UVCCM yawashauri wapinzani kutoubeza Utendaji wa Rais Magufuli

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM umevishauri vyama vya upinzani hususani UKAWA kutobeza utendaji wa Rais wa awamu ya tano Dokta John Magufuli na badala yake wamuunge mkono kwa maendeleo ya nchi.

vlcsnap-2016-05-19-11h46m55s165

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhamasihaji Sera, Utafiti na Mawasiliano wa UVCCM Abubakar Asenga alipozungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam.

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wamesema siasa za kupinga maendeleo kwa sasa hazina nafasi kwa maendeleo ya Taifa na badala yake wamewashauri wanasiasa hao kuwatumikia wananchi na kuiunga mkono Serikali iliyoko madarakani.

Abubakar Asenga ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhamasihaji Sera, Utafiti na Mawasiliano UVCCM amesema wanasiasa waache tabia ya kutafuta umaarufu na badala yake wamuunge mkono Rais Magufuli katika utekelezaji wa sera zake.

Akizungumzia Bunge linaloendelea mjini Dodoma, Asenga amewataka wabunge wanaotoa hoja kuzipima vyema na kuzikumbuka na pia Amewahimiza kupeleka maendeleo katika majimbo yao kama wajibu wao kikatiba.

Asenga amesema, UVCCM itaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli  pamoja na kumuunga mkono kasi yake ya kushughulikia wafanyabiashara wa dawa za kulevya  pamoja na wabadhilifu wa mali za umma .

StarTV

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Mwananchi

Wapinzani wapongeza utendaji wa Magufuli

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari amemshauri Rais John Magufuli kuipitia upya mikataba ya madini na kuifanyika marekebisho ili kuboresha maisha ya Watanzania.

 

5 months ago

Habarileo

UVCCM Manyara wakoshwa na utendaji wa Magufuli

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Manyara umempongeza na kumwomba Rais John Magufuli kuendelea na kazi nzuri anayoifanya ya kujenga nchi bila kurudi nyuma.

 

1 year ago

StarTV

Utendaji Wa Rais Magufuli wawafanya Wakenya kutamani awe Rais wao

Raia wa Kenya wamewataka Watanzania kutoa ushirikiano kwa Rais Dokta John Magufuli katika juhudi zake ya kupambana na Ufisadi na Ubadhilifu wa mali za umma anazoendelea kuzichukua tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba tano mwaka huu.

Wakenya hao wamesema kimsingi hata wao wanatamani kuwa na Rais  kama Dokta Magufuli kwa sababu ameonesha kuwa ni Mzalendo anayeipenda nchi yake na anayepigania maslahi ya wananchi masikini ambao kwa miaka kadhaa wamekosa fursa ya...

 

7 months ago

Bongo5

Lowassa azungumzia utendaji wa Rais Magufuli

Aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Edward Lowassa, amesema licha ya kukubali kazi za Rais John Magufuli, yapo maeneo ambayo yana mapungufu.

edwardlowassa-1024x1024

Ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na ripota wa BBC mjini Nairobi na aliweza kujibu maswali kadhaa. Moja ya maswali hayo ni pamoja na anavyouchukulia utendaji wa Dkt Magufuli.

“Kuna maeneo anafanya vizuri, kuna maeneo ambayo naamini tungefanya vizuri zaidi, hili niishie hapo, anafanya vizuri kiasi gani...

 

1 year ago

Habarileo

UVCCM yampa tano Rais Magufuli

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema unaunga mkono kasi ya utekelezaji kazi wa serikali ya awamu ya tano, chini ya Rais John Magufuli na kwamba anachofanyika sasa ndio kiu ya Watanzania.

 

8 months ago

Bongo5

UVCCM: Tutaandamana kumpongeza Rais Magufuli

Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umetangaza kufanya maandamano nchi nzima Agosti 31 mwaka huu, ikiwa ni siku moja tu kabla ya tarehe iliyotangazwa na Chadema kufanya maandamano na mikutano nchi nzima.

UVCCM

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu amesema lengo la maandamano yao ni kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya tangu alipoingia madarakani.

“Maandamano yetu ni ya amani, na tayari tumeshatoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi kama taratibu...

 

3 years ago

Tanzania Daima

UVCCM yasifu utendaji wa Dk. Shein

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), imepongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kufikia malengo ya milenia. Pongezi hizo, zilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani