Taifa Na Boys kuzindua kombe la Mapinduzi Disemba 30, Yanga na Azam kundi moja

Pazia la Mashindano ya Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Disemba 30, 2016 katika uwanja wa Amaan saa 2:15 Usiku ambapo kutakuwa na mchezo wa Derby ya Jangombe kati ya Taifa ya Jangombe na Jangombe boys ambapo mashindano ya msimu huu yameshirikisha vilabu 9, vitano vikitokea Zanzibar, vitatu Tanzania bara na kimoja kutaka Uganda ambao ndio mabingwa watetezi timu ya URA.

 

KUNDI A : Simba, URA, KVZ, Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys.

 

KUNDI B : Yanga, Azam, Zimamoto...

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Mtanzania

Yanga, Azam kundi moja Mapinduzi

ratibaHUSSEIN OMAR NA KOMBO ALI, ZANZIBAR

KLABU za Yanga na Azam zimepangwa kundi moja kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi visiwani Zanzibar, Januari 2, mwakani katika Uwanja wa Amaan.

Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa jana, Yanga na Azam wako Kundi B la michuano hiyo pamoja na timu za Mafunzo na Mtibwa Sugar ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wakati Kundi A, lina timu za Simba, URA ya Uganda, JKU ya Unguja na Jamhuri ya Pemba kundi ambalo linaonekana kuwa dhaifu...

 

1 year ago

Michuzi

YANGA WAPANGWA KUNDI MOJA NA SINGIDA UNITED KOMBE LA MAPINDUZI

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara timu ya soka ya Yanga imepangwa kundi moja na Singida United katika ushiriki wa michuano ya kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu huko visiwani Zanzibar.
 Yanga imepangwa katika kundi B lenye jumla ya timu sita huku kundi A lenye timu za Simba na Azam FC lina jumla ya timu tano.

Bingwa Mtetezi wa kombe hilo ni Azam ambao wapo kundi moja na mabingwa wa kombe la Shirikisho Simba sambamba na URA kutoka Uganda,Jamhuri na...

 

2 years ago

Michuzi

AZAM YAPANGWA KUNDI B NA YANGA, YAJIZATITI KUCHUKUA KOMBEKLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imepangwa Kundi B kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayotarajia kufanyika ndani ya Uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar kuanzia Desemba 30 hadi Januari 13 mwakani.

Uongozi wa Azam FC umeweka wazi mikakati yao ya kutaka kuuchukua ubingwa wa msimu huu  ambapo kwa mwaka huu iliishia hatua ya makundi huku ikiwa  imepangwa pamoja na Yanga kwa mara ya pili mfululizo na timu nyingine zikiwa ni Jamhuri na Zimamoto, zote za visiwani humo.
Timu hiyo...

 

2 years ago

MillardAyo

VIDEO:Goli moja la Himid Mao liloipa Azam FC kombe la Mapinduzi , Full Time 1-0

Tarehe 30 2016 ndio ilikuwa siku ambayo mashindano ya Mapinduzi Cup yalifunguliwa na leo January 13 2016 Kombe la Mapinduzi lilifikia katika hatua ya fainali ambapo   Azam FC walikutana na Simba SC kucheza katika hatua ya fainali  na Azam FC waliibuka washindi baada ya kuifunga Simba kwa goli 1-0 Goli la Azam FC lilifungwa katika dakika ya […]

The post VIDEO:Goli moja la Himid Mao liloipa Azam FC kombe la Mapinduzi , Full Time 1-0 appeared first on...

 

3 years ago

Mwananchi

Kombe la Mapinduzi lilete tija Yanga, Azam, Simba

Inawezekana kuhoji mashindano haya ya Kombe la Mapinduzi yaliyoanza jana kisiwani Zanzibar na kushirikisha timu mbalimbali, zikiwamo za Ligi Kuu ya Bara, yana manufaa gani kwa maendeleo ya soka?

 

3 years ago

Zanzibar 24

Simba, Yanga na Azam wapata mualiko Kombe la Mapinduzi

Mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanategemewa kuanza rasmi tarehe 1 January, 2017 hadi tarehe 13 January, 2017 ambapo vilabu vikubwa kutoka Tanzania Bara Simba, Yanga na Azam tayari wameshapelekewa mualiko wa kushiriki Mashindano hayo.

Akizungumza na Mtandao huu Katibu wa chama cha Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” Kassim Haji Salum amesema tayari wameshatoa mualiko kwa timu tatu kubwa za Tanzania Bara.

“Tayari tumeshatoa mualiko kwa timu tatu za Bara wakiwemo Simba, Yanga na Azam zote tumeziomba...

 

3 years ago

MillardAyo

Cheki pichaz na matokeo ya mchezo wa kukamiana wa Yanga na Azam FC Kombe la Mapinduzi

Bado burudani ya soka ipo Zanzibar kwa kuendelea kuchezwa michezo ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kupigwa mchezo wa tatu wa Kundi B mchana wa January 5 kwa kuzikutanisha timu za Mafunzo ya Zanzibar na Mtibwa Sugar ya Morogoro na mchezo kumalizika kwa Mtibwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0. Usiku wa January 5 ulichezwa […]

The post Cheki pichaz na matokeo ya mchezo wa kukamiana wa Yanga na Azam FC Kombe la Mapinduzi appeared first on TZA_MillardAyo.

 

4 years ago

Vijimambo

MSUVA APIGA HAT TRICK YANGA IKIIADHIBU TAIFA 4-0 KOMBE LA MAPINDUZI

Simon Msuva amefunga mabao matatu na kupika moja, Yanga SC ikiifumua mabao 4-0 Taifa ya Jang’ombe katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Mapinduzi, uliofanyika Uwanja wa Amaan usiku huu. Kazi nzuri iliyofanywa na Winga machachari wa Yanga Simon Msuva, imeiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya timu ya Taifa Jang'ombe katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Aman Mjini Zanzibar. Mabao matatu kati ya manne yalifungwa na Simon Msuva katika...

 

4 years ago

Vijimambo

AZAM NA YANGA TAIFA LEO KOMBE LA NGAO


Mpaka sasa ni 0-0 mpira ni mapumziko
Washambuliaji wa Yanga Saimon Msuva, Donald Ngoma raia wa Botoswana na Vicent Bossou raia wa Mali wanaitetekisha ngome ya Azam kila Mara kutokana na mashambulizi ya Mara Kwa Mara kutoka Kwa winga wao Kijana mdogo Geofrey Mwashiuya. Yanga kipindi cha kwanza walitoa mashambulizi kutoka upande wa Kusin kenda kaskazini kipindi cha pili Yanga watatoa mashambulizi kutoka kaskazini kwenda Kusin, historian ya uwanja huu wa Taifa goli la upande wa kusini uwa...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani