Uchunguzi shambulizi la Tundu Lissu, Familia yakinzana na CHADEMA

Familia ya Tundu Lissu imesema wao hawana mashaka na jeshi la polisi kufanya uchunguzi juu ya tukio lilomkuta ndugu yao ingawa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kikisisitiza uchunguzi ufanywe na vyombo vya kimataifa nasio jeshi la polisi.

Wakili Alute Mughwai ambaye ni kaka wa Tundu Lissu ametoa kauli hiyo huko jijini Arusha na kusema mpaka sasa wanaimani na uchunguzi unaofanywa na jeshi la polisi na iwapo familia itakaa kwa mara nyingine kuzungumzia suala hilo na kuja na kauli nyingine ya pamoja kama familia wataamua ni nani afanye uchunguzi wa tukio hilo kama kutakua na ulazima wa kufanya hivyo.

“Hatujakaa sisi kama wanafamilia kutoa msimamo wetu kuhusiana na uchunguzi wa tukio hilo, kwamba hatuna imani na jeshi la polisi na uchunguzi ufanywe na vyombo vya kimataifa lakini kama tukikutana tukawa na msimamo wetu tutatoa maoni yetu kama haja itakuwepo,” amesema Mughwai.

Hivyo amelitaka jeshi la polisi kuanzia uchunguzi wao kwa kufuatilia mkutano aliokuwa akizungumzia suala la Bombadier kukwama nchini Canada na alipozungumzia suala la kufuatiliwa na watu asiowafahamu.

Hata hivyo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jana kilisema kinahitaji serikali iruhusu wachunguzi wa kimataifa kuingia nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la kupigwa risasi kwa  Mbunge na Mwanasheria wao Tundu Lissu mnamo Septemba 7 mwaka huu mchana eneo la ‘Area D’ mjini Dodoma.

The post Uchunguzi shambulizi la Tundu Lissu, Familia yakinzana na CHADEMA appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

5 months ago

BBCSwahili

Chadema chakosoa hali ya uchunguzi wa Tundu Lissu

Chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema kimeuliza maswali mengi kuhusu hatua zilizopigwa katika uchunguzi wa Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu ambaye mwezi uliopita alipigwa risasi

 

5 months ago

Malunde

CHADEMA: HATUNA IMANI NA UCHUNGUZI UTAKAOFANYWA NA POLISI AU SERIKALI KUHUSU TUNDU LISSU


Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara na Wakili wa kujitegemea Tanzania. Prof Abadallah Safari amesema wao kama CHADEMA hawana imani na uchunguzi utakaofanywa na jeshi la polisi au serikali kuhusu shambulio la kujaribu kumuua Mbunge Tundu Lissu.


Akizungumza na wanahabari wakati wakitoa taarifa ya kamati kuu kupitia kikao walichokaa mwishoni mwa wiki iliyopita, Prof. Safari amesema kuwa wao hawana nia mbaya ya kutaka uchunguzi kufanywa na wachunguzi wa mambo ya nje lakini hii ni kutokana jinsi...

 

2 months ago

VOASwahili

Tundu Lissu afafanua shambulizi la kutaka kumuua Tanzania

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu wa chama cha Chadema amedai kuwa kuna viashiria vyote kwamba waliomshambulia kwa risasi akiwa kazini mjini Dodoma, Tanzania, wana uhusiano na serikali.

 

3 weeks ago

Malunde

FAMILIA YA TUNDU LISSU YALIA NA BUNGE


Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), imelitaka Bunge kutoa fedha za matibabu yake kama halitaki mtunga sheria wake huyo akafukuzwe hospitalini alikolazwa.

Lissu amelazwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Luvein nchini Ubelgiji tangu mapema mwezi huu baada ya kutibiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa miezi minne.

Msemaji wa familia ya Lissu, wakili Alute Mughwai, aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa miezi ni mitano sasa Lissu hajapata stahiki...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

Familia ya Tundu lissu yailalamikia Bunge

Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), imelitaka Bunge kutoa fedha za matibabu yake kama halitaki mtunga sheria wake huyo akafukuzwe hospitalini alikolazwa. Msemaji wa familia ya Lissu, wakili Alute Mughwai, aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake kuwa miezi ni mitano sasa Lissu hajapata stahiki zake kimatibabu kama Mbunge. “Tumemaliza miezi mitano tangu kutokea kwa tukio la kushambuliwa kwa Lissu na Bunge kama taasisi limeshindwa kutoa fedha za matibabu kwa...

 

5 months ago

Malunde

FAMILIA YA TUNDU LISSU KUFANYA KIKAO KIZITO

Shangazi yake Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, Ninaa Sawa(kushoto) akiwa na mama mdogo wa Lissu, Bula Muro nyumbani kwa wazazi wa Mbunge huyo Mahambe, Ikungi Singida. Picha zote na Herieth Makwetta. ***
Siku 10 baada ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi, familia yake imezungumzia tukio na kusema mwishoni mwa mwezi huu watafanya kikao Dar es Salaam wajue nini cha kufanya.

Baba mdogo wa Lissu, Muro Sawa (79), alisema kitu ambacho...

 

5 months ago

Zanzibar 24

Kikao chafanyika ndani ya familia ya Tundu Lissu

Siku 10 baada ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi, familia yake imezungumzia tukio na kusema mwishoni mwa mwezi huu watafanya kikao Dar es Salaam wajue nini cha kufanya. Baba mdogo wa Lissu, Muro Sawa (79), alisema kitu ambacho wazazi wangefurahia ni kumwona kijana wao akirudi nyumbani akiwa mzima. “Familia tutakaa kikao kushauriana ili tujue suala hili tunalitatua vipi, lakini niiombe Serikali kumzidishia ulinzi kijana wangu. Sisi...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani