TPDC Kusambaza Gesi Asilia Kwa Kushirikiana na Sekta Binafsi


Na: Frank Shija – MAELEZO.

TPDC kwa kushirikiana na Sekta binafsi wanatarjia kutekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji wa gesi asilian katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na baadhi ya mikoa mingine itakayoidhinishwa.

Hayo yamebainishwa na Kiamu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Musomba amesema kuwa miradi hiyo imeanza kwa kupitia upya taarifa ya awali ya upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba la kusambazia gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo mnamo mwezi machi 22, 2017 TPDC ilikaribisha jumla ya makampuni 9 ambayo yalikidhi vigezo vya kimanunuzi kwa ajili ya kazi hiyo.

“Napenda kuutaarifu umma kuwa TPDC inatarajia kutekeleza miradi mbaimbali ya usambazaji wa gesi asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Bagamoyo na Mkuranga Mkoani Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na baadhi ya mikoa mingine,” alisema Mhandisi Muyomba.

Aliongeza kuwa lengo la kupitia upya taarifa za awali ni kuboresha zaidi taarifa za kifedha, mahitaji ya kiufundi na utambuzi wa njia za kupitisha bomba na ugawaji wa kanda za usambazaji.

Aidha alisema kuwa ili kuharakisha usambazaji wa gesi, TPDC inakaribisha na kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika uendelezaji wa miundombinu itakayowezesha usambazaji wa gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam mara tu mapitio ya upembuzi yakinifu utakapomalizika.

Mtandao huo unakadiriwa kuwa na urefu wa takribani kilomita 65 ambao utahudumia, kwa kuanzia, nyumba 30,000, viwanda na vituo vya kushindilia gesi asilia pamoja na vituo vya kujazia gesi hiyo.

Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema kuwa hadi sasa TPDC imefanikiwa kukiunganisha na mtandao wa gesi asilia Kiwanda kimoja cha kutengeneza Vigae cha Goodwill kilichopo Mkuranga, Mkoani Pwani huku likiendelea na majadiliano na viwanda vingine vitatu kwa ajili ya kuunganishwa na mtandao huo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 TPDC inatambuliwa kuwa Shirika rasmi la taifa linalojiendesha kibiashara, ambapo sheria hii inaipa mamlaka TPDC kuruhusu makampuni mbalimbali kuendesha shughuli za sekta, zitakazokuwa zainadhibitiwa kwa utaratibu maalum chini ya usimamizi wa Mdhibiti anayetoa leseni. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uunganishwaji na usambazaji wa gesi asilia leo Jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uunganishwaji na usambazaji wa gesi asilia leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusinano na Mipango wa TPDC, Nathan  Mnyawami. 
Baadhi ya waaandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba (hayupo pichani) uliofanyika Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO. 

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Michuzi

TPDC YAPONGEZWA KWA KUTOA MAFUNZO YA MASUALA YA MAFUTA NA GESI ASILIA KWA WAANDISHI WA HABARI

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh. Gabriel Fabian Daqarro amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kuendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa Habari wa Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
Mh. Gabriel Daqarro ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ambayo yamefanyika Septemba 19 katika ukumbi wa Chuo cha Afya CEDHA mkoani Arusha.


“Ingawa mafunzo ni mafupi lakini napenda kulipongeza Shirika letu la Mafuta la Taifa kwa kuona umuhimu wa vyombo vya...

 

2 years ago

Michuzi

TPDC yatoa elimu ya uelewa kwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara juu ya gesi asilia

TPDC imefanya kikao kazi na Madiwani na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kwa lengo la kutoa elimu juu ya sekta ndogo ya gesi. Kikao hicho kimefanyika katika kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo Madimba, Mkoani Mtwara. Aidha katika kikao hicho TPDC imewataka Madiwani kusimamia zoezi la ulinzi shirikishi katika mitambo ya Madimba na katika maeneo linapopita bomba la gesi asilia. 

 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Fatma Ally (mwenye mtandio mwekundu) akipata maelezo kuhusu kiwanda...

 

2 years ago

Channelten

Serikali inakusudia kutumia zaidi ya shilingi bilion 400 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya kusambaza gesi asilia

g3-1

Serikali inakusudia kutumia zaidi ya shilingi bilion 400 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya kusambaza gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na viwandani kwenye mikoa ya Mtwara, Lindi na Dar es salaam.

Kwa sasa Serikali ipo kwenye mchakati wa kutafuta fedha hizo, kwa ajili ya kugharamia Usambazaji huo, ambap tayari Benki ya Maendeleo ya Afrika imeshaonesha nia ya kutoa sehemu ya fedha zinazohitajika.

Hayo yamebainishwa leo  na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli...

 

2 years ago

Michuzi

TPDC: Gesi asilia ipo na ziada

Mkurungezi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. James Mataragio, amesema hali ya uzalishaji wa gesi asilia nchini ni nzuri, alieleza kuwa mitambo ya kuchakata gesi asilia kule Madimba Mkoani Mtwara na Songo Songo Mkoani Lindi inao uwezo wa kuzalisha futi za ujazo milioni 240 za gesi asilia, huku gesi anayo tumika ikiwa futi za ujazo milioni 146 za gesi asilia. 
Dk. Mataragio ameongeza kuwa mchanganuo huo wa uzalishaji wa gesi unazidi mahitaji yetu kwa sasa na hivyo...

 

3 years ago

Michuzi

BODI YA TPDC YAKAMILISHA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA

Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti wake Bw. Michael Mwanda, imekamilisha ziara ya kukagua miundombinu ya kuchakata gesi asilia na bomba la gesi asilia katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es salaam. Katika ziara hiyo Bodi ya TPDC ilipata fursa ya kujionea na kufanya ukaguzi wa hatua za mwisho za ujenzi wa miundombinu hiyo.Moja ya kisima gesi asili kinacho endelea kufanyiwa utafiti, kilichopo kisiwa cha Songo Songo ambacho kinacho endeshwa na...

 

3 years ago

Michuzi

TPDC YAOMBA TOZO EWURA KUSAFIRISHA GESI ASILIA

Na Beatrice Lyimo- Maelezo.
GESI asilia ni bidhaa muhimu kwa maendeleo ya wananchi na uchumi wa nchi yeyote ikiwemo Tanzania.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Said Meck Sadick wakati wa ufunguzi wa taftishi juu ya maombi la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu mapendekezo ya tozo ya uchakataji na usafirishaji wa Gesi asilia uliofanyika.
Mhe. Sadick amesema  kuwa, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea maombi ya Shirika la...

 

1 year ago

Malunde

TPDC,DANGOTE WAKUBALIANA BEI YA MAUZO YA GESI ASILIA

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limefikia makubaliano na Kampuni ya Dangote Group of Industries kuhusu bei ya mauzo ya gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya kiwanda chake cha saruji kilichopo mkoani Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Kapulya Musomba alisema makubaliano hayo yanahusu kuunganisha miundombinu ya kusafirisha gesi asilia kutoka kwenye bomba kubwa kwenda kiwandani hapo na kukamilisha mkataba wa awali kwa...

 

1 year ago

Channelten

Miundombinu ya Gesi Asilia TPDC yawataka wananchi kuwa walinzi

g3-1-1024x682

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania-TPDC limewataka wananchi wanaopitiwa na miundombinu ya kusafirishia gesi asilia, kuhakikisha wanakuwa walinzi wa rasilimali hiyo ya Taifa, kwa kutojihusisha na uchimbaji wa mchanga au shughuli yeyote itakayo athiri bomba hilo lenye urefu wa kilometa 548.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania-TPDC Mhandisi KAPUULYA MUSOMBA wakati kukabidhi hundi ya shilingi milion kumi kwa wananchi wa serikali ya Mtaa...

 

2 years ago

Michuzi

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI DK. MHANDISI JULIANA PALLANGYO AKUTANA NA WATENDAJI KUTOKA TPDC KWA AJILI YA KUJADILI MATUMIZI YA GESI ASILIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk. James Mataragio (mbele) akielezea mikakati ya shirika hilo katika matumizi ya gesi asilia inayozalishwa kwa ajili ya matumizi ya majumbani na nyingine kuuzwa katika soko la nje katika kikao kilichokutanisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili matumizi ya...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani