Taifa ya Jang’ombe, JKU zaipiku Yanga ndani ya kikosi cha Zanzibar heroes

Timu ya Taifa ya Jang’ombe na JKU zimeongoza kutoa idadi kubwa ya wachezaji ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) baada ya kutoa wachezaji wanne kila timu ndani ya kikosi hicho chenye wachezaji 30.

 

Wachezaji wanne wa Taifa ya Jang’ombe waliyoitwa katika kikosi hicho nahodha wao ambae ni mlinda mlango Ahmed Ali “Salula”, mlinzi wa kati kinda Ibrahim Abdallah, kiungo Abdul Aziz Makame pamoja na mshambuliaji Ali Badru.

 

JKU ambayo nao wametoka idadi ya wachezaji wanne katika kikosi hicho yupo mlinda mlango wao Mohammed Abdulrahman “Wawesha”, mlinzi wa kati Issa Haidar “Mwalala”, kiungo Amour Suleiman “Pwina” pamoja na kiungo mshambuliaji Fesal Salum “Fei toto”.

 

Yanga imekama nafasi ya tatu katika orodha ya timu zilizotowa wachezaji wengi katika kikosi hicho ambapo imetoa wachezaji watatu akiwemo mlinzi wao wa kati Abdallah Haji “Ninja”, mlinzi wa kushoto Haji Mwinyi Ngwali pamoja na mshambuliaji Mateo Anton.

 

Jumapili iliyopita Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes),Hemed Suleiman (Morocco) alitangaza kikosi cha wachezaji 30 kwa ajili ya maandalizi ya kujiandaa na Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 hadi Disemba 9, 2017 nchini Kenya.

 

Kikosi kamili hicho:-

WALINDA MLANGO

Ahmed Ali “Salula” (Taifa ya Jang’ombe)

Nassor Mrisho (Okapi)

Mohammed Abdulrahman “Wawesha” (JKU)

 

WALINZI

Abdallah Haji “Ninja” (Yanga)

Mohd Othman Mmanga (Polisi)

Ibrahimm Mohammed “Sangula” (Jang’ombe Boys)

Adeyum Saleh “Machupa” (Kagera Sugar)

Haji Mwinyi Ngwali (Yanga)

Abubakar Ame “Luiz” (Mlandege)

Issa Haidar “Mwalala” (JKU)

Abdulla Kheir “Sebo” (Azam)

Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang’ombe)

 

VIUNGO

Abdul-swamad Kassim (Miembeni City)

Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang’ombe)

Mudathir Yahya (Singida United)

Omar Juma “Zimbwe” (Chipukizi)

Mohd Issa “Banka” (Mtibwa Sugar)

Amour Suleiman “Pwina” (JKU)

Mbarouk Marshed (Super Falcon)

Ali Yahya (Academy Spain)

Hamad Mshamata (Chuoni)

Suleiman Kassim “Seleembe” (Majimaji)

 

WASHAMBULIAJI

Kassim Suleiman (Prisons)

Matteo Anton (Yanga)

Ali Badru (Taifa ya Jang’ombe)

Feisal Salum (JKU)

Salum Songoro (KVZ)

Khamis Mussa “Rais” (Jang’ombe boys)

Mwalimu Mohd (Jamhuri)

Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto)

 

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

The post Taifa ya Jang’ombe, JKU zaipiku Yanga ndani ya kikosi cha Zanzibar heroes appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Zanzibar 24

Jku yaipiga mkono Taifa ya Jang’ombe: Ubaoni JKU 5-1 Taifa ya Jang’ombe

Timu ya Jku imeendeleza ubabe wake na kuendeleza rekodi yake ya kutokufungwa kufuatia kuiandika Taifa ya Jang’ombe ‘wakombozi wa ng’ambo’ 5-1 katika mechi ya mchezo wa ligi kuu Zanzibar kanda ya Unguja uliochezwa katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

Wafungaji wa JKU ni Emmanuel Martin (dkk 28 na dk86), Is-haka Othman ‘Bopa’ (dkk 37), Nassor Mattar (dkk 55) na Mohammed Abdalla (dkk 89)
Mfungaji wa Taifa ya Jang’ombe ni Hassan Msabah (dkk 20)

Kwa matokeo hayo JKU imeendelea kujikita kileleni...

 

3 months ago

Zanzibar 24

Zanzibar heroes kucheza na taifa ya Jang’ombe kesho

Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kesho Jumatano inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Taifa ya Jang’ombe pambano litakalopigwa majira ya saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan.

Zanzibar Heroes inajiandaa na Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017 nchini Kenya ambapo wamepangwa kundi A pamoja na ndugu zao Tanzania Bara, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar24.

The post Zanzibar heroes...

 

4 months ago

Zanzibar 24

Morocco atangaza kikosi cha Zanzibar Heroes, Ninja wa Yanga ndani

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes),Hemed Suleiman (Morocco) ametangaza kikosi cha wachezaji 30 kwa ajili ya maandalizi ya kujiandaa ma Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 hadi Disemba 9, 2017 nchini Kenya. WALINDA MLANGO Ahmed Ali “Salula” (Taifa ya Jang’ombe) Nassor Mrisho (Okapi) Mohammed Abdulrahman “Wawesha” (JKU) WALINZI Abdallah Haji “Ninja” (Yanga) Mohd Othman Mmanga (Polisi) Ibrahimm Mohammed “Sangula” (Jang’ombe Boys) Adeyum...

 

2 months ago

Zanzibar 24

Kikosi cha Zanzibar Heroes dhidi ya Libya, Wachezaji 8 wapya akiwemo Ninja wa Yanga

Kocha wa Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Hemed Suleiman “Morocco” ametangaza kikosi chake kitakachocheza leo kwenye Mashindano ya CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP kati ya Zanzibar dhidi ya Libya katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya, pambano litakalopigwa majira ya saa 08:00 za mchana.

ZANZIBAR HEROES

1.  Ahmed Ali (Salula) 1

2.  Mohd Othman Mmanga 6

3.  Haji Mwinyi Ngwali 16

4.  Abdullah Haji (Ninja) 5

5.  Issa Haidar Dau (Mwalala) 8 (Captain)

6.  Abdul azizi...

 

10 months ago

Zanzibar 24

Mjue mchezaji aliyefunga magoli mengi mechi za Jang’ombe Boys dhidi ya Taifa ya Jang’ombe.

Jina lake ni Khamis Mussa “Rais” ambae hadi leo bado rekodi yake haijavunjwa na mchezaji yoyote kwenye mechi ya Dabi ya Jang’ombe kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya Taifa ya Jang’ombe.

Ni Striker hatari wa Jang’ombe Boys, huyu jamaa ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi zilipokutana timu hizo.

Ameshafunga mabao mawili mpaka sasa na hakuna mwengine yeyote alifika mabao hayo.

Rais amefunga mabao hayo katika mchezo mmoja wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja ambapo...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Derby Taifa ya jang’ombe na jang’ombe boys kunogesha tamasha la fiesta

Tamasha la Fiesta 2016 Zanzibar litatanguliwa na mchezo maalum kwa kuwakutanisha Derby ya jang’ombe kati ya Taifa ya jang’ombe na jang’ombe Boys mchezo ambao utasukumwa Jumamosi tarehe 19/11/2016 saa 2:00 usiku katika Uwanja wa Amaan.

Mchezo huo ni maalum kwa kumtafuta nani mbabe wa jang’ombe ni Taifa au Boys ambapo wataoneshana siku hiyo kabla ya kukutana kwenye mchezo wao wa awali  ligi kuu soka Visiwani Zanzibar ambao utachezwa tarehe 10/12/2016.

Maandalizi yanaendelea vizuri kwani...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Victor Costa “Nyumba” ndani ya Taifa Jang’ombe

Victor Costa  “Nyumba” mlinzi aliengara sana miaka ya 2000 kutokana na uwezo aliokuwanao beki huyo wa Simba SC na timu ya taifa ya Tanzania, leo amewasili Visiwani Zanzibar na ujio wake kuja kusaini timu ya Taifa ya Jang’ombe.

Mtandao huu leo umemshuhudia mchezaji huyo akipokelewa Visiwani Zanzibar na Viongozi wa Taifa ya Jangombe na ndipo hapo ikataka kujua vipi inataka kumsajili au kuna nini kati yao.

Mtandao huu ukamtafuta msemaji wa timu hiyo ambae ni Haji Khalfan “Kiduka” ambapo yeye...

 

8 months ago

Mwanaspoti

Yanga waanzia Taifa Jang’ombe

Timu ya Yanga imeanza usajili wake kwa kumsajili mchezaji Abdallah Shaibu ‘Ninja’ aliyekuwa anakipiga katika timu ya Taifa Jang’ombe inayoshiriki katika Ligi Kuu ya nchini Zanzibar kwa mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo.

 

1 year ago

Zanzibar 24

Hakuna mbabe Taifa Jang’ombe na Jang’ombe Boys

Mchezo wa Derby ya Jangombe kati ya Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys umemalizika kwa kwenda sare ya mabao 2-2, mchezo ambao ni wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa saa 10 za jioni katika Uwanja wa Amaan.

Kikosi cha Jang'ombe boysKikosi cha Jang’ombe boys

Mabao yaTaifa kafunga Omar Yussuf Chande dakika 9 na Abdallah Mudhihir dk 60 wakati mabao ya Boys yote kafunga Khamis Mussa (Rais) dk 45 na 53.

Kikosi cha Taifa Jang[ombeKikosi cha Taifa Jang[ombe

Leo ni mchezo wa nne kukutana timu hizo katika mashindano mbali mbali...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani