Vijana Waaswa Kulinda na Kudumisha Muungano


Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma

Vijana Nchini wametakiwa kulinda na kudumisha Muungano kwa Vitendo kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho ikiwa ni sehemu ya kuonesha uzalendo.

Akizungumza wakati wa Kongamano lililofanyika mkoani Dodoma kuhusu Muungano lililowashirikisha wanafunzi zaidi ya 300 wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba amesema kuwa vijana wanalo jukumu kubwa katika kulinda Muungano na kuudumisha.

“Vijana tunawategemea muwe watetezi na walinzi wa Muungano wetu kwa kuwa huu ni urithi wa Taifa tunawajibika kuulinda na kuudumisha kwa faida ya kizazi hiki na kijacho” Alisisitiza Makamba. Akifafanua Makamba amesema kuwa vijna wanaowajibu wakuonesha uzalendo wao kwa kudumisha Muungano ambao unalitambulisha taifa nje ya mipaka yetu.

Mambo mengine yanayolitambulisha Taifa letu ni Lugha, Mipaka yetu, Historia, Utamaduni wa kisiasa na kijamii.“ Waasisi wa Taifa letu walikuwa na dhamira njema ndio maana waliasisi Muungano wetu na kuweka mipaka mipya ya Taifa letu tofauti na ile ya wakoloni hivyo hili ni jambo la kujivunia” Alisisitiza Mhe. Makamba.

Aliongeza kuwa vijana wanapaswa kuwapuuza wale wote wanaobeza Muungano kwa kuwa hawalitakii mema taifa letu.Kwa upande wake mwanasiasa mkongwe na Waziri (mstaafu) wa baraza la kwanza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Kwanza mara baada ya Uhuru Balozi Job Lusinde akizungumza katika mahojiano maalum mjini Dodoma amewaasa vijana kudumisha Muungano kwa kujifunza historia ya Muungano ili waweze kushiriki kikamilifu katika kuuenzi.

“Vijana wajitahidi wawe waadilifu kwa kulinda uhuru wetu, umoja wetu na muungano wetu kwa faida ya kizazi hiki na kijacho” Alisisitiza Balozi Lusinde.

Akifafanua Balozi Lusinde amesema vijana wanapaswa kuepuka vitendo vya wizi na ufisadi ili kuchochea maendeleo.Mada zilizotolewa katika Kongamano hilo ni pamoja na Historia na faida za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mtazamo wa Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.

Kongamano kuhusu Muungano limefanyika Mkoani Dodoma ikiwa ni siku chache kabla ya maadhimisho ya siku ya Muungano yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26, 2018 mjini Dodoma, Kongamano hilo limewahusisha wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma, Mipango, CBE, St. John, Chuo cha Madini na Chuo cha Maendeleo Vijijini Hombolo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

1 month ago

Michuzi

Vijana Waaswa Kulinda na Kudumisha Muungano


Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma


Vijana Nchini wametakiwa kulinda na kudumisha Muungano kwa Vitendo kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho ikiwa ni sehemu ya kuonesha uzalendo.
Akizungumza wakati wa Kongamano lililofanyika mkoani Dodoma kuhusu Muungano lililowashirikisha wanafunzi zaidi ya 300 wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba amesema kuwa vijana wanalo jukumu kubwa katika kulinda Muungano na...

 

4 years ago

Habarileo

Waaswa kudumisha moyo wa muungano

 Samia Suluhu HassanWATUMISHI waliostaafu katika Ofisi ya Makamu wa Rais wametakiwa kuendelea na moyo wa kuudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na uhifadhi wa mazingira.

 

4 years ago

Michuzi

Watanzania waaswa kudumisha na kuuenzi muungano.


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Job Ndugai .
(Na Jovina Bujulu, MAELEZO DODOMA).   Muungano wa Tanzania bara na Zanzibar ni jambo la kujivunia kwa watanzania wote na katika bara la Afrika.
Hayo yamesemwa leo na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Job Ndugai wakati wa mahojiano katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha TBC ONE.
Mh. Ndugai ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema kuwa jambo la Muhimu...

 

4 years ago

Michuzi

VIJANA WAASWA KUDUMISHA AMANI

 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma akimvisha kofia ya ukamanda Profesa Peter Msolla baada ya kuteuliwa kuwa Kamanda wa UVCCM wilaya ya Kilolo sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kidabaga.  Mbunge wa jimbo la Kilolo,Profesa Peter Msola akila kiapo cha kuwa kamanda wa UVccm mbele ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma. Mbunge wa jimbo la Kilolo,Prof Peter Msola akiwaapisha makamanda wa vijana ccm katika wilaya ya Kilolo sherehezz ilizofanyika katika uwanja wa Kidabaga.
Na...

 

2 years ago

Dewji Blog

Watanzania waaswa kudumisha amani iliyopo nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa watanzania kudumisha amani iliyopo ambayo ilipatikana baada ya Mashujaa mbalimbali kuipigania na hata kujitoa uhai wao kwa ajili ya Taifa.

Akizungumza leo, wakati akihutubia wananchi mara baada ya kumaliza shughuli za maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa  iliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma.

Rais Magufuli alisema kuwa maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa  ni muhimu kwa...

 

12 months ago

Michuzi

WASHIRKI WA UMISETA MKOANNI RUVUMA WAASWA KUDUMISHA NIDHAMU

Vijana wa shule za sekondari wanaoshiriki UMISETA mkoa wa ruvuma wametakiwa kudumisha nidhamu wawapo uwanjani ili waweze kufikia malengo yao. Wito huo umetolewa na afisa elimu mkoa wa ruvuma GHARAMA KINDERU wakati wa kufungua michezo hiyo ili kuweza kupata timu itakayo wakilisha mkoa wa ruvuma katika michuano ya UMISETA inayotarajia kufanyika jijini mwanza mwezi juni mwaka huu

 

4 years ago

Habarileo

Mwinyi asisitiza kudumisha muungano

Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka Watanzania kuhakikisha wanadumisha na kuulinda Muungano ili kizazi kijacho kiweze kuyaona mafanikio ya Muungano huo na kuacha ukiwa imara.

 

4 years ago

Tanzania Daima

Watanzania wahimizwa kudumisha, kuuenzi Muungano

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Alhaji Mohamed Sinani, amewataka Watanzania kuendelea kudumisha na kuuenzi Muungano kwa masilahi ya taifa ikiwa ni njia pekee ya kuwaenzi waasisi...

 

4 years ago

Habarileo

Mchungaji ahimiza viongozi kudumisha Muungano

VIONGOZI nchini wamehimizwa kutimiza wajibu wao wa kutendea taifa haki kwa kudumisha Muungano, amani na mshikamano na kulipatia katiba bora, inayotokana na maoni ya wananchi.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani