TFF:KAMATI YA MAADILI YAPITIA SHAURI LA WATUHUMIWA WA KUGHUSHI NA UDANGANYIFU WA MAPATO.

Kamati ya Maadili iliyokutana Januari 18, 2018 imepitia shauri lililowasilishwa na Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF wakiwatuhumu viongozi wanne kwa makosa ya kughushi na udanganyifu wa mapato kwenye mchezo namba 94 kati ya Ndanda FC na Simba uliochezwa Disemba 30,2017.
Shauri la kwanza lililomuhusu Katibu msaidizi wa Ndanda Ndugu Selemani Kachele,Kamati imegundua kuwa mtuhumiwa aliitwa wakati wa kuhesabu mapato kuthibitisha deni dhidi ya Ndanda lenye thamani ya Shilingi Milioni mbili laki mbili na elfu hamsini(2,250,000),deni ambalo TFF waliagiza wakatwe kwenye mapato ya mechi hiyo,Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mtwara alithibitisha kuwa alimuita kuthibitisha uhalali wa deni hilo baada ya Muhasibu wa Ndanda kugoma kulipa deni hilo ambalo linahusu pango la Ndanda kwa Mama mwenye Nyumba.
Hata hivyo Kamati ilimuhoji zaidi na akashindwa kutoa uthibitisho wa kulipwa kwa deni hilo na hakuna kumbukumbu zozote zinazoonyesha kuwa deni hilo limelipwa.Kamati imempa onyo kwa mujibu wa kifungu cha 6(1)(a) kanuni za maadili ya TFF toleo la 2013 na imeiomba Sekretarieti ya TFF ifuatilie kama deni hilo limeshalipwa ili kuepusha ulipaji wa Zaidi ya mara moja.
Shauri la Pili lilimuhusu Muhasibu msaidizi wa Simba Ndugu Suleiman Kahumbu.Kamati haikuendelea na tuhuma dhidi yake baada ya Sekretarieti ya TFF kuamua kuondoa shauri dhidi yake kwa kuwa alitoa ushirikiano na kutosheka kuwa hana hatia na badala yake alitumika kama shahidi wa upande wa washtaki.
Shauri la tatu lilimuhusu Katibu mkuu wa Chama cha soka Mtwara Ndugu Kizito Mbano.Kamati ilimuhoji mtuhumiwa na alikiri kuwepo kwa mawasiliano na msimamizi wa kituo Ndugu Dunstan Mkundi kuhusu nia ya kughushi fomu ya marejesho ya mapato ya mchezo kati ya Ndanda FC na Simba SC.
Ndugu Kizito Mbano hakutoa taarifa yoyote ile wala kuonyesha ushirikiano kwa Sekretarieti ya TFF na Bodi ya Ligi wakati yeye akiwa msimamizi msaidizi wa kituo na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Mtwara,hivyo Kamati imemkuta na hatia na imemuhukumu kutojihusisha na shughuli za Mpira wa Miguu kwa kipindi cha miaka Mitano(5) kwa mujibu wa kifungu cha 73(7) cha kanuni za maadili TFF toleo la 2013.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

StarTV

Watuhumiwa watatu wafikishwa mahakamani  kwa makosa ya kughushi na udanganyifu.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU imewafikisha mahakamani aliyekuwa Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Harry Kitilya pamoja na wafanyakazi wawili wa Benki ya Stanbic Tanzania Shose Senare na Sioi Solomoni kwa makosa nane ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Katika makosa hayo watuhumiwa Harry Kitilya na Sioi Solomoni wanakabiliwa na makosa manne wakati Shose Senare akikabiliwa na makosa yote nane.

 Mbele ya hakimu mkazi mkuu wa mahakama ya hakimu...

 

1 year ago

Michuzi

SHAURI LA KESSYT LARUDI KAMATI YA SHERIA TFF

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ilikutana jana Jumapili Novemba 27, 2016 kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Bodi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia mashauri manane.a
Shauri la 1. Klabu ya Simba dhidi ya Young Africans na mchezaji Hassan Hamis Ramadhani Kessy
Shauri hili sasa limerudi rasmi kwenye meza ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji. Kamati iliyoketi chini ya Makamu Mwenyekiti, Mwanasheria Raymond Wawa imekubali shauri hilo kurejea kwenye Kamati...

 

10 months ago

Michuzi

MANARA APELEKWA KAMATI YA MAADILI YA TFF

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Baada ya kutoa kauli zisizo nzuri kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) na kuitupia shutuma mbalimbali hatimaye kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho hilo limefanya maamuzi ya kumfikisha Msemaji wa Simba Hajji Manara mbele ya kamati ya maadili.
TFF imeweka wazi kuwa kila mwanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania analazimika kuheshimu na kufuata kanuni za maadili za shirikisho kama zilivyoainishwa kwenye kanuni zake mbali mbali.
Katika Mkutano wa klabu ya...

 

3 weeks ago

Michuzi

KAMATI YA MAADILI TFF YAMUADHIBU MJUMBE BODI YA LIGI

Na Agness Francis Globu ya jamii.
KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imemfungulia mashitaka Mwenyekiti wa Abajalo FC na Mjumbe wa Bodi ya Ligi Edgar Chibula kwa tuhuma ya kuikashifu na kuidhalilisha Kamati ya Bodi ya Ligi ya TFF katika vyombo vya  Habari ambapo ni kinyume na sheria. 
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,Ofisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema kuwa  Chibura alishitakiwa Februari 28 mwaka huu kwa kosa la  kuzungumza maneno yasiofaa kwa...

 

2 years ago

Michuzi

KAMATI YA MAADILI YA TFF YATUPILIA MBALI KESI YA JERRY MURO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KAMATI ya maadili ya TFF imetupilia mbali shauri la Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanga Jerry Muro baada ya kuona mapungufu kibao kwenye barua ya wito pamoja na kushindwa kuanbatanisha sababu za kuitwa kwake, na katika.barua ya Juni 29 Muro alitumiwa wito wa kuitwa kwenye kamati ambayo haikuwekwa wazi ni kamati gani pia hakukuwa na viambatanisho vyovyote vya mashataka dhidi yake kitu kilichopelekea kutupiliwa mbalo.
Mwenyekiti wa Kamati ya...

 

2 years ago

MillardAyo

AUDIO: Kauli ya Jerry Muro baada ya kuishinda TFF katika kamati ya maadili

01 (1)

July 1 2016 taarifa za mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Jerry Muro kuitwa na kamati ya maadili kujieleza kutokana na kauli zake, iliingia kwenye headlines kabla ya leo July 2 kuitikia wito, baada ya kamati kuona Jerry hana cha kujibu na barua kuwa iliandikwa kimakosa, Jerry Muro alifunguka haya. […]

The post AUDIO: Kauli ya Jerry Muro baada ya kuishinda TFF katika kamati ya maadili appeared first on MillardAyo.Com.

 

2 years ago

Dewji Blog

Kamati ya Maadili ya TFF kukaa leo kuamuru hatma ya Hafisa Habari wa Yanga, Jerry Muro

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajiwa kuwa na kikao chake leo Jumamosi ya Julai 2, 2016 kwenye ukumbi wa ofisi za TFF zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, makutano ya barabara za Shaurimoyo na Uhuru, Ilala jijini Dar es Salaam.

Viongozi watatu kutoka wanachama wa TFF wanahitajika kufika kwenye kikao hicho kinachotarajiwa kuanza saa 4.30 asubuhi.

Viongozi hao ni Jerry Muro – Msemaji wa Young Africans S.C (Pichani chini)
Nassib Mabrouk – Katibu...

 

2 years ago

Michuzi

Kamati ya Maadili TFF Yamfungia Jerry Muro, Kutojishughulisha na maswala ya soka kwa Mwaka Mmoja

MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro (pichani) amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka pamoja na kutozwa faini ya Sh. Milioni 3, baada ya kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kilichokaa leo kwenye Makao Makuu ya Shirikisho hilo, chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Wilson Ogunde 
Muro amefungiwa baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka mawili kati ya matatu yaliyowasilishwa na TFF mbele ya Kamati ya hiyo, ambayo ni...

 

3 years ago

Tanzania Daima

Watuhumiwa kujipatia mil. 128 kwa udanganyifu waachiwa huru

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru watu wawili waliokuwa wakikabiliwa na kosa la kujipatia sh milioni 128.3 kwa njia ya udanganyifu pamoja na kuingilia mawasiliano ya mtandao wa simu....

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani