Uchunguzi wa Polisi umekamilika sakata la Mwanafunzi kupotea na kuonekana Iringa

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa ufafanuzi kuhusu kile kinachoitwa kutekwa kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Nchini TSNP, Abdul Nondo.

Akizungumza na Wandishi wa Habari Kamanda wa polisi  Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa amesema mnamo Machi 7, mwaka huu walipokea taarifa kutoka kwa wenzao wa Iringa ambapo walithibitisha kupatikana kwa mwanafunzi huyo akiwa mzima huku akiwa hajaripoti kituo chochote cha Polisi.

Mambosasa amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalumu kwa...

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Zanzibar 24

Polisi wazungumzia sakata la Mwanafunzi kupotea na kupatikana Iringa

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limeeleza kuwa limefungua jalada la uchunguzi ili kubaini ukweli kama Mwenyekiti wa  Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Omari Nondo alikuwa ametekwa au la ili liweze kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire akiongea na waandishi wa habari ameeleza kuwa bado uchunguzi dhidi ya tukio hilo unaendelea ili waweze kubaini kama ni kweli ametekwa na kuwakamata wahusika kwa ajili ya kuwachukulia hatua zaidi za...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Lissu mikononi mwa polisi kwa sakata la kupotea Ben Saanane

Mbunge na Mwanasheria wa CHADEMA,Tundu Lissu anashikiliwa na Jeshi la Polisi kufuatia sakata la kupotea kwa Ndg. Ben Saanane.
Lissu amesema anashikiliwa na Polisi kufuatia mkutano wake na waandishi wa habari akiongelea sakata la Ben Saanane.

Tarehe 14 Desemba mwaka huu, Lissu alizungumza na waandishi wa habari akiomba vyombo vya ulinzi kusaidia kupatikana kwa kiongozi huyo.

The post Lissu mikononi mwa polisi kwa sakata la kupotea Ben Saanane appeared first on Zanzibar24.

 

1 year ago

Malunde

RIPOTI YA UCHUNGUZI KIFO CHA MWANAFUNZI ALIYEPIGWA RISASI NA POLISI YAZUA TAFRANI MUHIMBILI


Ndugu wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi, jana walisusia kwa muda kuchukua mwili wa binti huyo wakishinikiza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kueleza sababu za kifo chake.


Jambo hilo lilizua sintofahamu kabla ya kutulizwa kwa kuelezwa kwa mdomo na madaktari kuwa alipigwa risasi kichwani.

Jana asubuhi, ndugu hao walikusanyika katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili wakisubiri uchunguzi ukamilike ili...

 

5 years ago

CloudsFM

POLISI IRINGA YASEMA MWANAFUNZI WA RUCO ALIKUWA ANATEMBEA HUKU MWILI UKIWAKA MOTO

Mwili wa Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College - RUCO) umesafirishwa jana kuelekea mkoani kwao kilimanjaro kwa mazishi.Wanafunzi kadhaa wa chuo hicho na baadhi ya wananchi wa manispaa ya Iringa waliogusa na tukio hilo walijitokeza katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako shughuli ya kuuga mwili huo ilifanyika.Jeshi la Polisi mkoani iringa linawashikilia watu wanne...

 

5 years ago

Michuzi

JESHI LA POLISI IRINGA WALAKAMATA WATUHUMIWA WA MWANAFUNZI ALIYECHOMWA MOTO, MWILI WAKE WAAGWA LEO


Marehemu Daniel Anael Lema enzi za uhai wake

Mwili wa Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College - RUCO) umeagwa leo na kusafirishwa kuelekea mkoani kwao kilimanjaro kwa mazishi.Wanafunzi wa chuo hicho na wananchi wa manispaa ya Iringa walioguswa na tukio hilo walijitokeza katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako shughuli ya kuuga mwili huo ilifanyika.Jeshi  la Polisi...

 

5 years ago

CloudsFM

POLISI AMRUBUNI MWANAFUNZI KUFANYA NAYE MPENZI,AMWACHA CHUMBANI KWAKE,NYUMBA YAKE YAUNGUA MOTO,MWANAFUNZI AFARIKI DUNIA

Wananchi wa Mlangali, Ludewa wakiwa wamekizingira kituo cha polisi Mlangali mara baada ya kuipeleka maiti ya mtoto aliyeteketea kwa moto katika kituo hicho.KIONGOZI wa mbio za mwenge Kitaifa awatuliza wananchi wa Mlangali wilaya ya Ludewa ambao baadhi yao waliandamana kituo cha polisi kushinikiza kutolewa kwa askari polisi aliyedaiwa kusababisha kifo cha mtoto ili auwawe.Kiongozi huyo aliwaomba wananchi wa Mlangali kutokubali kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na...

 

2 years ago

Malunde

KISHINDO KIKUBWA UCHUNGUZI SAKATA MCHANGA WA MADINI

NI kubwa kuliko. Ndivyo unaweza kusema baada ya Rais Dk. John Magufuli kulazimika kuagiza zaidi ya vigogo 10 wahojiwe na vyombo vya dola kuhusu ushiriki wao wa namna mbalimbali, ikiwamo kusaini mikataba ya madini na kuisababishia nchi hasara ya Sh trilioni 108.46 za mapato ya Serikali.
Vigogo hao ambao ni mawaziri watano wa zamani wa Nishati na Madini (akiwamo marehemu Abdallah Kigoda), wanadaiwa mbali na kusaini mikataba hiyo, pia kwa nyakati tofauti wakiwa katika nyadhifa zao, waliifanyia...

 

2 years ago

Mwananchi

Timu yakamilisha uchunguzi sakata la pacha Temeke

Timu iliyoundwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuchunguza tuhuma za wizi wa mtoto pacha katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke, imekamilisha kazi yake.

 

2 years ago

Mwananchi

Timu ya Waziri Ummy yaanza uchunguzi sakata la mapacha

Dar es Salaam. Timu maalumu iliyoundwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kufanya upya uchunguzi wa tuhuma za wizi wa mmoja wa watoto pacha katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke, imeanza kazi hiyo.

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani