TRENI YA TANZANIA HADI RWANDA KUTUMIA UMEME


RWANDA na Tanzania zimekubaliana kujenga reli ya kisasa (SGR) ya umeme kutoka Isaka, Kahama mkoani Shinyanga hadi Kigali, Rwanda badala ya ile ya awali iliyokuwa iwe ya kisasa lakini yenye kutumia nishati ya dizeli.
Wataalamu wanasema treni ya umeme ni bora zaidi lakini pia ni rafiki wa mazingira ikilinganishwa na treni inayotumia dizeli. Wakati wa mkutano wao wa pili mjini Kigali, Mawaziri wa usafirishaji wa nchi zote mbili, waliagiza Shirika la Maendeleo ya Usafirishaji la Rwanda (RTDA) na Kamati ya Pamoja ya Ufuatiliaji (JTMC) kupitia upya upembuzi yakinifu kwa niaba ya nchi zote mbili kabla ya kuanzisha Kitengo cha Utekelezaji Mradi (PIU).
Waziri wa Nchi wa Rwanda (Usafirishaji), Jean de Dieu Uwihanganye na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania, Profesa Makame Mbarawa, mwishoni mwa wiki walisaini tena makubaliano mengine ya utekelezaji wa mradi huo. Muda uliopangwa kuanza kwa ujenzi wa reli hiyo itakayounganisha Bandari ya Dar es Salaam na Kigali, umebaki kuwa Oktoba, 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusainiwa makubaliano hayo, Uwihanganye alisema mabadiliko hayo yametokana na ukweli “tunataka kupunguza muda na gharama za usafirishaji wa abiria na bidhaa kati ya Dar es Salaam na Kigali na kuiboresha reli hiyo. Hiyo ndiyo sababu ya kupitiwa upya kwa upembuzi yanikifu.” Profesa Mbarawa alisema serikali zote mbili zitapitia upembuzi huo baada ya taratibu za manunuzi na huenda ikawa ndani ya mwezi mmoja.
Katika mpango wa kutumia treni ya umeme, treni ya abiria itakuwa ikisafiri kwa mwendokasi wa Kilometa 160 kwa saa na ile ya mizigo itakuwa ikisafiri kwa mwendokasi wa Kilometa 120 kwa saa,” alisema Profesa Mbarawa. Imeelezwa kuwa umbali kati ya Dar es Salaam na Kigali ni Kilomita 1,320. Hivyo, kwa mabadiliko hayo, inaweza kuchukua saa 15 kwa mzigo kusafirishwa kutoka Dar es Salaam hadi Kigali wakati abiria wakitumia saa 10 kusafiri.
Aidha, reli hiyo ya kisasa kutoka Bandari ya Dar es Salaam hadi Kigali inatarajiwa kugharimu Dola za Marekani zipatazo bilioni 2.5 (Sh trilioni 5.5 za Tanzania). Imeelezwa kuwa Tanzania itachangia dola bilioni 1.3 wakati Rwanda itachangia dola bilioni 1.2. Waziri Mbarawa na ujumbe wake walikuwa nchini Rwanda kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na walirudi nchini juzi jioni. Unafuu wa bidhaa Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya uchumi, reli ya kisasa inayotarajiwa kujengwa na kuziunganisha Tanzania na Rwanda itapunguza sana gharama za usafirishaji mizigo.
Kwa Rwanda inakadiriwa kuwa reli itakapoanza kutumika itapunguza gharama za usafirishaji kwa wastani wa Dola za Marekani 1,500 (Sh milioni 3.3 za Tanzania) kwa kila kontena, hivyo kuleta unafuu wa bidhaa kwa watumiaji. Kwa sasa, Rwanda inakadiriwa kusafirisha tani 950,000 za mizigo kwa mwaka kiasi ambacho kitapaa zaidi reli ya kisasa itakapoanza kazi. Uganda inanufaika pia kwa barabara lakini pia kwa usafiri wa majini kwa kupitishia mizigo yake Ziwa Victoria, Mwanza ambako mizigo hufikishwa kwa treni inayotoka Dar es Salaam.
Wasafirishaji wa mizigo wa Rwanda wanasema kwa wastani, huwagharimu Dola za Marekani 4,990 (Sh milioni 11 za Tanzania) kusafirisha kontena la urefu wa futi 20 wakati katika nchi nyingine na Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa kontena la aina hiyo, gharama yake inakadiriwa kuwa Dola 2,504 (Sh milioni 5.5 za Tanzania). Hata hivyo, Waziri Uwihanganye amesema kwa sasa gharama ya kusafisha kontena moja kati ya Kigali na Dar es Salaam ni wastani wa Dola za Marekani 3,912 (Sh milioni 8.6 za Tanzania).
Alipotakiwa kulinganisha umbali kati ya Dar es Salaam-Kigali upande wa Korido ya Kati na ile ya Korido ya Kaskazini, Mombasa-Kampala-Kigali, Kayitakirwa alisema; “Ya Kaskazini ni ndefu, kilometa 1,661 na ina mipaka miwili ya kuvuka tofauti na Korido ya Kati inayolazimu kupita mpaka mmoja wa Rusumo, tena umbali ni kilometa 1,495 tu.” Kwa mujibu wa Shirika la Taifa la Takwimu la Rwanda, bandari ya Dar es Salaam ndiyo inayotumika kupitisha mizigo mingine ya Rwanda kwa zaidi ya asilimia 80, wakati ile ya Mombasa mizigo ni wastani wa asilimia 20 na 30.
Theodore Murenzi, dereva na mmoja wa wasafirishaji wa mizigo wa Rwanda, anasema malori kati ya 200 na 250 huvuka mpaka wa Rusumo kuingia au kutoka Rwanda na Tanzania kila siku. Tayari Rwanda imeanza kujenga vituo kadhaa vikubwa vya stesheni za reli nje ya Jiji la Kampala. Stesheni kubwa ya abiria inajengwa Ndera, wilayani Gasabo wakati ile ya mizigo inajengwa Masaka, wilayani Kicukiro.
Chanzo- Habarileo

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

11 months ago

Mwananchi

Tanzania kama Ulaya, treni ya umeme kupunguza safari

Treni ya umeme inayotarajiwa kuanza kazi baada ya miezi 30 nchini itakuwa ya pili Afrika itakayosafiri kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa, baada ya ile ya nchini Morocco.

 

1 year ago

MillardAyo

‘Hadi sasa Tanzania tunanunua umeme toka Uganda, Zambia na Kenya’ – Prof. Muhongo

Ni waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo akiongelea yaliyozungumzwa kwenye kikao cha ushirikiano wa nchi za Afrika Mashariki ambao lengo lake ni kusaidia nchi hizi kupata umeme mwingi wa uhakika na wa bei nafuu. ‘Sasa ili tuyapate hayo matatu tunalazimika kuwa kama nchi nyingine duniani ambazo zinauziana umeme, ndugu zangu Watanzania hadi sasa […]

The post ‘Hadi sasa Tanzania tunanunua umeme toka Uganda, Zambia na Kenya’ – Prof. Muhongo appeared first on...

 

2 years ago

Michuzi

SYMBION POWER YAWA YA KWANZA KUTUMIA GESI KUTOKA MTWARA KUZALISHA UMEME KWA KUTUMIA BOMBA JIPYA LA KM 487 MJINI DAR ES SALAAM

  DAR ES SALAAM, Tanzania. Tarehe 21 Septemba 2015 -- Symbion Power yenye tawi lake maeneo ya Ubungo leo imetangaza kuwa imefanikiwa katika majaribio ya kutumia gesi asilia katika mitambo yake . Gesi inapatikana  Ghuba ya  Mnazi iliyo karibu na Mtwara Kusini mwa Tanzania. 
Kwa zaidi ya Mwaka mmoja sasa ; Mitambo hii yenye uwezo wa kuzalisha kiasi cha Megawati 120 haikuweza kufanya uzalishaji wowote kutokana na ukosefu wa gesi asilia kama chanzo cha nishati Tanzania


“Kwa mara nyingine Symbion...

 

2 years ago

Michuzi

UONGOZI WA KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL) LASITISHA HUDUMA YA TRENI YA JIJI MAARUFU KAMA TRENI YA MWAKYEMBE.

Shimo katika tuta la reli  eneo la Buguruni kwa Mnyamani  ambalo limesababishwa na mvua inayoendelea kunyesha hapa nchini ambapo ukarabati wa eneo hilo unaendelea ili kufanikisha usafiri kurejea hapo kesho.

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL) Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa huduma ya treni ya jiji maarufu kama Treni ya Mwakyembe awamu ya jioni ya leo Februari 09, 2016. 
Taarifa imefafanua kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na maji ya mvua kuchimba shimo kubwa...

 

3 years ago

BBCSwahili

Treni ya umeme yaanza kutumika Ethiopia

Wasafiri jijini Addis Ababa wamejawa na msisimko baada ya kuzinduliwa kwa treni ya umeme ya kubeba abiria mijini humo.

 

1 year ago

Dewji Blog

Serikali kununua treni ya umeme mwakani

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imepanga kununua treni ya umeme inayotarajiwa kuwasilini nchini mwezi Juni, 2017.

Treni hiyo inatarajiwa kufanya safari katika jiji la Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema serikali inauwezo wa kutekeleza ahadi hiyo kwa kuwa fedha za kununulia treni hiyo zipo.

Pia Magufuli amesema serikali iko katika harakati za uboreshaji na ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri, ikiweno ujenzi wa reli za kisasa kuanzia Dar es Salaam, Mwanza na nchi...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Treni ya umeme inakuja july 2017

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imepanga kununua treni ya umeme inayotarajiwa kuwasilini nchini mwezi Juni, 2017.

Treni hiyo inatarajiwa kufanya safari katika jiji la Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema serikali inauwezo wa kutekeleza ahadi hiyo kwa kuwa fedha za kununulia treni hiyo zipo.

Pia Magufuli amesema serikali iko katika harakati za uboreshaji na ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri, ikiweno ujenzi wa reli za kisasa kuanzia Dar es Salaam, Mwanza na nchi...

 

11 months ago

Mwananchi

Gwajima ajipanga kununua treni ya umeme

Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema amedhamiria kununu treni ya umeme  baada ya Rais John Magufuli kuonyesha dhamira ya kujenga reli  ya kisasa(standard gauge).

 

3 years ago

Michuzi

Treni ya abiria imeahirishwa kuondoka hadi kesho Januari 14, 2015

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kuwataarifu wananchi na abiria waliokuwa wasafiri na treni ya leo kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi kesho saa 11 jioni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa safari hiyo ni ajali ya treni ya mizigo iliyotokea leo Jumanne Januari 13, 2015 saa 9 alasiri maeneo ya Stesheni ya Pugu Mpiji ambapo mabehewa matatu ya treni ya mizigo iliyokuwa inasafiri kwenda Bara yaliacha njia na moja kuanguka...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani