USIRI WATAWALA YANGA NA SIMBA, KUVAANA LEO USIKU UWANJA WA AMAAN, ZANZIBAr


Na Zainab Nyamka, 
Globu ya Jamii, ZanzibarIKIWA imebakia masaa machache kufikia mtanange wa watani wa jadi kuelekea nusu fainali ya kombe Mapinduzi, viongozi wa timu hizo mbili wamegoma kuzungumza na vyombo vya habari na zaidi wakisema mpira ni dakika 90.Wakati  Simba wakiingia msituni wakitoka pale walipokuwa wanakaa toka kuanza kwa mashindano haya, Yanga wameendelea kusalia pale pale huku wakiwaficha wachezaji wao na kuamua kufanya mazoezi usiku kwenye Uwanja wa Amani.Mashabiki wa pande zote mbili wamejinadi kuweza kuondoka na ushindi katika mchezo huo huku kwa upande wa Simba wakijiamini zaidi wakiwa na imani na kikosi chao kwa kuweza kupata matokeo mazuri zaidi, Yanga wakiwa na uchungu wa kupoteza katika mchezo wao wa hatua ya makundi dhidi ya Azam.Mechi hiyo ya nusu fainali ya watani wa jadi itapigwa leo majira ya saa 2:15 katika uwanja wa Amaan. Kabla ya mchezo huo kutakuwa na nusu fainali ya kwanza kati ya Azam na Taifa Jang'ombe. 
Jang’ombe inakutana na Azam FC katika mchezo leo  Jumanne saa 10.15 jioni, hapo hapo Amaan, baada ya kumvua taji bingwa mtetezi wa michuano hiyo, URA ya Uganda kwa kuifunga bao 1-0 katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi A.Mara ya mwisho Azam FC kukipiga na Jang’ombe ilikuwa ni Julai 31 mwaka jana kwenye mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu huu, ambapo mabingwa hao wa Ngao ya Jamii walishinda bao 1-0 lililowekwa kimiani kiufundi na mshambuliaji aliyekuwa katika majaribio Mburundi Fuadi Ndayisenga.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Vijimambo

YANGA NI MWENDO WA NNE TU UKISOGEA UNAZO UWANJA WA AMAAN, ZANZIBAR, LEO.

COUTINHO AKISHANGILIA BAADA YA KUFUNGA BAO KWENYE UWANJA WA AMAAN, ZANZIBAR, LEO. Yanga sasa haikamatiki kwani ukiwasogelea, unakula zako nne.
Baada ya kuitwanga Taifa ya Jang'ombe kwa mabao 4-0 katika mechi ya Kombe la Mapinduzi, wamefanya hivyo tena kwa Polisi Zanzibar.
Katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Yanga ilipata mabao yake kupitia Andrey Coutinho aliyefunga mawili, Kpah Sherman na Simon Msuva.
Yanga ingeweza kufunga mabao mengi zaidi kutokana na kuutawala mchezo,...

 

3 years ago

Michuzi

Mchezo wa Kirafiki Kati ya Simba na Polisi Usiku Huu Uwanja wa Amaan Simba Ikiwa mbele kwa bao 2--0

Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdan akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Polisi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan.Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdan akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Polisi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan.
Kikosi cha timu ya Polisi Zanzibar kilichokubali kipigo cha bao 2--0 kutoka kwa timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

 

1 year ago

Zanzibar 24

Simba SC yaendelea mazoezi uwanja wa Amaan Zanzibar

Timu ya Simba leo asubuhi imeendelea kufanya mazoezi katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar kwa kujiandaa na mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya watani wao wa jadi Yanga unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 

Simba wapo hapa Unguja tangu juzi Ijumaa na wanatarajia kuondoka Visiwani Ijumaa ijayo ambapo walianza mazoezi yao jana asubuhi katika uwanja huo wa Amaan na leo wakiendelea tena asubuhi kuanzia 3:00 hadi 5:00 ambapo kuanzia kesho Jumatatu wanatarajia...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Yanga yaomba kutumia uwanja wa Amaan Zanzibar

YANGA SC imeomba kutumia Uwanja wa Amaan, Zanzibar kwa mechi zake mbalimbali za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Taarifa ya Kaimu Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit imesema kwamba hatua hiyo inafuatia Serikali kuizuia klabu hiyo pamoja na mahasimu wao, Simba SC kutumia Uwanja wa Taifa.
Yanga imeiandikia barua Wizara ya Habari Utakii na Michezo Zanzibar kuomba kuhamia Uwanja wa Amaan, baada ya kufungiwa kwa Uwanja wa Taifa.

50

The post Yanga yaomba kutumia uwanja wa Amaan Zanzibar appeared...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Meneja uwanja wa Amaan Zanzibar afurahishwa na maombi ya Yanga

Meneja wa Uwanja wa Amaan Simai Mohd Mavune amefurahishwa na taarifa za Klabu ya Yanga kuomba kuutumia uwanja wa Amaan kwa mashindano mbalimbali ambayo inashiriki ikiwemo ligi kuu Tanzania bara pamoja na Mashindano mengine.

Simai amesema taarifa hizo yeye kama Meneja wa Uwanja huo bado hazijamfika kwasababu ya utaratibu unaanzia juu ngazi ya Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo, lakini taarifa hizo ni njema kwake kwani watafaidika kwa ujio wa timu hiyo.

“Izo taarifa za Yanga kuutaka...

 

3 years ago

Michuzi

NEWS UPDATES KUTOKA CCM DODOMA USIKU HUU: USIRI WATAWALA TANO BORA YA WAGOMEA WA CCM

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari usiku huu nje ya ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma, mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokaa kupitisha majina matano ya wagombea Urais yatakayopelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM kujadiliawa hapo saa nne asubuhi. Nape hakutaja majina ya wagomea hao waliopita kwenye tano bora, kwa kuseka atataja asuhuhi. Muda mfupi baada ya Katibu wa NEC,...

 

3 years ago

Michuzi

Ligi Kuu ya Zanzibar: Shaba na Chuoni bao 1-1 uwanja wa Amaan leo

Mashabiki wa timu ya Shaba wakishangilia timu yao wakati ikicheza na timu ya Chuoni katika uwanja wa Amaan, jioni leo na katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 1--1.Mchezaji wa timu ya Shaba akiondoa mpira golini kwake wakati wa mchezo wa ligi kuu ya grand malt mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan.

 

2 years ago

Dewji Blog

Simba SC vs Azam FC uwanja wa Uhuru Dar, Yanga vs Mwadui uwanja wa Kambarage hapatoshi leo

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2016/2017 inatarajiwa kuendelea tena leo Jumamosi Septemba 17, 2016 kwa michezo sita ambayo itazikutanisha timu pinzani 12 katika viwanja sita tofauti.

Michezo ya leo ni Mwadui FC itakayoikaribisha Young Africans kwenye Uwanja wa CCM Kambarage. Mwadui ambayo inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Stand United wakati Young Africans ina makali ya kuilaza Majimaji ya Songea mabao 3-0.

Mechi nyingine yenye mvuto...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani