Taifa Jang’ombe ndio timu pekee iliyotetemesha nyavu za Simba Mapinduzi Cup

Mpaka timu ya Simba inatinga fainali katika Mashindano ya Mapinduzi CUP baada ya kuitoa Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-2 kufuatia sare ya 0-0 dakika 90, timu hiyo imeruhusu lango lake kufungwa bao moja tu bao ambalo walijifunga wenyewe na beki wao Novaty Lufungo akiwa katika harakati za kuokowa mpira langoni kwao ilikuwa ni dakika ya 76 mchezo wa makundi kati ya Simba na Taifa ya Jang’ombe ambapo Simba alifanikiwa kushinda mabao 2-1 katika mchezo huo.

Baada ya hapo Simba hajafungwa tena mpaka sasa anasubiri Fainali dhidi ya Azam FC ambayo itapigwa siku ya Ijumaa January 13, 2017 majira ya Saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Amaan.

Mchezo wa pili Simba aliifunga KVZ bao 1-0, kisha akatoka sare ya 0-0 na URA na mchezo wa mwisho wa makundi akawafunga Jang’ombe Boys mabao 2-0 huku mcchezo wao wa nusu fainali walishinda kwa penalti 4-2 baada ya dakika 90 kwenda sare ya 0-0.

Simba wanaenda kucheza fainali na timu ngumu Azam ambayo wao hawajaruhusu lango lao kuguswa hata mara moja katika michezo yote waliocheza.

Azam walianza mchezo wao wa kwanza kwa kuifunga Zimamoto ya Visiwani Zanzibar bao 1-0, wakatoka sare tasa (0-0) na Jamhuri ya Pemba kisha kuifuga Yanga kipigo takatifu cha mabao 4-0, hivyo imecheza michezo yote hiyo bila ya lango lao linaloongozwa na Aishi Manula kuguswa.

Fainali hiyo itakuwa ngumu sana kwani katika historia Azam hajawahi kupoteza fainali ambapo aliwahi kucheza mara mbili mfululizo mwaka 2012 na 2013 na zote kufanikiwa kutwaa Ubingwa baada ya kuzifunga timu ya Jamhuri na timu ya Tusker ya Kenya, hivyo ana historia nzuri ya kutopoteza michezo ya fainali katika Kombe hilo.

Kwa upande wao Simba ndio timu inayoongoza kubeba kombe hilo mara nyingi (3) ambapo ilifanikiwa kuchukua mwaka 2008 mbele ya Mtibwa, wakachukua tena mwaka 2011 mbele ya Yanga na mwaka 2015 mbele ya Mtibwa hivyo ikifanikiwa kuchukua na mwaka huu itakuwa ni mara ya nne wakati Azam wao wakifanikiwa kutwaa kombe hilo itakuwa mara ya tatu sawa sawa na Simba na hapo ndipo panapokuja ugumu wa fainali hiyo huku Simba akitaka kuzidi kuweka rikodi ya kubeba mara nyingi wakati Azam wanataka kuwafikia Simba kwa kubeba taji hilo kwa mara ya tatu.

The post Taifa Jang’ombe ndio timu pekee iliyotetemesha nyavu za Simba Mapinduzi Cup appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Zanzibar 24

Leo ndio leo: Taifa Jang’ombe, Jang’ombe Boys hapatoshi Mapinduzi Cup

Pazia la Mashindano ya Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake leo Disemba 30, 2016 katika uwanja wa Amaan saa 2:15 Usiku ambapo kutakuwa na mchezo wa Derby ya Jang’ombe kati ya Taifa ya Jang’ombe na Jang’ombe boys ambapo mashindano ya msimu huu yameshirikisha vilabu 9, vitano vikitokea Zanzibar, vitatu Tanzania bara na kimoja kutoka Uganda ambao ndio mabingwa watetezi timu ya URA.

 

KUNDI A :Simba, URA, KVZ, Taifa ya Jang’ombe na Jang’ombe Boys.

 

KUNDI B :Yanga, Azam,...

 

1 year ago

MillardAyo

Ushindi wa Jang’ombe Boys unaoweka rekodi Mapinduzi Cup 2017

screen-shot-2017-01-05-at-7-08-04-pm

Michuano ya Kombe la Mapinduzi imeendelea tena leo kwa mchezo wa Kundi A kuchezwa saa 10:15 jioni, kabla ya saa 20:15 kuchezwa mchezo wa pili wa Kombe la Mapinduzi kati ya URA dhidi ya Simba, mchezo wa kwanza wa Kundi A leo ulikuwa ni kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya KVZ. Mchezo wa Jang’ombe Boys […]

The post Ushindi wa Jang’ombe Boys unaoweka rekodi Mapinduzi Cup 2017 appeared first on millardayo.com.

 

1 year ago

Zanzibar 24

Mjue mchezaji aliyefunga magoli mengi mechi za Jang’ombe Boys dhidi ya Taifa ya Jang’ombe.

Jina lake ni Khamis Mussa “Rais” ambae hadi leo bado rekodi yake haijavunjwa na mchezaji yoyote kwenye mechi ya Dabi ya Jang’ombe kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya Taifa ya Jang’ombe.

Ni Striker hatari wa Jang’ombe Boys, huyu jamaa ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi zilipokutana timu hizo.

Ameshafunga mabao mawili mpaka sasa na hakuna mwengine yeyote alifika mabao hayo.

Rais amefunga mabao hayo katika mchezo mmoja wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja ambapo...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Derby Taifa ya jang’ombe na jang’ombe boys kunogesha tamasha la fiesta

Tamasha la Fiesta 2016 Zanzibar litatanguliwa na mchezo maalum kwa kuwakutanisha Derby ya jang’ombe kati ya Taifa ya jang’ombe na jang’ombe Boys mchezo ambao utasukumwa Jumamosi tarehe 19/11/2016 saa 2:00 usiku katika Uwanja wa Amaan.

Mchezo huo ni maalum kwa kumtafuta nani mbabe wa jang’ombe ni Taifa au Boys ambapo wataoneshana siku hiyo kabla ya kukutana kwenye mchezo wao wa awali  ligi kuu soka Visiwani Zanzibar ambao utachezwa tarehe 10/12/2016.

Maandalizi yanaendelea vizuri kwani...

 

2 years ago

Zanzibar 24

KVZ yaendelea kugawa pointi kwa timu za Jang’ombe: Ubaoni KVZ 0- 1 Jang’ombe Boys

Maafande wa Valantia KVZ jana usiku katika mchezo wa ligi kuu Zanzibar kanda ya Unguja uliopigwa uwanja wa amaan majira ya usiku iliendelea kugawa pointi kwa watoto wa Jang’ombe mara hii ikiwa kwa Jang’ombe Boys. Goli la boys lilifungwa na Chinga dakika ya 86.

Ushindi huo wa goli 1-0 ulioupata Boys unaipa pointi tatu muhimu katika mbio za ligi kuu kanda ya Zanzibar ambapo hadi sasa ipo raundi ya 10 lakini nne bora haitabiriki. Boys wanafikisha pointi 17 sambamba na maafande wa polisi .

 

The...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Mshabiki namba 1 wa Taifa Jang’ombe asisitiza timu za vikosi zote watazipiga

Baada ya jana Timu ya Taifa ya jang’ombe kuwachapa Maafande wa Mafunzo kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja, mshabiki wao mkuu Salum Rajab “Mutu” amesisitiza msimamo wake wa kuzifunga timu zote za Vikosi katika ligi hiyo.

Salum amesema lazima zije vizuri timu za Vikosi kwani wamepania kuzichapa zote na uwezo huo wanao na huyo KMKM aliyenusurika na kipigo mzunguko wa pili waje vizuri.

“Ahadi yangu ile ile Kisandu nakuambia tena mana nshawahi kukuambia, timu...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Hakuna mbabe Taifa Jang’ombe na Jang’ombe Boys

Mchezo wa Derby ya Jangombe kati ya Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys umemalizika kwa kwenda sare ya mabao 2-2, mchezo ambao ni wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa saa 10 za jioni katika Uwanja wa Amaan.

Kikosi cha Jang'ombe boysKikosi cha Jang’ombe boys

Mabao yaTaifa kafunga Omar Yussuf Chande dakika 9 na Abdallah Mudhihir dk 60 wakati mabao ya Boys yote kafunga Khamis Mussa (Rais) dk 45 na 53.

Kikosi cha Taifa Jang[ombeKikosi cha Taifa Jang[ombe

Leo ni mchezo wa nne kukutana timu hizo katika mashindano mbali mbali...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Simba yabeba point 3 mbele ya Taifa Jang’ombe

Baada ya kuchezwa mchezo wa pili wa Kundi A Kombe la Mapinduzi 2017 leo January 1, usiku wa January 1 ilikuwa ni zamu ya wekundu wa Msimbazi Simba kucheza mchezo wao wa kwanza wa Kundi A dhidi ya Taifa Jang’ombe katika uwanja wa Amaan Zanzibar.

Huu ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba lakini ulikuwa ni mchezo wa pili kwa Taifa Jang’ombe ambao mchezo wao wa awali walicheza dhidi ya Jang’ombe Boys na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Hassan Seif mnamo dakika...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Jku yaipiga mkono Taifa ya Jang’ombe: Ubaoni JKU 5-1 Taifa ya Jang’ombe

Timu ya Jku imeendeleza ubabe wake na kuendeleza rekodi yake ya kutokufungwa kufuatia kuiandika Taifa ya Jang’ombe ‘wakombozi wa ng’ambo’ 5-1 katika mechi ya mchezo wa ligi kuu Zanzibar kanda ya Unguja uliochezwa katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

Wafungaji wa JKU ni Emmanuel Martin (dkk 28 na dk86), Is-haka Othman ‘Bopa’ (dkk 37), Nassor Mattar (dkk 55) na Mohammed Abdalla (dkk 89)
Mfungaji wa Taifa ya Jang’ombe ni Hassan Msabah (dkk 20)

Kwa matokeo hayo JKU imeendelea kujikita kileleni...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani