TFF YAUNDA KAMATI YA TUZO ZA WACHEZAJI CHINI YA MSAFIRI MGOYI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeunda Kamati ya Tuzo za Wachezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, chini ya Mwenyekiti, Ahmed Iddi Mgoyi, maarufu kama Msafiri Mgoyi.
Katika Kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti atakuwa Almasi Kasongo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam, wakati Katibu Mkuu ni Amir Mhando, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu itakuwa inachagua wachezaji bora wa mwezi, goli  bora, mwamuzi bora, kocha, kipa bora na mchezaji bora wa msimu. 
Ahmed Iddi Mgoyi maarufu kama Msafiri Mgoyi ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za Wachezaji Bora wa Ligi Kuu
Wajumbe wa Kamati hiyo ni Katibu Mkuu wa zamani wa Simba SC, Patrick Kahemele, Kocha wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula, mchezaji wa zamani wa kimataifa nchini, Said George na Waandishi wa Habari Ibrahim Masoud, Fatma Likwata, Salehe Ally, Gift Macha na Zena Chande.

 Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Alfred Lucas

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Michuzi

TFF YAUNDA KAMATI YA TAIFA STARS


Katika kuimarisha maandalizi ya Timu ya Taifa (Taifa Stars) kuelekea katika mashindano mbalimbali ikiwemo mechi mbili za ugenini na nyumbani dhidi ya Algeria, Rais wa TFF Jamal Malinzi ameunda kamati maalum itakayoitwa “Kamati ya Taifa Stars” ambayo majukumu yake yatakua:(i) Kuimarisha huduma kwa wachezaji,(ii) Uhamasishaji na Masoko,(iii) Kuhamasisha wachezaji,(iv) Kuandaa na kusimamia mkakati wa Ushindi.
Kamati hii itaongozwa na Mwenyekiti Farough Baghouzah, Teddy Mapunda (Katibu), Wajumbe...

 

3 years ago

Michuzi

TFF YAUNDA KAMATI YA USHAURI YA LIGI

RAIS wa Shirikiso la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi ameteua Kamati ya ushauri ya Ligi Kuu (VPL) na ligi Daraja la Kwanza (FDL) nchini.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Alhaj Ahmed Mgoyi na katibu wa Kamati ni mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi nchini (TPLB) na wajumbe wengine saba.
1. Alhaji Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti)2. Boniface Wambura (Katibu)3. Kennedy Mwaisabula- Mjumbe4. Idd Mshangama- Mjumbe5. Amiri Mhando- Mjumbe6. Grace Hoka- Mjumbe7. Ibrahim Kaude (Vodacom)- Mjumbe8. Baruan Muhuza...

 

4 years ago

Tanzania Daima

Taswa yaunda Kamati ya Tuzo

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), kimeunda Kamati Maalumu ya kusimamia utoaji wa Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania. Kamati hiyo ya watu 12, itakuwa chini ya uenyekiti...

 

6 months ago

Michuzi

NYAMLANI, MGOYI WATEULIWA TFF

 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia amewateua Makamu wa Rais wa zamani wa TFF, Athuman Nyamlani na Ahmed Mgoyi kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF. Rais Karia ameteua kwa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo katika Katiba ya TFF ikiwa ni wiki moja baada ya kupatikana kwa viongozi wa shirikisho katika uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 12, mwaka huu.
Rais Karia aliwatambulisha viongozi hao kwenye Kikao cha Kamati ya Utendaji iliyofanyika Jumanne Agosti 22, mwaka huu...

 

10 months ago

MillardAyo

LIVE: Kutoka TFF kamati ya hadhi za wachezaji inazungumza na waandishi

Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji iliyochini ya wakili Richard Sinamtwa inazungumza na waandishi wa habari muda huu kutoka katika makao makuu ya shirikisho la soka Tanzania TFF, bado haijawekwa wazi wanachozungumza lakini kuna uwezekano mkubwa ikawa ni mvutano wa point tatu kayi ya Simba vs Kagera Sugar. VIDEO: Adhabu aliyopewa Haji Manara wa Simba […]

The post LIVE: Kutoka TFF kamati ya hadhi za wachezaji inazungumza na waandishi appeared first on millardayo.com.

 

2 years ago

Dewji Blog

UEFA yatoa orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka, Neymar apigwa chini

Chama cha Soka barani Ulaya (UEFA) kimetangaza oodha ya wachezaji 10 ambao watawania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya.

Katika hali ambayo imewashangaza wengi, mshambuliaji wa Barcelona, Neymar amekosekana katika oodha hiyo licha ya kuisaidia Barcelona kushinda kombe la Liga kwa msimu wa 2015/2016 kwa kufunga goli 31 katika michezo 49.

Aidha katika orodha hiyo, hakuna mchezaji hata mmoja wa ambaye anacheza Ligi Kuu ya Uingereza hali ambayo inafanya kuwepo na mtizamo tofauti kuhusu...

 

5 months ago

Michuzi

Msafiri Zawose awaomba Watanzania kumpigia kura Tuzo za Afrima

 Na Humphrey Shao
Msanii wa Muziki wa Asili nchini anayetamba katika majukwaa ya kimataifa Msafiri Zawose amewataka watanzania wazidi kumpigia kura hilo aweze kutwaa tuzo ya Afrima katika kipengele cha Muziki wa asili
Zawose ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa Michuzi blog juu ya Mipango yake ya kufanya matamasha nje ya nchi.
"Cha kwanza ni kuwataka watanzania waingie katika website ya afrima kisha kipita katika kipengele cha best tradional music na kumchagua Msafiri Zawose...

 

2 years ago

Habarileo

ZFA yaunda Kamati tano

CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA) Taifa kimeunda kamati tano zitakazosimamia masuala ya soka visiwani. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa chama hicho, Masoud Attai alipozungumza na gazeti hili ofisini kwake Amaan mjini Unguja.

 

5 months ago

BBCSwahili

Msanii Msafiri Zawose amechaguliwa kuwania Tuzo za Muziki za Afrika, Afrima

Msanii Msafiri Zawose amechaguliwa kuwania Tuzo za Muziki za Afrika, zinazofahamika kwa jina la Afrima katika kipengele cha muziki wa Asili

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani