TANZANIA,HISPANIA WAANDAA KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI MJINI MADRID

Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa ambao pia unawakilisha Tanzania katika nchi ya Hispania kwa kushirikiana na Shirikisho la wafanyabiashara la Madrid (Madrid chamber of commerce – CAMARA) pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) uliandaa kongamano la kwanza la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Hispania tarehe 12/03/2018 mjini Madrid. 
Kongamano hilo liliudhuriwa na watendaji wakuu wa makampuni makubwa Madrid nchini Hispania yapatayo 60. Kongamano hilo lilifunguliwa na Bw. Augusto de Castaneda, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara la Madrid. Katika kongamano hilo, Mhe. Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Hispania, mwenye makazi nchini Ufaransa, aliyashawishi makampuni hayo kuja kuwekeza nchini Tanzania. 
Balozi Shelukindo alieleza juhudi mbalimbali alizozichukua Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamuhri ya muumngano wa Tanzania katika kupambana na rushwa jambo ambalo limetengeza mazingira bora ya kufanya biashara na kuwekeza nchini. Balozi Shelukindo alieleza kwamba hali ya utulivu na usalama ambayo imeendelea kuwepo nchini Tanzania imekuwa ni kivutio kikubwa cha uwekezaji kutoka nje. 
Bw. Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ambaye alishiriki katika kongamano hilo aliezea mazingira bora ya uwekezaji nchini pamoja na fursa mbalimbali zinazoweza kupatikana Tanzania. 
Pia aliendelea kuelezea jinsi Kituo cha Uwekezaji kilivyojiandaa kuwapokea wawekezaji kutoka Hispania kuja kuwekeza nchini kwa kuwasaidia kujua taratibu na sheria mbalimbali zinazohusu uwekezaji nchini. Aidha Bw. Mwambe alielezea fursa za kipaumbele ambazo ni viwanda, kilimo, miundombinu pamoja na nisharti. 
Bi. Devota Mdachi, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) alitoa mada kuhusu vivutio vya utalii vinavyopatikana nchini Tanzania na kuyakaribisha makampuni ya Hispania kuja kuwekeza katika sekta hiyo muhimu katika uchumi wa Tanzania. Bw. Gilead Teri Mkurugenzi wa Sera kutoka Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) alielezea mchango wa sekta binafsi katika uchumi wa Tanzania na namna Taasisi hiyo itakavyoshirikiana na wawekezaji kutoka Hispania. 
Baada ya kongamano hilo Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara la Madrid Bw. Augusto de Castaneda aliahidi kwamba wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Hispania watafanya ziara nchini Tanzania hivi karibuni kuchangamkia fursa hizo.Mheshimiwa, Samwel Shelukindo Balozi wa Tanzania nchini Hispania mwenye makazi Ufaransa , Makamu wa Rais wa Madrid Chamber of Commerce Bw. Augusto de Castaneda Bw. Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania na Bi. Devota Mdachi, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakiwa kwenye meza kuu wakati wa kongamano hilo.Baadhi ya wawakilishi wa makampuni ya Kihiispania walioshiriki kwenye kongamano hilo.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Tanzania Daima

TPSF, TMS Consultants waandaa kongamano la uwekezaji

TAASISI ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wakishirikiana na Kampuni ya Kukuza Mitaji ya (TMS Consultants) imewaomba wadau wa maendeleo kushiriki katika kongamano la kimataifa la siku tatu kuhusu uwekezaji wa...

 

2 years ago

Michuzi

KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA INDIA

Kufuatia tukio la ugeni wa kitaifa wa Mheshimiwa Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India hapa nchini, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), pamoja na Jukwaa la Biashara la India (IBF) na Shirikisho la Biashara na Viwanda la India (FICCI) wanaandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika Siku ya Jumapili tarehe 10 Julai 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es...

 

1 year ago

Michuzi

TAARIFA YA KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MAURITIUS

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Taasisi ya Sekta Binafsi ya Tanzania (TPSF); Bodi ya Uwekezaji ya Mauritius (BOI), Taasisi ya Biashara na Viwanda ya Mauritius (MCCI) pamoja na Shirika la Serikali la Viwanda Vidogovidogo la Mauritius (Enterprise Muritius kinaratibu Kongamano la Biashara na Uwekezaji Kati ya Tanzania na Mauritius litakalofanyika tarehe 23 Machi, 2017 Port Louis, Mauritius. 
Lengo la kongamano hili...

 

9 months ago

Michuzi

Siku ya Kongamano la Biashara ya Kilimo na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uholanzi yafanaKatika kutekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi, Ubalozi wa Tanzania kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi uliopo Tanzania, Wizara ya Masuala ya Uchumi na Wizara ya Mambo ya Nje za Uholanzi na Taasisi ya Netherlands–African Business Council (NABC)kwa pamoja ziliandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji lililofanyika hapa The Hague, Uholanzi tarehe 31 Mei 2017. 
Lengo kuu la Kongamamo hilo, pamoja na kuendeleza na kukuza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uholanzi, nikutangaza fursa...

 

1 year ago

Michuzi

LAPF ILIVYOSHIRIKI KONGAMANO LA UWEKEZAJI MJINI MOROGORO

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Dk. Stephen Kebwe akizungumza katika kondamano la uwewkezaji linalofanyika mkoani Mrorogoro. (Picha na Francis Dande) Afisa Kumbukumbu wa LAPF, Florian Mbassa akitoa maelezo kuhusu Mfuko wa LAPF kwa mmoja wa washiriki wa kongamano hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Dk. Stephen Kebwe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kondamano la uwekezaji mijini Mrorogoro.  
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Morogoro, Lusingi Sitta (katikati) akiwa na Meneja Masoko na...

 

4 years ago

Michuzi

maandalizi ya kongamano la uwekezaji na biashara linaloanza kesho dar es salaam

Mkurugenzi wa Huduma wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Bi. Nakuala Senzia (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusiana na kongamano la siku mbili la uwekezaji na biashara linalotarajiwa kuanza kesho jijini Dar es Salaam.  Wengine katika picha ni Meneja Mawasiliano wa TIC Bi. Pendo Gondwe, (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Paul Omara (wa tatu kushoto), Afisa Habari Mkuu wa benki hiyo, Bi. Naomi Vincent na Mkuu wa...

 

4 years ago

Michuzi

TIC kuongoza kongamano la siku mbili la uwekezaji na biashara jijini Dar

Mkurugenzi wa Huduma wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Bi. Nakuala Senzia (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusiana na kongamano la siku mbili la uwekezaji na biashara linalotarajiwa kuanza kesho jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Meneja Mawasiliano wa TIC Bi. Pendo Gondwe, (katikati) na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Paul Omara. Benki hiyo ndiyo inayodhamini mkutano huo. Meneja Mawasiliano wa TIC Bi....

 

3 years ago

Dewji Blog

Makamu wa Rais Dkt. Bilal afungua kongamano la uwekezaji ukanda wa ziwa Tanganyika, mjini Kigoma

02

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika jana Sept 9, 2015 kwenye Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma. (Picha na OMR).

03

4

Mwakilishi wa Umoja wa wafanyabishara wa Burundi, akizungumza.

5

Waziri wa Nchi- Uwekezaji na Uwezeshaji, Eng. Christopher Chiza, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dkt. Bilal ili kufungua Kongamano hilo.

3

Sehemu ya...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani