikana kama Pacemaker CRTD kwa mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 68...

 

2 months ago

Michuzi

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA HOSPITALI YA BLK YA NCHINI INDIA WATOA HUDUMA YA MATIBABU YA MOYO BILA YA KUFUNGUA KIFUA KWA WAGONJWA 16

Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India wakimwekea mgonjwa kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa jina la kitaalam Pacemaker . JKCI kwa kushirikiana na BLK hospital kwa kutumia mtambo wa Cath Lab wamewafanyia wagonjwa 16 huduma mbalimbali za matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization).Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete...

 

12 months ago

Michuzi

UINGEREZA YAIFAGILIA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, JKCI

Kaimu Muuguzi Mkuu wa taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Flora Kasembe, (wapili kulia), akitoa maelezo ya namna wanavyohudumia wagonjwa waliolazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi cha JKCI, wakati Naibu Balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, (wapili kushoto), alipotembelea kambi ya upasuaji wa moyo iliyoendeshwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na taasisi ya hiari ya Uinegereza ya Muntada Aid, Mei 3, 2016. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa ...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani