TCRA YAWAASA WAMILIKI WA MITANDAO YA KIJAMII KUCHUJA HABARI ZAO KWA WEREDI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Wamiliki wa mitandao ya kijamii wameaswa kuchuja habari zao ambazo wamekuwa wakizipata na kuzisambaza kwa jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa Redio ama televisheni za Mitandaoni.
Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui , Valerie Msoka wakati alipokutana wamiliki wa mitandao ya Kijamii pamoja na waandishi wa habari, Valerie amesema kuwa upashanaji wa habari lazima kuangalia na usalama wa nchi pamoja kuacha uchochezi ambao unachonganisha na jamii au mamlaka.

Amesema kuwa takribani miaka mitano kulikuwa hakuna fursa za kupata matangazo ya televisheni kupitia mitandao ya kijamii, lakini sasa imeenea kwa watanzania wengi na inaendelea kuongezeka kadri ya teknolojia inavyokuwa, hivyo kunahitajika kuwepo umuhimu wa kusimamia huduma ya mitandao hiyo ili iweze kuleta tija kwenye taifa na si vinginevyo.

Valerie amesema kuwa TCRA kupitia kamati ya maudhui inatambua na kuthamini kuwepo kwa fursa ya upashanaji wa habari na serikali iliamua kuruhusu huduma hiyo wakati miongozo na taratibu stahiki zikiendelea kutayarishwa.
 Amesema vyombo vya habari katika mitandao ya kijamii vya Radio, Televisheni na bado teknolojia inaendelea kukua na haviwezi kuzuia kutokana na mfumo wa upashanaji wa habari. Mwenyekiti huyo anasema habari zingine hazina tija kwa jamii na zingine zinaleta uchochezi ndani ya jamii na wakati mwingine kuingilia faragha za watu ambazo ambazo hazitakiwa kufikia jamii kama sehemu ya habari.

Amesema wadau wa mitandao ya kijami na watumiaji wa mitandao hiyo wanahakikisha wanahabarisha kwa kuzingatia habari zizojenga umoja wa kitaifa, mshikamano na ushirikiano baina ya watanzania bila kujenga hofu , kuchochea chuki na uhasama baina ya watanzania. Aidha amesema habari za matusi katika mitandao ya kijamii hayavumiliki ,kwani zinakiuka misingi ya uandishi na uhuru na wajibu wake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa TCRA, Valerie Msoka akizungumza na wadau wa mitandao ya kijamii juu uchujaji wa habari ambazo zinatakiwa  kuwafikia jamii na zinazolenga uimarishaji wa usalama wa nchi na mshikamano watanzania, leo jijini Dar es Salaam.Picha na Michuzi Jr-Michuzi Media Group.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa TCRA, Valerie Msoka (katikati) akipitia taarifa wakati wa mkutano wa wadau wa mitandao ya kijamii ambao wanasambaza taarifa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maudhui, Abdul Ngalawa na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka.
Kaimu Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka akizungumza katika mkutano wa wadau wa mitandao ya kijamii ambao wasambazaji wa taarifa kwa jamii leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waandishi wa habari na wamiliki wa mitandao ya Kijamii wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wamiliki wa Mitandoa ya Kijamii, kutoka Jamii Media Maxence  Mello akichangia jambo katika suala zima la uchujaji wa Habari katika mitandano ya Kijamii, katika mkutano uliowahusu Wamiliki wa radio, Televisheni za mtandaoni na mitandano mingine ya kijamii uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),mapema leo jijini Dar
Mmoja wa wamiliki wa Mitandao ya Kijamii,kutoka Mtembezi Media,Antonio Nugaz akichangia jambo katika suala zima la uchujaji wa Habari katika mitandano ya Kijamii,ndani ya mkutano uliowahusu Wamiliki wa radio,Televisheni za mtandaoni na mitandano mingine ya kijamii uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),mapema leo jijini  Dar

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

5 months ago

Malunde

TCRA YAWAONYA WAMILIKI WA MITANDAO YA KIJAMII

Wamiliki wa mitandao ya kijamii wameaswa kuchuja habari zao ambazo wamekuwa wakizipata na kuzisambaza kwa jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa Redio ama televisheni za Mitandaoni.
Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui , Valerie Msoka wakati alipokutana na baadhi ya wamiliki wa mitandao ya Kijamii pamoja na waandishi wa habari.

Valerie amesema kuwa upashanaji wa habari lazima kuangalia na usalama wa nchi pamoja kuacha uchochezi ambao unachonganisha jamii au mamlaka.

Amesema kuwa...

 

2 years ago

Dewji Blog

MSEMAJI WA SERIKALI: Wamiliki wa Blog/mitandao ya kijamii zingatieni maadili ya upashaji habari za Uchaguzi Mkuu Okt 25

DSC_4292

Mkurugenzi Idara ya Habari, Assah Mwambene (mwenye suti nyeusi aliyesimama-kulia) akisikiliza kwa makini mawazo na maoni yaliyokuwa yakitolewa na  Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

DSC_4305

Mkurugenzi Idara ya Habari, Assah Mwambene (kushoto) akisikiliza kwa makini maoni yaliyokuwa yakitolewa na Umoja wa Bloggers Tanzania (TBN), Kulia kwake ni Afisa wa Idara hiyo.

Na Andrew Chale, Modewjiblog

[DAR ES SALAAM]...

 

3 years ago

Vijimambo

KAMANDA MPINGA ATOA ONYO KWA WAMILIKI WA MITANDAO YA KIJAMII

Kamanda Kikosi cha Usalama BarabaraniMohamed Mpinga Na Mwandishi Wetu
KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani (Trafic), Mohamed Mpinga , ameonya wamiliki wa mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi na kuthibitika kama zina ukweli ndani yake.

Kamanda Mpinga, alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la baadhi ya mitando kusambaza taarifa kuwa kulikuwa na basi la Kampuni ya Dar Express limepata ajali.

Alisema,...

 

3 years ago

Michuzi

KAMANDA MPINGA ATOA ONYO KWA WAMILIKI WA MITANDAO YA KIJAMII INAYOPOTOSHA UMMA

Na Mwandishi Wetu
KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania (Trafic), Mohamed Mpinga (pichani), ametoa onyo kwa  baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi na kuthibitika kama zina ukweli ndani yake.
Kamanda Mpinga, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la baadhi ya mitando kusambaza taarifa kuwa kulikuwa na basi la Kampuni ya Dar Express limepata ajali.
Alisema, onyo hilo...

 

3 years ago

Michuzi

BASATA, TCRA WATAKA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO YA KIJAMII KWA WASANII

Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) mapema wiki hii wamelaani matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii miongoni mwa wasanii wakati wa programu ya Jukwaa la Sanaa iliyofanyika makao makuu ya Baraza hilo yaliyoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati akiwasilisha mada iliyohusu ‘Matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa wasanii’, Meneja mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy alisema kuwa wasanii ni kioo cha jamii hivyo kwa...

 

1 year ago

Channelten

Makundi ya mitandao ya kijamii yameshauriwa kutoitumia mitandao hiyo kwa kupashana habari peke yake

Makundi ya mitandao ya kijamii yameshauriwa kutoitumia mitandao hiyo kwa kupashana habari peke yake ,badala yake waitumie pia katika kuwaunganisha pamoja na kuhamasishana kubuni na kuanzisha miradi ya kimaendeleo kama,kilimo,biashara na ufugaji ili wajikwamue kiuchumi waondokane na umaskini.

Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba,ametoa ushauri huo wakati akifungua semina ya kwanza ya kundi la mtandao wa kijamii la fursa kanda ya kaskazini, iliyofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na...

 

3 years ago

Mwananchi

TCRA yawaonya viongozi wa dini na mitandao ya kijamii

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka viongozi wa dini kutumia nafasi kukemea juu ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwa waumini wao na kuelimisha madhara yanayoweza kusababishwa na teknolojia hiyo katika jamii.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani