UBALOZI WA NORWAY WAIPATIA UN TANZANIA DOLA MILIONI 5.1 KUFANIKISHA MPANGO WA UNDAP II


Ubalozi wa Norway nchini umeipatia msaada wa dola bilioni 5.1 Umoja wa Mataifa Tanzania ili kusaidia kufanikisha Mpango wa Misaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II).

Makubaliano hayo yamesainiwa na Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez katika ofisi za ubalozi wa Norway uliopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balozi Kaarstad alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo inatolewa na Norway ili kufanikisha mpango wa UNDAP II ambapo kwasasa imefika dola milioni 10.5 na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali na UN katika mpango huo.Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa Umoja wa Mataifa Tanzania. (Picha zote na Rabi Hume)
"Lengo la msaada huu ni kuwasaidia wakimbizi waliopo Kigoma na kwa wananchi wa Kigoma kwa ujumla, makubaliano mapya tuliyosaini leo yanalenga maeneo yaliyokusudia. Kusaidia kilimo ili kuwezesha kuwepo chakula cha kutosha kwa ajili ya wakimbizi na wananchi wanaozunguka hayo maeneo ya kambi,
"Sehemu nyingine ambayo msaaada huu unalenga, ni kusaidia ni kumaliza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto. Matumaini yetu msaada huu utafungua milango kwa washirika wengine wa maendeleo kuchangia ili kufanikisha mapango huu," alisema
Naye Rodriguez aliushukuru Ubalozi wa Norway kwa msaada waliowapatia na kwa serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao inautoa kwa Umoja wa Mataifa ili kufanikisha mpango huo.Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez akizungumza kuhusu msaada ambao wameupokea kutoka Ubalozi wa Norway.
Rodgriguez alisema msaada huo utatumika kama ulivyopangwa kwa wakimbizi na wananchi waliopo mkoa wa Kigoma kwa kuhakikisha kunakuwa na chakula cha kutosha kwa wakimbizi wote wanaokadiriwa kufikia 340,000, lakini pia kuhakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia kwa watu wote.
"Kwa miongo mingi, Norway imeendelea kuwa mshirika wa kuaminika kwa Tanzania na Umoja wa mataifa. Kwa kuweka mkazo katika mahitaji ya wanawake na watoto walio hatarini, rasilimali hizi zitatoa mchango muhimu katika kukidhi mahitaji ya wenye uhitaji mkubwa kama ilivyoelezwa katika Malengo ya Dunia." alisema Rodriguez.Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez na Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad wakisaini makubaliano ambayo yatawezesha Norway kuongeza dola milioni 5.1 katika makubaliano ya Mpango wa Misaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II).

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

3 months ago

Michuzi

Ubalozi wa Norway waipatia UN Tanzania dola milioni 5.1 ili kufanikisha UNDAP II

Ubalozi wa Norway nchini umeipatia msaada wa dola bilioni 5.1 Umoja wa Mataifa Tanzania ili kusaidia kufanikisha Mpango wa Misaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II). Makubaliano hayo yamesainiwa na Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez katika ofisi za ubalozi wa Norway uliopo jijini Dar es Salaam. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balozi Kaarstad alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada...

 

8 months ago

Michuzi

NORWAY YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA DOLA MILIONI 10.5 KUBORESHA ELIMU


Benny Mwaipaja, WFM, DAR ES SALAAM
SERIKALI ya Norway imeipatia Tanzania msaada wa Dola Milioni 10.5 za Marekani kupitia programu ya miaka mitatu ya maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, inayotarajiwa kuanza Mwaka Mpya wa Fedha- Julai Mosi mwaka huu.
Mpango huo pamoja na uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta ya Mafuta, umezinduliwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango na Kaimu Katibu Mkuu...

 

4 months ago

Michuzi

Ubalozi wa Norway nchini Tanzania wachangia Milioni 300 Sauti za Busara 2018

Balozi wa Norway nchini Tanzania kupitia kwa Balozi wake Balozi Bi. Hanne-Marie Kaarstad leo wameweza kutiliana saini mkataba wa udhamini wa donge nono la kiasi cha Dola 128200(USD) ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania Milioni 300, ambazo zitaenda kusaidia Shirika lisilo la Kiserikali la Busara Promotion kwa ajili ya tamasha la Sauti za Busara 2018. Halfa hiyo ya kutiliana saini imefanyika mapema leo Novemba 2,2017 katika Ubalozi wa Taifa hilo la Norway, Jijini Dar es Salaam na...

 

3 years ago

Habarileo

Ubalozi wa China nchini waipatia TSN kompyuta 15

UBALOZI wa China nchini umetoa msaada wa kompyuta 15 kwa Kampuni ya Magazeti ya Tanzania Standard Newspapers (TSN), ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kuboresha mradi wa elimu unaotekelezwa TSN, wachapishaji wa gazeti hili na magazeti dada ya Daily News, Sunday News, HabariLeo Jumapili na SpotiLeo.

 

2 years ago

Dewji Blog

UN yazindua sehemu ya pili Mpango wa Misaada ya Maendeleo (UNDAP 2)

Katika kuendeleza juhudi zake za kusaidia mataifa wanachama, Umoja wa Mataifa (UN) umezindua mpango mpya wa misaada ya maendeleo nchini (UNDAP 2) baada ya mpango wa kwanza wa UNDAP 1 kukamilika kwa mafanikio makubwa na hivyo kuzinduliwa mpango mpya ambao utaendeleza hatua uliyoishia mpango wa kwanza.

Katika mpango huu mpya UN inataraji kutoa kiasi cha Dola Bilioni 1.3 ambazo zitatumika katika kuboresha kusaidia kukuza uchumi na upatikanaji wa ajira, kuboresha huduma zinazopatikana katika...

 

2 years ago

Mwananchi

Norway: Tanzania isiige mpango wa gesi kutoka nchi nyingine duniani

Ushirikiano baina ya Tanzania na Norway umedumu kwa zaidi ya miaka 50 na kwa muda mrefu, ulikuwa umeegemea kwa Tanzania kupewa mikopo na taifa hilo la ukanda wa Scandinavia.

 

2 years ago

Michuzi

MGODI WA BULYAHULU WAIPATIA MSALALA ZAIDI YA MILIONI 700 KWA AJILI YA USHURU WA HUDUMA

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akikabidhi hundi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Patrick Karangwa,ikishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa(katikati)Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mgodi wa BulyanhuluMkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Vita Kawawa akizungumza wakati wa ziara yake katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ambapo amesisitiza kuwa kodi ya ushuru wa huduma...

 

12 months ago

Zanzibar 24

SIGHTSAVERS waipatia Wizara ya Afya Mashine ya uchunguzi wa uwoni Yenye thamani ya Shilingi zaidi ya Milioni 78

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Sightsavers Tanzania Gospert Katunzi akimkabidhi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo mashine ya uchunguzi wa uwoni baada ya kufungua kambi ya uchunguzi wa macho katika kijiji cha Uroa Mkoa Kusini Unguja. (kushoto) Mbunge wa Jimbo la Chwaka Bangwanji Mensuria Mshamba ambae alifanikisha kambi hiyo.

 

Dkt. Abdulrahaman Abdalla wa Kitengo cha macho cha Mikunguni akimfanyia uchunguzi wa macho mwanafunzi Hafsa Suleiman Ali katika kambi ya uchunguzi wa macho Kijiji cha...

 

2 years ago

Mwananchi

Ubalozi wa Norway wafafanua safari Z’bar

Ubalozi wa Norway nchini umetoa ufafanuzi kuwa balozi wake, Hanne-Marie Kaarstad hakutembelea wala kuzungumza na viongozi wa CUF Zanzibar, bali aliyefanya hivyo ni ofisa mmoja wa ubalozi ambaye alitembelea visiwa hivyo na kuwajulia hali viongozi wa vyama vya CUF na CCM.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani