TANZANIA YAKUBALI KUPELEKA WALIMU WA SOMO LA KISWAHILI RWANDA

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amepokea barua yenye ujumbe wa Rais wa Jamhuri wa Rwanda Mhe. Paul Kagame iliyowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum ambaye ni Waziri wa Elimu wa Rwanda Dkt. Musafiri Papias Malimba.

Pamoja na kupokea barua hiyo, Mhe. Rais Magufuli na Dkt. Musafiri Papias Malimba wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda ikiwemo katika sekta ya elimu hususani maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Rwanda kwa kuamua lugha ya Kiswahili ianze kufundishwa katika shule zake na ameahidi kuwa Tanzania ipo tayari kutoa walimu wa kwenda kufundisha lugha hiyo.

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

10 months ago

Bongo5

Rais Magufuli kupeleka walimu wa Kiswahili Rwanda

Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amepokea barua yenye ujumbe kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, iliyowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum ambaye ni Waziri wa Elimu wa Rwanda Dkt. Musafiri Papias Malimba.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam, Wengine ni Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura na Afisa...

 

10 months ago

Zanzibar 24

JPM kupelekwa walimu wa Kiswahili Rwanda

Rais Dkt. John Magufuli amepokea barua yenye ujumbe kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, iliyowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum ambaye ni Waziri wa Elimu wa Rwanda Dkt. Musafiri Papias Malimba.

Barua hiyo ambayo imepokelewa Alhamisi hii Ikulu, kutoka kwa mjumbe maalum akiwa ni waziri wa Elimu Rwanda Dkt Malimba, aliiwasilisha kwa Rais Magufuli.

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa pamoja na kupokea barua hiyo, Mheshimiwa Rais Magufuli na Dkt Malimba wamezungumzia masuala mbalimbali ya...

 

9 months ago

Mwananchi

Walimu wa Tanzania kwenda Afrika Kusini kufundisha Kiswahili

Rais John Magufuli amesema wamekubaliana na Rais Jacob Zuma kupeleka walimu kutoka Tanzania kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kufundisha Kiswahili.

 

8 months ago

CCM Blog

TANZANIA YAOMBWA KUISAIDIA SUDAN KUSINI WALIMU WA KISWAHILI

Jenerali TabanADDIS ABABA - ETHIOPIA
Serikali ya Sudan Kusini imeoimba Tanzania kuisaidia katika utoaji wa mafunzo mbalimbali kwa wataalamu wake hasa wa sekta ya afya, kilimo na kupatiwa walimu wa lugha la Kiswahili kwa sababu taifa hilo linataka kuanza kufundisha lugha hiyo kwenye shule mbalimbali nchini humo.

Makamu wa Kwanza Rais wa Serikali ya Sudan Kusini Jenerali Taban Deng Gai ametoa maombi hao baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kando mwa...

 

8 months ago

BBCSwahili

Sudan Kusini yaomba walimu wa Kiswahili kutoka Tanzania

Serikali ya Sudan Kusini imeoimba Tanzania kuisaidia katika utoaji wa mafunzo mbalimbali kwa wataalamu wake hasa wa sekta ya afya, kilimo na kupatiwa walimu wa lugha la Kiswahili.

 

3 months ago

RFI

Rwanda yakubali kuwapokea wahamiaji 30,000 wa Afrika kutoka Libya

Serikali ya Rwanda imesema iko tayari kupokea wakimbizi 30,000 wa Afrika kutoka Libya. Rwanda imejibu wito kutoka Umoja wa Afrika kufuatia suala la soko la watumwa nchini Libya.

 

10 months ago

Michuzi

KUNA MWENENDO MZURI KATIKA SOMO LA KISWAHILI-TWAWEZA

Na Hassan Silayo

Mwenendo wa somo la Kiswahili nchini umeendelea kuimarika na hii ni kutokana na jitihada mbalimbali ziliwekwa na serikali katika somo hilo.

Akitoa ripoti matokeo ya utafiti wa Uwezo,Meneja wa Uwezo Tanzania Zaida Mgalla alisema kuwa kwa watoto walikuwa darasa la tatu walioweza kufauli majaribio ya Kiswahili mwaka 2011 walikuwa asilimia 29 tofauti na asilimia 56 ya mwaka 2015.

Bi. Zaida Aliongeza kuwa kwa darasa la saba kumekuwa na ongezeko la watoto kujifunza na kufanya vizuri...

 

2 years ago

StarTV

Matokeo Kidato Cha Pili Wanafunzi wafaulu zaidi somo la Kiswahili

 

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili 2015 ambapo wanafunzi 324,068 sawa na asilimia 89.12 ya watahiniwa 363,666 wamefaulu huku somo la Kiswahili likiongoza kwa ufaulu wa asilimia 86.34 na somo la hesabu ukiwa chini zaidi kwa asilimia 15.21.

Miongoni mwa waliofaulu wasichana ni 164,547 sawa na asilimia 89.00 na wavulana 159,521 sawa na asilimia 89.24 na wengine 39,567 sawa na asilimia 10.88 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha...

 

4 years ago

Tanzania Daima

Wanaharakati, walimu watoa somo Bunge la Katiba

WANAHARAKATI mbalimbali nchini wamewataka wajumbe wa Bunge la Katiba kuwa makini na kutunga kanuni ambazo hazitawanyima uhuru wa kupaza sauti makundi yaliyoko pembezoni. Wito huo ulitolewa jijini Dar es Salaam...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani