TUNDU LISSU AFICHUA KILICHOCHELEWESHA BOMBADIER KUFIKA

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amedai kuwa ndege aina ya Bombardier Q 400-Dash 8 iliyonunuliwa na Serikali, imezuiwa nchini Canada kutokana na Serikali kudaiwa fidia.
Ndege hiyo ilitakiwa iwasili nchini mwezi uliopita, lakini hadi sasa hakuna taarifa kuhusu ujio wake.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Lissu aliyekuwa ameongozana na Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema na Frederick Sumaye (mwenyekiti wa Kanda ya Pwani), alisema ndege hiyo inashikiliwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd inayoidai Serikali dola 38.7milioni sawa na Sh87bilioni.
Alisema kutokuja kwa ndege hiyo kama ilivyopangwa licha ya kukamilika, kunatokana na maamuzi yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Nne, wakati huo Rais John Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi, wa kuvunja mkataba wa kampuni hiyo ya Canada iliyokuwa ikijenga barabara ya Tegeta Wazo-Bagamoyo.
Lissu, ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki, alisema baada ya uamuzi huo, Stirling ilifungua kesi Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi, ikidai kukiukwa kwa mkataba na ilipofika Juni 2010, mahakama hiyo ilitoa tuzo ya ushindi kwa kampuni hiyo, ikiitaka Serikali ilipe fidia ya dola 25 milioni za Kimarekani, huku deni hilo likiwekewa riba ya asilimia nane.
Kwa madai ya Lissu, Serikali ilikataa kulipa fidia hiyo hadi Juni 30 mwaka huu wakati mahakama hiyo ilipoipa Stirling kibali cha kukamata mali zote za Tanzania zitakazokuwa katika nchi za Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ubelgiji, Uganda na Canada.
Lissu ameibua tuhuma hizo miezi mitatu baada ya Serikali kutangaza kuwa ndege hiyo mpya ingewasili Julai.
Akizindua safari za Kampuni ya Usafiri wa Anga la Tanzania (ATCL), Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani alisema ndege hiyo aina ya Bombadier Dash 8-Q 400 imenunuliwa kuimarisha huduma za shirika hilo la Serikali.
Alisema hatua hiyo itaiweza ATCL kufikisha ndege nne na hivyo kupanua mtandao wa huduma zake na kufikia masoko ya nchi jirani kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Lakini kutowasili kwa ndege hiuyo kumeibua maswali na katikati ya wiki, mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe aliandika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii akihoji mustakabali wa chombo hicho cha usafiri wa anga.
Chini ya swali hiyo, mchangiaji anayeonekana kwa jina la Mbarawa amejibu kuwa kulikuwa na matatizo kidogo yaliyochelewesha na kuahidi kuwa ndege hiyo itawasili mapema.
Akizungumzia suala hilo, Lissu alidai kuwa hata Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Augustine Mahiga alienda Canada kushughulikia suala hilo.
“Waziri Mahiga akatae kama hakuwa Canada Agosti 3 mwaka huu kimyakimya katika mkutano wa maridhiano na kampuni hiyo ili waachie ndege iletwe Tanzania. Wameikamata hadi wapewe dola 12.5milioni,”alisema Lissu.
Alipoulizwa kuhusu madai ya kushikiliwa kwa ndege hiyo, Ngonyani alisema anachofahamu makubaliano ya manunuzi na kampuni inayotengeneza hiyo yamekwamishwa na ratiba za kampuni hiyo yenye zabuni nyingi za kuzalisha ndege.
“Mimi sina taarifa ya kushikiliwa kwa ndege hiyo, ila ninachojua ndege itakuja. Katika makubaliano ilitakiwa ifike Julai, lakini ratiba zao kwa miezi miwili ijayo hadi Oktoba, ndege itakuwa tayari na itakuwa imeshakamilika,” alisema.
“Unajua Bombardier sasa hivi kwenye soko la ndege ndiyo ‘talk of the day (gumzo). Nchi nyingi zinahitaji, kwa hiyo oda ni nyingi na foleni inakuwa kubwa.
“Lissu ni mwanasiasa anayeweza kuzungumza lolote, ila ukweli utajulikana baadaye. Wasipoleta watakuwa wame-breach contract (wamekiuka mkataba) na sidhani kama watafanya hivyo maana wana kazi zetu nyingi.”
Alipoulizwa kuhusu maagizo ya mkataba wake, alisema kwa sasa yuko nje ya ofisi na asingeweza kueleza kwa undani makubaliano ya mkataba huo katika masharti na muda wa matengenezo itakuwaje.
“Hapa sina details zake, nikirudi kutoka safari nitafute,” alisema.
Kuhusu madai ya kampuni hiyo ya Stirling, Ngonyani alisema serikali kudaiwa si jambo la kushangaza. Alisema tangu Serikali ilipoingia madarakani mwaka 2015, wizara hiyo ya ujenzi ilikuwa inadaiwa Sh1.12 trilioni, lakini hadi Julai, tayari limepungua hadi Sh900 bilioni.
“Mimi sina taarifa kuhusu deni hilo ila kikubwa Serikali kudaiwa si big deal (jambo la kushangaza), ila tunafanyaje katika kuyalipa madeni, pengine inawezekana deni hilo likawa ni sehemu ya madeni tunayodaiwa,” alisema.

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

6 months ago

Malunde

MCHUNGAJI PETER MSIGWA AMPA MAKAVU MBUNGE MSUKUMA KUHUSU TUNDU LISSU,BOMBADIER

Mbunge wa Iringa mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa ameibuka na kumchana Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku 'Msukuma' na kusema uelewa wake juu ya hoja za Mwanasheria Tundu Lissu ni mdogo sana.
Msigwa amesema haya siku moja baada ya Mbunge Msukuma kudai kuwa yeye anaunga mkono kauli ya serikali kuhusiana na wanasiasa kuchochea sakata la ndege huku akiwatuhumu kuwa wapinzani wanatafuta kiki na kusema ni waongo watupu.
"Msukuma anasukumwa na uelewa Mdogo wa mambo ya...

 

4 months ago

Malunde

KAKA WA TUNDU LISSU AFUNGUKA ALICHOKIONGEA TUNDU LISSU BAADA YA KUTOKA ICU

Kaka wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Alute Mughwai ameeleza jinsi alivyomtoa mdogo wake chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na kile ambacho alikisema mara tu baada ya kutoka ndani kwa mara ya kwanza.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano, Alute amesema Lissu mara baada ya kutoka si yeye pekee alifurahi hata ndugu zake waliokuwapo walifurahia tukio hilo.
“Manesi walipanga kumtoa nje Jumamosi (Oktoba 14) na kwa kuwa Lissu alijua tunakwenda, aliwaeleza wasimtoe wasubiri ndugu zake...

 

6 months ago

Malunde

MSUKUMA AMLIPUA TUNDU LISU....ADAI ANATAFUTA KIKI TU MAMBO YA BOMBADIER

Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Msukuma amefunguka na kusema kuwa Rais Magufuli hausiki katika sakata la kuvunja mkataba ambao umepelekea ndege ya Tanzania  Bombadier Q-400 Dash 8 kushikiliwa nchini Canada na kusema wapinzani wanatafuta kiki.
Mbunge Msukuma amesema kwa upeo wake jinsi alivyosikiliza upande wa upinzani na majibu ya serikali anaona wazi kuwa ni kweli baadhi ya wapinzani wa nchii hii wanahusika katika kukwamisha jambo hilo kama ambavyo serikali ilivyosema na kudai Rais...

 

1 month ago

Zanzibar 24

Vicent Lissu azungumzia hali ya Tundu Lissu nchini Ubelgiji

Ndugu wa Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, ambaye anaendelea na matibabu nchini Ubelgiji, Vicenti Mughwai alisema jana kuwa afya ya kaka yake Lisu  inazidi kuimarika na sasa anaweza kufanya mambo mengi mwenyewe ikiwamo kwenda kuoga na kutembea kwa kutumia magongo. Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), alipelekwa Ubelgiji Januari 7, mwaka huu, akitokea Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alipokuwa akipatiwa matibabu tangu Septemba 7, mwaka jana...

 

5 months ago

Malunde

MKE WA TUNDU LISSU AFUNGUKA KWA MARA KWANZA....DEREVA WA LISSU ASEMA HANA KUMBUKUMBU TUKIO LA KUPIGWA RISASI

Nairobi. Kwa mara ya kwanza, Alicia Magabe ambaye ni mke wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia tukio la mumewe kushambuliwa kwa risasi na kudokeza kwamba haliwezi kuwa limetokana na sababu nyingine isipokuwa kazi ambazo amekuwa akizifanya.
Pia amezungumzia kuhusu afya yake na kueleza kuwa bado siyo nzuri na kuwaomba Watanzania waendelee kumuombea.
Mbali ya Alicia ambaye pia ni mwanasheria, dereva wa Lissu naye amezungumza akisema ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na...

 

4 years ago

GPL

Tundu Lissu…

Tundu Lissu. Na Saleh Ally
Yanga damu aliyevuliwa viatu na mashabiki wa Simba SC
MMOJA wa wanasiasa machachari nchini ni Tundu Lissu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), amekuwa akitajwa karibu kila sehemu yanapozungumziwa masuala mbalimbali yanayohusiana na siasa hapa nchini kutokana na umaarufu alionao.… ...

 

1 year ago

Mtanzania

‘Tundu Lissu mgongwa’

Tundu Lissu

Tundu Lissu

* Aenda kutibiwa nchini Ujerumani, Mahakama yaonya

NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

WADHAMINI wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), wameonywa na mahakama kwa kushindwa kuhakikisha mshtakiwa anafika mahakamani siku ya kesi, huku ikielezwa mshtakiwa huyo ni mgonjwa.

Kutokana na hali hiyo ilielezwa mahakamani hapo kuwa, mbunge huyo ni mgonjwa na amekwenda nchini Ujerumani kwa ajili ya matibabu.

Hatua hiyo iliifanya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi...

 

1 year ago

MwanaHALISI

Tundu Lissu akamatwa

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, anaandika Josephat Isango. “Nashikiliwa na polisi hapa Kituo Kikuu kutokana na ile press conference (mkutano na waandishi wa habari) kuhusu kupotea kwa Ben Saanane,” alimweleza mwandishi wa ...

 

1 year ago

TheCitizen

Tundu Lissu arrested

The Chief Whip of the Official Opposition Camp and Singida East MP, Mr Tundu Lissu (Chadema) was on Monday evening arrested outside the National Assembly grounds and has been taken to Dar es Salaam allegedly to answer unspecified charges.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani