TANZANIA NA KOMORO ZAAHIDI KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO.

Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Komoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba mapema wiki hii alikabidhi hati za utambulisho kwa Rais wa Muungano wa Visiwa vya Komoro Mhe. Azali Assoumani. Hafla ya kukabidhi hati hizo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Ikulu ya Komoro ijulikanayo kama Beit.

Wakati akihutubia, Mhe. Mabumba alijitambulisha kwa Mhe. Rais na kueleza furaha yake ya kuteuliwa kuwa Balozi wa pili kutoka Tanzania kuja kutumikia nchini Komoro. Aidha, alieleza furaha yake kwa mapokezi mazuri aliyoyapata tangu kuwasili kwake Visiwani humo na kwamba yamemfanya ajisikie yupo nyumbani. 

Alieleza kuwa anatambua kazi kubwa iliyopo mbele yake na kuahidi kuwa katika kipindi chake wakati akiwa Balozi nchini humo atajitahidi kukuza mahusiano yaliyopo baina ya Tanzania na Komoro. Sambamba na hilo, Mhe. Balozi alieleza dhamira yake ya kutaka kuona mahusiano baina ya nchi hizi mbili yanakuwa na manufaa kwa pande zote halikadhalika kukua kwa uhusiano wa kindugu kwani mahusiano baina ya Tanzania na Komoro ni ya kihistoria.

Pia Mhe. Rais Assoumani katika hotuba yake naye alianza kwa kuonyesha furaha yake ya kuwasili kwa Balozi pamoja na kukiri kupokea barua ya kurejea Balozi aliyepita na ya kuwasili kwa Balozi wa sasa. Vilevile alieleza kuwa kila Mkomoro hujisikia nyumbani pindi anapo tembelea Tanzania kutokana na ukarimu wanao onyeshwa wanapokuwa huko. 
Aidha Mhe. Rais alimuhakikishia Mhe. Balozi kuwa atarajie kupata ushirikiano wake pamoja na wa Serikali yake katika kipindi chote atakapo kuwa nchini humo.
Mhe. Balozi Mabumba alitumia fursa hiyo pia kumuomba Mhe. Rais Assoumani kufanye ziara ya kikazi nchini Tanzania ili kuweza kudumisha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili.


Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Komoro Mhe. Sylvester M. Mabumba (kulia) akiwasili katika Ikulu ya Komoro kwaajili ya hafla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho, kushoto ni Mnikulu wa Ikulu ya Komoro Bw.Hashim Mohamed. Hafla ya kukabidhi Hati hizo ilifanyika mapema wiki hii katika Ikulu hiyo.

Mhe. Balozi Mabumba akijitambulisha sambamba na kutoa salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kukabidhi Hati za Utambulisho. 
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

6 months ago

Michuzi

SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA UGANDA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wake wa kiuchumi na kidiplomasia baina yake na Uganda. Amesema Tanzania na Uganda zinauhusiano wa muda mrefu na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inafarijika na ushirikiano huo.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Oktoba 12, 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Bw. Richard Kaonero jijini Dar es Salaam.
“Tunaimani kubwa na...

 

2 years ago

Dewji Blog

Tanzania,Malaysia kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji- Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemhakikishia Waziri Mkuu wa Malaysia Mhe. Najib Razak kuwa serikali yake ya awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Malaysia hususani katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukuza biashara na uwekezaji.

Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 24 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kupokea barua yenye ujumbe wa Waziri Mkuu wa Malaysia iliyoletwa kwake na Mjumbe Maalum wa Waziri...

 

2 years ago

Dewji Blog

Wajasiriamali Wanamama kutoka Tanzania waingia mkataba wa ushirikiano na wenzao wa Komoro

Ziara ya Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania (Tanzania Saccos for Women Enterprenuers) imezaa matunda baada ya kikundi hicho cha kina mama kufanikiwa kuingia mkataba wa ushirikiano (MoU) katika masuala ya biashara na Kukundi cha Wanawake Wajasiriamali wa Comoro (Association of Women Entrepreneurs in Comoro).

Makubaliano hayo ya ushirikiano yalifikiwa kufuatia ziara ya siku mbili iliyofanywa na Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania nchini Komoro tarehe 14 Juni...

 

2 years ago

Michuzi

BALOZI WA TANZANIA NCHINI KOMORO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KOMORO,

Balozi Chabaka Kilumanga akipokea zawadi kutoka kwa Rais. Azzali OusmanKutoka Kushoto Rais Azali Ousman, Balozi wat Tanzania nchini Komoro Mhe. Chabaka Kilimunga, Bw. Mudrick Soragha Mkuu wa Afisa Ubalozi na Bi. Sheehat Kassim Mkalimani .Mhe. Chabaka Kilumanga Balozi wa Tanzania ndani ya Muungano wa Visiwa vya Komoro leo tarehe 17 Oktoba, 2016 alikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Col. Azzali Ousmani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Komoro katika Ikulu ya Bait Salam. Hii ni mara...

 

1 year ago

Channelten

Kenya na Somalia zaahidi kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi

raisi

Marais wa Kenya na Somalia jana waliahidi kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi, kwa kupambana bila huruma na wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab, ambao wameongeza mashambulizi ya kigaidi kwenye nchi hizo mbili.

Rais Uhuru Kenyatta na Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wamekubaliana kuendelea na mapambano dhidi ya kundi la al-Shabaab hadi litakapokuwa sio tishio.

Akiongea mjini Nairobi kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo na mgeni wake kutoka Somalia, Rais...

 

11 months ago

Michuzi

BALOZI SYLEVESTER MABUMBA, BALOZI WA TANZANIA VISIWANI KOMORO AWASILISHA NAKALA YA HATI ZAKE ZA UWAKILISHI KWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KOMORO, MHE, MOHAMED BACCAR DOSSAR

Mhe. Sylvester Mabumba Balaozi wa Tanzania ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Komoro jana tarehe 09 Mei aliwasilisha nakala za hati zake za uwakilishi kwa Mhe. Mohambed Baccar Dossar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Komoro. Hafla hiyo ilifanyika siku hiyo hiyo ambayo Mhe. Balozi aliwasili Visiwani Komoro jambo ambalo linaonesha jinsi gani nchi hizi mbili zimedhamiria katika kuboresha na kukuza mahusiano yaliopo baina yao.

Katika hafla hiyo Mhe. Dossar alichukua fursa hiyo ...

 

4 years ago

Habarileo

Tanzania, India kuimarisha ushirikiano

TANZANIA na India zimeeleza kuridhishwa na uhusiano na ushirikiano uliopo baina yao na kusisitiza dhamira ya kweli ya kuuimarisha kwa faida ya wananchi. Hayo yalielezwa kwenye mazungumzo kati ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa India, Mohamed Hamid Ansari. Dk yuko nchini humo kwa ziara ya kikazi.

 

2 years ago

BBCSwahili

Tanzania na Kenya kuimarisha ushirikiano

Kenya na Tanzania zimekubaliana kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kukuza biashara.

 

2 years ago

Michuzi

Tanzania na Japan kuimarisha ushirikiano

Serikali imesisitiza umuhimu wa kupanua ushirikiano wake na Japan katika nyanja mbalimbali ili kuleta tija kwa nchi zote mbili.
Hayo yalielezwa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipokutana na ujumbe kutoka Japan ulioongozwa na Rais wa Chama cha Uchumi na Maendeleo ya Afrika (AFRECO), Tetsuro Yano aliyeambatana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida.
Ujumbe huo kutoka Japan ulimtembelea Waziri Muhongo ofisini kwake ili kujadiliana masuala...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani