Ukweli kuhusiana na wenye vyeti feki kwenye Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi nchini limekanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwahusisha askari wake kuwepo katika majina ya vyeti feki na kusema taarifa hizo ni za uongo na wala hazijatolewa na Jeshi hilo. Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, ACP Advera Bulimba na kusema wanaendelea kumtafuta mtu aliyesambaza taarifa hiyo kwa lengo la kupotosha umma ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake na kuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia...

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Global Publishers

Jeshi la Polisi: Vyeti feki vyawaondoa askari kazini ni uzushi

Polisi_1_-_Msemaji_Msaidizi_wa_Jeshi_la_Polisi_Nchini_ASP_Advera_Senso_akitoa_ufafanuzi_kwa_waandishi_wa_habari_hawapo_pichani-e1427469063120Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera John Bulimba – SSP.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kutoa taarifa za uzushi na uongo kutumia majina ya taasisi, mashirika ya umma na ofisi za Serikali na kueneza taarifa hizo katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kupotosha wananchi.

Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na taarifa kuhusu Jeshi la Polisi iliyosambazwa jana katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari...

 

3 years ago

Global Publishers

Jeshi Linawasaka Walioeneza Uzushi Kuhusu Vyeti Feki vya Polisi

Msemaji-wa-Jeshi-la-Polisi-Advera-John-BulimbaMsemaji wa Jeshi la Polisi,  SSP-Advera John Bulimba.

Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kutoa taarifa za uzushi na uongo kutumia majina ya taasisi, mashirika ya umma na ofisi za Serikali na kueneza taarifa hizo katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kupotosha wananchi.

Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na taarifa kuhusu Jeshi la Polisi iliyosambazwa jana katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari ‘chujio Jesho la polisi, vyeti feki vyawaonndoa askari...

 

2 years ago

MillardAyo

VIDEO: Polisi wana mpango huu kwa wale wenye vyeti feki maofisini

jaj

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa watatu wakazi wa buguruni kwa kosa la kukutwa na nyaraka bandia za serikali kama vyeti vya kidato cha nne, stika za SUMATRA, vyeti vya vyuo vya uuguzi, vyeti vya kuzaliwa, leseni bandia za biashara, nyaraka za bima pia walikutwa na mihuri mbalimbali ya ofisi […]

The post VIDEO: Polisi wana mpango huu kwa wale wenye vyeti feki maofisini appeared first on millardayo.com.

 

5 months ago

Malunde

KUHUSU WALIOFUKUZWA KWA VYETI FEKI, WENYE VYETI VYA DARASA LA 7

HATIMA ya mafao ya wafanyakazi wa serikali walioondolewa kwenye ajira kutokana na kubainika kuwa na vyeti feki itajulikana kabla ya Bunge la Bajeti, imefahamika.

Hatua hiyo inatokana na serikali kujibu hoja nane za Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) na kwamba suala la kulipwa au kutolipwa haki zao litafahamika Machi au Aprili, mwaka huu.

Hoja zingine ni ajira ya waliomaliza darasa la saba, kupandishwa madaraja, madeni ya wafanyakazi, nyongeza za mishahara, kutofanyika vikao...

 

1 year ago

Malunde

HOFU YA VYETI FEKI : MATANGAZO YA KUPOTELEWA VYETI KWENYE MAGAZETI YAFURIKA

MATANGAZO ya upotevu wa vyeti yameongezeka katika magazeti mbalimbali na kwa siku ya jana pekee yalikuwapo 90.

Kitendo cha matangazo hayo kuongezeka kimeibuka ikiwa imebaki siku moja kwa baadhi ya watumishi wa Serikali wanaodaiwa kuwa na vyeti feki kutakiwa kukamilisha mchakato wa kukata rufaa.

Taarifa ya watumishi hao, ambao ni miongoni mwa 9,932 kutakiwa kukata rufaa ilitangazwa wiki iliyopita na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,...

 

4 years ago

Mwananchi

Wenye vyeti feki wakaangwa bungeni

Wabunge juzi jioni walichachamaa wakitaka mawaziri na wabunge wanaohusishwa na vyeti feki kulithibitishia Bunge juu ya uhalali wa vyeti vyao.

 

2 years ago

Mtanzania

Wenye vyeti feki waambiwa wajisalimishe

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

WAKATI msako wa watumishi hewa ukiwa umeshika kasi nchini, Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limewataka watu wote wanaojijua wazi kuwa wanamiliki vyeti bandia kujisalimisha wenyewe.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Charles Msonde, alitoa tangazo hilo jana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo pia alitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita na ya ualimu.

“Necta ndiyo yenye dhamana ya kutoa vyeti vyote vya watahiniwa...

 

2 years ago

Mtanzania

Panga la mwisho wenye vyeti feki

necta*Necta sasa yatangaza kuwafuata kwenye vituo vyao vya kazi

*Yatoa ratiba ya kupita mkoa kwa mkoa, itakagua cheti cha kidato cha nne, sita na ualimu

 

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

HATUA ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kutoa ratiba ya kufanya uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne, sita na ualimu kwa watumishi wote wa umma sasa ni wazi imezidi kupandisha joto kwa vigogo na watumishi mbalimbali ambao hawana sifa za kielimu kushika nafasi walizo nazo.

Katika taarifa yake ya sasa Baraza la...

 

1 year ago

Mwananchi

Wenye vyeti feki wapata ahueni

Watumishi waliobainika na vyeti feki na wanaonaweonewa wamepewa fursa ya kukata rufaa kwenda wizara ya utumishi.

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani